Tuesday, July 21, 2026

POLISI KATA MAILIMOJA AMTEMBELEA MZEE NA KUTOA MSAADA.





Na Mwandishi Wetu, Kibaha

Polisi Kata wa Mailimoja, Mkaguzi wa Polisi, Tupilike Mwabulambo ameambatana na Stesheni Sajenti Lusekelo Mwakalinga wa Wilaya ya Kibaha kumtembelea mzee Hamisi Nampatima wa mtaa wa Uyaoni ikiwa ni sehemu ya mpango wa kuwafikia wahitaji waliopo kwenye kata yake na kutoa msaada.

Akikabidhi baadhi ya mahitaji kwa mzee huyo Julai 20, 2026 INSP Tupilike alieleza kuwa kuna makundi mbalimbali katika jamii ambao wana changamoto ikiwemo za kiusalama na mahitaji muhimu hivyo anatembelea kaya hizo kuwasikiliza na kutoa kile alichojaliwa kwa wakati huo.

Kwa upande wake Mzee Hamis Nampatima, alilishukuru Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani kwa msaada wanaompatia kwani sio mara ya kwanza kufika kwake, Mara kadhaa Sajenti wa Polisi Salum Ally wa Polisi Wilaya ya Kibaha amekua akimsaidia kwa kumpatia pesa na mahitaji mbalimbali ya nyumbani.

Naye, Mwenyekiti wa Mtaa wa Uyaoni, Katani humo, Bw. Fadhili Kindamba alipongeza Jeshi la Polisi kwa namna wanavyoshirikiana na wananchi kuimarisha ulinzi na usalama na kutatua changamoto zao zingine za kijamii.

No comments:

Post a Comment