Na John Gagarini, Mafinga
MWANAFUNZI wa kidato cha sita wa Shule ya Sekondari ya JJ
Mungai Octavian Luoga (20) amejeruhiwa kichwani kwa kupigwa fimbo na mwalimu
wake kwa tuhuma za kushindwa kuingia darasani.
Akizungumza jana mjini Mafinga na waandishi wa habari mara
baada ya kutoka kwenye Hospitali ya Mafinga wilaya ya Mufindi mkoani Iringa
alipotoka kupatiwa matibabu mwanafunzi huyo alisema kuwa mbali ya kupigwa na
fimbo kichwani pia alipigwa makofi na mateke.
Luoga alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya asubuhi
Septemba Mosi akiwa bwenini amepumzika
kutokana na kuumwa na mishipa ya kichwa huku akiwa na wenzake wawili Wilson Due
na Nsajigwa Moses ambao wote walikuwa wakiumwa jambo lililomfanya ashindwe
kuingia darasani.
“Walimu wawili walikuja na kunitaka niende ofisini kwa ajili
ya kupewa adhabu nikawaambia mimi naumwa ndiyo sababu ya kushindwa kuingia
darasani mara wakaanza kunipiga nikawaambia nuamwa naomba mnisikilize wakakataa
wakasema nimewajibu vibaya,” alisema Luoga.
Alisema kuwa kutokana na kipigo hicho ikabidi aende ofisini na
kufika kule akaanza kupigwa makofi,mateke na fimbo maeneo mbalimbali ya mwili
na mwalimu mkuu msaidizi Huruma Nyalusi akidai kuwa nawadharau walimu.
“Mwalimu alinipiga fimbo kichwani na damu zikaanza kunitoka
hata hivyo hawakutaka kunipeleka hospitali ndipo wanafunzi wengine
wakalazimisha nipelekwe ambapo tulienda polisi na baadaye hospitali kwa ajili
ya matibabu nikashonwa nyuzi kadhaa,” alisema Luoga.
Aidha alisema kuwa walimu na wanafunzi wanafahamu matatizo
yake na wiki moja iliyopita alilazwa kutokana na tatizo lake hilo hilo hali
ambayo ilimfanya ashindwe kuingia darasani ambapo hata mahudhuria yake darasani
ni mazuri lakini huwa anashindwa kuingia darasani kutokana na kuumwa kwake.
Baadhi ya wanafunzi walisema kuwa baadhi ya walimu wa shule
hiyo wamekuwa na tabia ya kupiga wanafunzi kupita kiasi huku wakati mwingine
wakiwapiga ngumi, makofi, vichwa mateke na kuwachapa fimbo zisizo na idadi.
Jitihahada za kumpata mwalimu Nyalusi aliyehusika na tukio
hilo hazikuweza kufanikiwa kwani alikuwa akihojiwa kwenye kituo cha polisi cha
Mafinga kuhusiana na tukio hilo baada ya wanafunzi wa kidato cha sita
kuandamana kwenda polisi kulalamika.
Hata hivyo jitihada za
kumpata mwalimu mkuu wa shule hiyo Mariano Mwanyingu hazikuweza kufanikiwa
kwani hakuwepo shuleni hapo kwani aliondoka kabla ya tukio hilo kutokea na
haifahamiki atarudi baada ya muda gani.
Kwa upande wake mkuu wa polisi wilaya ya Mufindi Ambwene
Mwanyasi alikiri kupokelewa kwa mwalimu huyo ambaye alihusika na tukio hilo kwa
ajili ya kuhojiwa.
Mwisho.
MWANAFUNZI wa kidato cha sita wa Shule ya Sekondari ya JJ
Mungai iliyopo kwenye Halmashauri ya Mji wa Mafinga wilaya ya Mufindi mkoani
Iringa Octavian Luoga (20) amejeruhiwa
kichwani kwa kupigwa fimbo na mwalimu wake kwa tuhuma za kushindwa kuingia
darasani.
Akizungumza jana mjini Mafinga na waandishi wa habari mara
baada ya kutoka kwenye Hospitali ya Mafinga wilaya ya Mufindi mkoani Iringa
alipotoka kupatiwa matibabu mwanafunzi huyo amesema kuwa mbali ya kupigwa na
fimbo kichwani pia alipigwa makofi na mateke.
Luoga amesema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya asubuhi
Septemba Mosi akiwa bwenini amepumzika
kutokana na kuumwa na mishipa ya kichwa huku akiwa na wenzake wawili Wilson Due
na Nsajigwa Moses ambao wote walikuwa wakiumwa jambo lililomfanya ashindwe
kuingia darasani.
Amesema kuwa walimu wawili walikwenda na kumtaka aende
ofisini kwa ajili ya kupewa adhabu kwani hakwenda darasani akawaambia anaumwa
ndiyo sababu ya kushindwa kuingia darasani mara wakaanza kumpiga licha ya
kuwaomba wamsikilize wakakataa wakasema amewajibu vibaya.
Amesema kuwa kutokana na kipigo hicho ikabidi aende ofisini
na kufika kule akaanza kupigwa makofi,mateke na fimbo maeneo mbalimbali ya
mwili na mwalimu mkuu msaidizi Huruma Nyalusi akidai kuwa nawadharau walimu.
Aidha amesema kuwa mwalimu alimpiga fimbo kichwani na damu
zikaanza kumtoka hata hivyo hawakutaka kumpeleka hospitali ndipo wanafunzi
wengine wakalazimisha apelekwe ambapo walienda polisi na baadaye hospitali kwa
ajili ya matibabu nikashonwa nyuzi kadhaa.
Amesema kuwa walimu na wanafunzi wanafahamu matatizo yake na
wiki moja iliyopita alilazwa kutokana na tatizo lake hilo hilo hali ambayo
ilimfanya ashindwe kuingia darasani ambapo hata mahudhuria yake darasani ni
mazuri lakini huwa anashindwa kuingia darasani kutokana na kuumwa kwake.
Baadhi ya wanafunzi wamesema kuwa baadhi ya walimu wa shule