TAASISI mbalimbali nchini zimetakiwa kuwajengea uwezo vijana juu ya umuhimu wa mbio za Mwenge wa Uhuru katika kujenga uzalendo na uwajibikaji katika usimamizi wa shughuli za maendeleo na kutambua fursa za kiuchumi.Friday, March 28, 2025
VIJANA WAFUNDISHWE UMUHIMU WA MBIO ZA MWENGE
TAASISI mbalimbali nchini zimetakiwa kuwajengea uwezo vijana juu ya umuhimu wa mbio za Mwenge wa Uhuru katika kujenga uzalendo na uwajibikaji katika usimamizi wa shughuli za maendeleo na kutambua fursa za kiuchumi.Wednesday, March 26, 2025
MAKAMU WA RAIS DK MPANGO KUZINDUA MBIO ZA MWENGE KITAIFA PWANI
MAKAMU wa Rais Dk Philip Isdor Mpango atazindua mbio za Mwenge kitaifa Mkoani Pwani Aprili 2 mwaka huu kwenye uwanja wa Shirika la Elimu Kibaha.Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Ridhiwani Kikwete akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya juu ya uzinduzi huo amesema kuwa maandalizi ya uzinduzi yanaenda vizuri.
Kikwete amesema kuwa tayari Makamu wa Rais ameshathibitisha kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo wa mbio za Mwenge kwa mwaka 2025.
"Kwa vitu vilivyobakia niwaombe mhakikishe vinafika kwa wakati ili kila kitu kiwe kwenye sehemu yake na bado tutaendelea kuangalia maandalizi ili siku hiyo mambo yawe mazuri,"amesema Kikwete.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amesema kuwa maandalizi yako vizuri ambapo hadi Machi 29 mambo mengi yatakuwa yamekamilika.
Kunenge amesema kuwa huduma zote zitapatikana kuanzia suala la afya, vyoo, maji, taa kubwa, umeme ambapo kutakuwa na jenereta endapo umeme utakatika.
Amewataka wananchi wa Mkoa huo na mikoa jirani na Watanzania kwa ujumla kujitokeza siku hiyo ili kuweka historia ya Pwani kuzindua mbio za Mwenge Kitaifa.
Tuesday, March 25, 2025
JK AWASILISHA UJUMBE MAALUMU KWA RAIS WA SENEGAL KUTOKA KWA RAIS SAMIA
Mhe. Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amewasilisha ujumbe maalumu kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwenda kwa Rais wa Jamhuri ya Senegal, Mhe. Bassirou Diomaye Faye jijini Dakar.
Katika mazungumzo yao ya kirafiki, Rais Mstaafu alieleza dhamira ya dhati ya Rais Samia na Serikali anayoiongoza ya kuendeleza na kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia, kiuchumi na kijamii kati ya Tanzania na Senegal.
Pamoja na masuala ya ushirikiano wa kiserikali, Rais Mstaafu pia alisisitiza umuhimu wa kukuza uhusiano baina ya wananchi wa mataifa haya mawili kupitia sekta za elimu, biashara, utalii, na maendeleo ya vijana na wanawake.
Ziara hii ni sehemu ya juhudi endelevu za Tanzania kuimarisha uhusiano wa kimataifa na mataifa ya Afrika Magharibi, huku ikiweka msisitizo kwa diplomasia ya uchumi na ushirikiano wa watu kwa watu.
MAANDALIZI UWASHWAJI MWENGE WA UHURU KITAIFA PWANI MBIONI KUKAMILIKA
Thursday, March 20, 2025
TANROADS YATOA UFAFANUZI LORI LILILOZIDISHA UZITO MIZANI YA VIGWAZA.
WAKALA wa Barabara Tanzania (TANROADS) imetoa ufafanuzi juu ya taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ya lori la mizigo lililokamatwa kwenye mizani ya Vigwaza kuwa taratibu za kulikamata lori hilo ulifuatwa.
TCRA KUSHIRIKIANA NA TBN KUSADIA KUZALISHA MAUDHUI YENYE TIJA
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeahidi kufanyakazi na Mtandao wa Wana Blogu Tanzania (TBN) pamoja na vyama vingine vya waandishi wa habari ambavyo vinawakilisha mahitaji na matakwa ya wanachama wao.
Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 19 Machi 2025 Jijini Dar es Salaam na Meneja wa Huduma za Utangazaji wa TCRA, Mhandisi Andrew Kisaka, alipokutana na ujumbe wa TBN ofisini kwake, katika kikao cha kujadiliana changamoto mbalimbali zinazowakabili Bloga nchini.
“Sisi huwa tunapenda kufanya kazi na vyama ambavyo vinawakilisha mahitaji na matakwa ya wanachama wao, badala ya kufanyakazi na mwaandishi mmoja mmoja…tunafurahi sana kufanyakazi na waandishi kupitia vyama vyao,” amesema Mhandisi Kisaka.
Mhandisi Kisaka amesema kuwa TCRA imefurahi kukutana na TBN kwa kuwa wanafahamu kuwa Bloga wanasehemu kubwa sana kwenye maudhui ya ndani, na hata kwenye usajili wa TCRA Bloga wanachukua nafasi kubwa sana katika maudhui ya mtandaoni.
“Kwa hiyo TBN mtakuwa silaha moja wapo nzuri sana yakutuwezesha sisi kama Mamlaka ya Mawasiliano nchini, tunao simamia utangazaji pamoja na maudhui ya mtandaoni kuwa karibu na nyinyi na kuhakikisha maudhui ya mtandaoni yanaleta tija na maendeleo kwa wananchi,” amesema Mhandisi Kisaka.
Friday, March 14, 2025
RAIS MSTAAFU DK KIKWETE AFANYA ZIARA NCHINI JAPAN KUIMARISHA USHIRIKIANO KATI YA BODI YA SHIRIKA LA ELIMU LA KIMATAIFA (GPE) NA JAPAN
Rais mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Elimu la Kimataifa (GPE), yupo Tokyo nchini Japan kwa ziara maalum yenye lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya GPE na serikali ya Japan katika kutatua changamoto za elimu ya msingi katika nchi zinazoendelea.
Katika siku yake ya kwanza Tokyo, Dkt. Kikwete amefanya mazungumzo na Waziri wa Fedha wa Japan, Mhe. Shin-ichi Yokohama, pamoja na Naibu wake, Mhe. Atsushi Mimura.
Mazungumzo hayo yalijikita katika ushirikiano wa kifedha ili kusaidia miradi ya elimu inayosimamiwa na GPE, ikiwemo upatikanaji wa rasilimali kwa ajili ya kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto wa nchi zinazoendelea.
Baada ya mazungumzo hayo, Rais Mstaafu Kikwete alikutana na Bw. Akihiko Tanaka, Rais wa Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Japan (JICA).
Shirika hili limekuwa na mchango mkubwa katika miradi ya maendeleo barani Afrika, na mazungumzo yalihusu namna JICA inaweza kusaidia jitihada za GPE katika kukuza elimu bora.
Dkt. Kikwete pia alikutana na Bw. Yohei Sasakawa, Mwenyekiti wa Taasisi ya Nippon. Bw. Sasakawa, mwenye umri wa miaka 86, ni mtu mashuhuri wa kusaidia miradi ya kijamii duniani.
Katika mazungumzo yao, waligusia nafasi ya sekta binafsi katika kusaidia elimu, hasa kupitia taasisi zisizo za kiserikali. Vilevile, Bw. Sasakawa alishangaza dunia baada ya kufanikisha kupanda Mlima Kilimanjaro tarehe 12 Februari 2024, kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 85 ya kuzaliwa kwake – hatua inayothibitisha kuwa umri si kikwazo kwa ndoto kubwa.
Katika siku zinazofuata, Rais Mstaafu Kikwete anatarajiwa kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Mhe. T. Miyaji, pamoja na wabunge wa Bunge la Japan, ambapo ajenda kuu itakuwa nafasi ya elimu na teknolojia katika maendeleo ya jamii.
Pia, atashiriki mijadala maalum kuhusu elimu na teknolojia, kufanya mahojiano na vyombo vya habari, pamoja na kukutana na Mhe. Tetsuro Yano, Rais wa Taasisi ya AFRECO, ambayo inahusika na kukuza ushirikiano kati ya Japan na Afrika.
Ziara hii ni sehemu ya juhudi endelevu za Dkt. Kikwete katika kuboresha mifumo ya elimu duniani, hasa katika nchi zinazoendelea.
Japan ni mshirika muhimu wa maendeleo ya elimu barani Afrika, na ushirikiano huu unaweza kuwa na mchango mkubwa katika kuhakikisha watoto wengi zaidi wanapata fursa ya elimu bora.





