Tuesday, July 21, 2026

MASAUNI AWATAKA WANANCHI KUTUMIA FURSA YA HEWA UKAA




Na Mwandishi Wetu, Rufiji

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhandisi Hamad Masauni amewataka wananchi kutumia miradi ya utunzaji wa mazingira ili kupata hewa ukaa na kujiongezea kipato.

Masauni aliyasema hayo Wilayani Rufiji alipokuwa akizungumza na wananchi wakati wa ziara yake Mkoani Pwani kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo.

Alisema kuwa hewa ukaaa ni jambo kubwa la kiuchumi hivyo wananchi watumie kila fursa inayogusa hewa ukaa watumie rasilimali vizuri kupitia misitu. 

"Rufiji ina fursa nyingi za uzalishaji hewa ukaa kupitia, misitu migomba mikorosho kwani hii ni biashara nzuri watumieni wataalam ili wawape moingozo ili kuongeza kipato kwa kutumia fursa hii,"alisema Masauni.

Aidha alisema kuwa mabadiliko ya tabia nchi ni chanzo cha biashara kupitia mkataba wa Paris baada ya kukubaliana nchi zenye rasilimali za kupunguza hewa ukaa zilipwe.

"Kupitia kilimo madini na faida ya kuhifadhi miti tutalipwa hiyo ni changamoto muifanyie kazi kwani mna rasilimali za kutosha za kuwa miradi ya hewa ukaa,"alisema Masauni

Aliongeza kuwa Watanzania wanapaswa kutunza amani iliyopo na kuachana na yale yanayoweza kuharibu amani ya nchi kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma.

"Kipindi cha nyuma kulitokea changamoto hata wanaccm walikuwa hawavai sare za chama lakini sasa watu wana amani hivyo tunzeni amani kwani  umuhimu wa amani unajulikana na vijana wanasababu ya kuenzi umoja na kurithisha watoto wetu na Muungano ndiyo kiungo cha amani kupitia  waasisi wa taifa letu wametuachia msingi wa amani,"alisema Masauni.

Aliipongeza Wilaya ya Rufiji kwa kutekeleza kikamilifu kupitia ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye miradi mbali mbali ya maendeleo ya elimu afya miundombinu kilimo maji.

Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani Mwinshehe Mlao alisema kuwa Wilaya hiyo imepiga hatua kubwa ya kimaendeleo ukilinganisha na zamani kupitia uongozi wa Rais Dk Samia Suluhu Hassan.

Mlao alisema kuwa kwa ujumla Mkoa umepiga hatua kubwa ya maendeleo hivyo watu wanapaswa kuona jinsi gani maendeleo yaliyopatikana chini ya CCM.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge 
alisema kuwa mwaka wa fedha Mkoa ulipangiwa kukusanya bilioni 88 lakini hadi Juni 30 mwaka huu tayari zimekusanywa bilioni 135 na kuwa mkoa wa pili baada ya Dar es Salaam. 

Kunenge alisema kuwa Mkoa unajivunia Rais kwa kuwatumikia Watanzania na Rufiji ina miradi mikubwa ya uwekezaji na moja mradi alionyesha Urusi ni kilimo cha ndizi kupitia moja ya kampuni kubwa afrika.

Alisema kuwa kwa sasa kuna mifugo mingi na kuna ranchi ndogo na uchumi usitegemee chanzo kimoja ili kuwa salama kwa kutumia bahari na utalii kwani huwezi kushindana na mabadiliko ya dunia ni kijini na dira 2050 inataka kuwa na ajira milioni nane pato la Taifa trilioni moja pato la mwnanchi milioni 18 kwa mwaka.

Akikaribisha ugeni wa Waziri Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Luteni Kanali Fredrick Komba alisema kuwa Wilaya hiyo imefanikiwa kupanda miti ya mikorosho ipatayo milioni 1.5.

No comments:

Post a Comment