Monday, August 5, 2024

BRELA KUANZA KUSAJILI WAKULIMA

Na Wellu Mtaki, Dodoma

OFISA Usajili wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Gabriel Gilangay amesema wakala huo umejipanga kuanza kuwasajili  Wakulima kwa kuwapa nembo ambayo itawatambulisha kibiashara. 

Gilangay amesema hayo Jijini Dodoma kwenye maonesho ya Wakulima Nanenane wakati akizungumza na Waandishi wa habari na kueleza kuwa Wakala huo unashughulikia mambo mengi  kwa wakulima nchini ikiwemo usajili wa Biashara. 

Mbali na hayo amesema  BRELA hutoa huduma hizo ili kuhakikisha  biashara za kilimo zinakubalika kisheria ikiwa ni pamoja na kutoa huduma za ushauri kuhusu jinsi ya kufuata taratibu za kisheria katika biashara ya kilimo, ikiwa ni pamoja na kanuni za usajili, sheria za biashara, na masharti ya leseni.

Kwa upande mwingine Wakala huo hushughulikia Kampuni za Umma,Kampuni zinazoshiriki soko la hisa,Kampuni za Kibinafsi na Kampuni zinazomilikiwa na watu wachache.

No comments:

Post a Comment