Bodi ya Bima ya Amana (DIB) ikiwa na jukumu la kusimamia amana za wateja zinapokuwa kwenye mabenki endapo benki ikifilisika inaweza kumlinda mteja aliyeweka amana zake asiweze kupata hasara.
Hayo yameelezwa na mwenyekiti wa bodi ya Amana (DIB) Emmanuel Tutuba wakati akizungumza na waandishi wa habari katika banda la maonyesho ya nanenane Zuguni Jijini Dodoma huku akiwataka wananchi waliokuwa wateja wa benki zilizofilisika waweze kufika katika taasisi hiyo ili kuhakikiwa na kupewa stahiki zao.
Amesema DIB mpaka sasa imeongeza zaidi ya shilingi trilioni 1 ambazo wanaendelea kuwekeza sehemu mbalimbali ambazo fedha hizo ni za wateja endapo benki ikifilisika mteja aweze kupata gawio lake kulingana na alivyowekeza.
"Tangu kuanzishwa DIB ilipewa mtaji mwaka 1994 na benki kuu ya Taifa (BOT) walipewa kiasi cha shilingi bilioni1.5 kwa sasa wana atirioni 1.2.3 fedha hizo zinaendele kuongezeka kwa sababu wanaendelea kuwekeza sehemu mbalimbali fedha hizo zipo kwa ajiri ya kukinga amana za wateja hata kama bank ikitokea bahati mbaya ikafilisika kila aliyekuwa na account kwenye benki atalipwa kulingana na kiwango ambacho alichokuwa anaweza kulingana na kiwango cha asilimia atarejeshewa,"amesema Tutuba.
Pia ametoka wito kwa wateja wa benki FDME kama kuna mtu ajapewa mgawanyo wa asilimia 30 aweze kufika kwenye bodi ya bima ya Amana ili aweze kupatiwa utaratibu.
"Wametoa wito kwa wateja kwenye benki FDME kama kuna mtu ajapewa mgawanyo wa asilimia 30 cha awali aweze kufika taasisi hii ya bima ya amana ili aweze kupitia taratubu zote kujiludhisha Ili arejeshewa kiwango 30 Cha awali." Amesema Tutuba.
Aidha Tutuba hakusita kueleza mfano wa faida ya mfuko huo unaosimamiwa na DIB kupitia mfano wa zile benki ambazo zilizowahi kufilisika nchini.
Amewapongeza kusimamia shughuli zao za kusimamia amana za wateja na cha msingi DIB kazi yake ni kuweka na kuendelea kuwekeza bima ili kukinga viatarishi ambavyo vitajitokeza endapo benki itafilisika, pia kuna baadhi ya watu ambao benki zao zilifilisika mwanzano wanatakiwa wafiki DIB" Amesema Tutuba.
No comments:
Post a Comment