Na John Gagarini, Chalinze
UONGOZI wa Mradi wa maji wa Wami
Chalinze wilayani Bagamoyo umetakiwa kutoa taarifa juu ya ukosefu wa maji ambao
kwa sasa umedumu takribani mwezi mzima ambapo baadhi ya wanasiasa wa vyama vya
upinzani wapotosha ukweli kuhusu tatizo hilo.
Hayo yalisemwa na diwani wa kata ya Bwilingu
Nassa Karama katika viwanja vya Masoko wakati mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani
Kikwete alipokwenda kusikiliza kero za wananchi wa kata hiyo.
Karama alisema kuwa maji kwa sasa ni
kilio kikubwa kwa wakazi wa mjin huo huku
wao wakiwa hawana utaalamu wa kujua tatizo la ukosefu wa maji linatokana na nini
hivyo kushindwa kuwapa majibu sahihi wananchi ambapo hali hiyo imesababishwa
ndoo kuuzwa kwa shilingi 700 kutoka shilingi 200.
“Suala la kutotoka kwa maji ni la
kitaalamu na wahusika wa mradi wa maji wa Wami Chalinze wanapaswa kutoa taarifa
juu ya changamoto zinazosababisha ukosefu wa maji ili majibu yasitolewe na
wanasissa ambao wanatumia fursa hiyo kupotosha ukweli wa tatazi hilo,” alisema
Karama.
Alisema kuwa wananchi wanapata usumbufu
mkubwa kwani kwa sasa wananunua maji kwa baadhi ya watu wenye magari ya kuuza
maji ambapo kabla ya tatizo hilo walikuwa walikuwa wakinunua kwa sh.200 na sasa
ni sh.700 hali inayosababisha kuwapa wakati mgumu baadhi ya wananchi ambao
baadhi yao kipato chao ni cha chini.
“Baadhi ya wanasiasa hao wanapotosha
kwa wananchi kuwa kuna mashine mbalimbali za kukamilisha mradi huo zimeuzwa
Nairobi nchini Kenya jambo ambalo linachanganya wananchi na kuleta tafsiri
tofauti kutokana na tatizo hilo,”
alisema Karama.
Aliutaka uongozi wa maradi kuo kutoa
taarifa juu ya ukosefu wa maji ili kutowapa mwanya wanasiasa wenye nia ya kutumia jambo hilo kama mtaji wao
wa kisiasa.
Naye Mbunge wa Jimbo la Chalinze
Ridhiwani Kikwete akijibu kuhusiana na maswali hayo alisema anafanya taratibu
ya kumpeleka waziri wa maji ili aweze kwenda kutembelea maeneo yenye kero kubwa
jimboni humo kujionea hali halisi ya ukosefu wa maji.
Ridhiwani alisema kuwa tatizo kubwa la
ukosefu wa maji linatokana na tope linaloingia katika mitambo hali
inayosababisha maji kushindwa kutokana ambapo kwa sasa wamenunua chujio kwa
ajili ya kuchuja uchafu ambao umekuwa ukiziba na maji kushindwa kutoka.
Aliwataka wanasiasa kuacha kupotosha
ukweli kwani si jambo zuri kupotosha wananchi na kuwataka wataalamu
kujenga tabia ya kutoa taarifa ya vikwazo vilivyopo ili wananchi wajue.
Mwisho.
Na John Gagarini, Fukayosi
BAADHI ya viongozi wa Kijiji cha Kidomole wilayani
Bagamoyo mkoani Pwani waliohusika kuuza ardhi ya Kijiji hicho kinyume cha
sheria wametakiwa kujiandaa kusimama kwenye vyombo vya sheria kujibu tuhuma
hizo.
Viongozi hao kwa wameuza eneo kubwa la
Kijiji ambapo wananchi wa maeneo hayo wanatakiwa kuondoka na kumpisha mununzi
huyo ambaye amechukua eneo kubwa la kijiji.
Akizungumza na wananchi wa Kijiji hicho
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete, wakati wa ziara ya kutembelea na
kukagua shughuli za maendeleo alisema viongozi hao lazima wachukuliwe hatua za
kisheria kwa ukiukaji wa maadili ya uongozi.
“Inashangaza
kuona mtu anakuja na risiti na kusema kuwa kanunua eneo lote la Kijiji na
wananchi wanatakiwa kuondoka kumpisha eti mwekezaji jambo kama hili
haliwezekani kwani taratibu haziruhusu na viongozi waliofanya hivi wajiandae
kwa kukimbilia tutapambana nao ili haki ya wananchi ipatikane,” alisema
Ridhiwani.
Alisema kuwa
hatakuwa tayari kuona wananchi hao wanaondolewa kwani sheria za ardhi
haziruhusu kuuza eneo la Kijiji zaidi ya hekari 50 zaidi ya hapo lazima suala
hilo lipelekwe kwa kamishana wa ardhi.
“Inashangaza
kusikia kiongozi kauza hekari zaidi ya 100 kwa mwekezaji sheria haisemi hivyo hata
hizo hekari 50 lazima wanakijiji waridhie kwa kufanya mkutano mkuu ili
kumpitisha muombaji lakini siyo watu wawili au watatu wanakaa huko ofisini na
kuuuziana eneo kinyemela utaratibu huu haupo kisheria,” alisema Ridhiwani.
Akizungumzia
kuhusiana na baadhi ya maeneo ya Kijiji kuwemo kwenye eneo la ranchi ya Taifa (NARCO)
alisema kuwa uongozi wa halmashauri unapaswa kuonyesha mipaka kwani wananchi
walioko kwenye eneo hilo walianza kuishi kabla ya ranchi hiyo.
Aidha alisema
maeneo yote yanayomilikiwa na ranchi ya Taifa yaliwekewa mipaka na inajulikana
rasmi kisheria tofauti na hapo ambapo ranchi hiyo ndo inaanza kuonyesha mipaka
huku kukiwa hakuna alama yoyote na kuutaka uongozi wa ranchi kushirikiana na
wananchi hao ili kuondoa malalamiko kwani wanapaswa kuondolewa kwenye maeneo
hayo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment