Na Wellu Mtaki,Dodoma.
Wakala wa Usajili wa biashara na leseni (BRELA) imeweka mfumo wa kujisajili katika mtandao ambao utazuia mteja kuacha kutumia mtu ambaye atasimamia katika usajili ambao utamfanya mteja kulipa kiasi cha ziada tofauti na malipo ambayo yamewekwa na BRELA
Hayo yameelezwa leo tarehe 6 Agost 2024 na Msaidizi wa Usajili Yvonne Massele wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya nanenane Zuguni Jijini Dodoma huku akiwataka wananchi kutembelea banda la Brela ili kutambua huduma zinazopatika katika banda hilo.
Massele amesema kuwa mfumo wa usajili wa Brela kwa njia ya Mtandao unamsaidia mteja kurahisisha usajiri kwa mteja ambaye yupo mbali na huduma.
"Sasa hivi tunajisajiri kwa njia ya mfumo na ukiingia kwenye Mfumo unaweza kupata naomba ya malipo ( control number) na kama mteja atapata changamoto Kuna mawasiliano ambayo atawasiliana na mtoa huduma moja kwa moja,"amesema Massele.
Aidha ameelaza kuwa huduma ambazo zinatolewa katika maonesho ya nanenane ni pamoja na usajili wa kampuni, usajili wa biashara, usajili wa harama za biashara, huduma pamoja na kutoa leseni ya biashara jina la kampuni kwa siku hiyo hiyo uliofika kujisajili.
"Ujio wao ni kwa ajili wa kutoa huduma zetu za Brela ambazo zinafanyika ni usajiri wa kampuni, usajili wa biashara , usajili wa harama za biashara na huduma pamoja na kutoa leseni la biashara la kundi A pamoja na leseni za viwanja,"amesema Massele
Pia amesema kuwa wanaendelea kutoa Elimu kwa wafanyabiashara wadogo na wakubwa ili waweze kutambua namna ya kusajili biashara zao kwa wale ambao bado hawajasajili
"Tumekuja kutoa Elimu kwa wafanyabiashara wadogo wadogo ambao awajasajili biashara waweze kusajili biashara zao na wale ambao biashara zao zishakuwa waweze kusajiri majina ya Kampuni " amesema
No comments:
Post a Comment