MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Fadhili Maganya amewataka wanachama waache kuchafuana kuelekea uchaguzi wa ndani mwakani.
Maganya aliyasema hayo Mjini Kibaha alipokuwa akizungumza na viongozi wa Jumuiya hiyo pamoja na wanachama wa CCM Kibaha Mjini wakati wa ziara yake kutembelea Mkoa wa Pwani kukagua uhai wa chama na miradi ya maendeleo.
Alisema kuwa chama hakina shida nao bali wafuate miongozo na utaratibu wa chama kama unavyoelekeza.
"Mwakani tunaingia kwenye uchaguzi wa ndani baadhi wameanza kuchafuana tusikubali hali hiyo asitokee mtu wa kutoa maelekezo bali chama ndiyo kinatoa maelekezo,"alisema Maganya.
Aidha alisema kuwa watu wanaanza kukinzana na uchaguzi wa mwakani na unabeba taswira ya uchaguzi wa 2030 hivyo chama kitangulizwe mbele na siyo mtu.
"Tuwaacheni walioko madarakani wafanye kazi kwani muda wa uchaguzi bado watu wasubiri hadi muda utakapofika,"alisema Maganya.
Alibainisha kuwa kuna baadhi ya watu wanasiasa wa upinzani na wanaharakati wamekuwa wakibeza na kutoa lugha za maudhi na kudhalilisha wasipewe nafasi kwani wakidai eti serilali iliyopo ni haramu.
"Tusiruhusu tabia hiyo kwani Rais Dk Samia Suluhu anafanya kazi kubwa kwa kushirikiana na chama chake kwani Tume ya Uchaguzi iliita vyama vyote na kutaka visaini sheria za uchaguzi lakini baadhi vilikataa,"alisema Maganya.
Aliongeza kuwa uchaguzi ulikuwa wazi kwa kila chama na viongozi walichaguliwa kwa utaratibu uliowekwa na Tume ya Uchaguzi hivyo havina haja ya kulalamika.
"Kamati za siasa za chama zinapaswa kutatua migogoro ya ardhi kwa kushirikiana na serikali ambayo inafanya kazi kubwa kutatua migogoro hiyo,"alisema Maganya.
Naye Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya (CCM-NEC) kupitia Jumuiya ya Wazazi na Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa alisema kuwa Jumuiya imekuwa mstari wa mbele kuimarisha chama.
Jumaa alisema kuwa kwa sasa Jumuiya hiyo imeimarika sana na kuwa mhimili mkubwa wa chama katika utekelezaji wa ilani.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka alisema kuwa Jumuiya ya Wazazi imefanya kazi kubwa katika utekelezaji wa ilani.
Koka alisema kuwa kwenye uchaguzi Mkuu Jumuiya hiyo iliongoza kwa kupiga kura na kuufanya Mkoa wa Pwani kuongoza kwenye suala la kura.
Awali akitoa taarifa ya Wilaya Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Moses Magogwa alisema kuwa uptikanaji wa huduma kwa sasa kwa wananchi ni asilimia 98.
Magogwa alisema kuwa Hslmashauri ya Manispaa imekuwa ikifanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato ambapo asilimia 60 yanatokana kodi na ushuru mbalimbali wa huduma.
Alisema kuwa ujenzi wa barabara ya njia sita kutoka Maili Moja hadi Picha ya Ndege unatarajia kuanza na barabara kwa ajili ya magari ya mizigo nao utaanzia Picha ya Ndege.

No comments:
Post a Comment