Baadhi ya wawekezaji toka nchini China wakiwa wanamsikiliza mkuu wa mkoa wa Pwani hayuko pichani walipomtembelea ofisini kwake Mjini Kibaha |
Mkuu wa mkoa katikati waliokaa akiwa na ugeni toka nchi ya China walipomtembelea ofisini kwake mjini Kibaha |
Mkuu wa mkoa wa Pwani na mgeni wake na katibu tawala wa mkoa wakiwa wanafuatialia mazungumzo |
Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akimkabidhi zawadi mwakilishi wa wawekezaji toka nchi ya China |
Wataalamu wa mkoa |
Wataalamu wa mkoa |
Mkuu wa mkoa wa Pwani akimkabidhi zawadi moja ya wawakilishi wa wawekezaji toka nchi ya China Na John Gagarini, Kibaha |
WAWAKILISHI wa makampuni toka nchi ya China wameonyesha nia ya kuwekeza kwenye sekta mbalimbali mkoani Pwani baada ya kuonyeshwa fursa za uwekezaji kwenye mkoa huo.
Wakizungumza baada ya kumtembelea mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo wawakilishi hao baada ya kuonyeshwa maeneo hayo ya uwekezaji kwa njia ya video waliahidi kuwatuma wataalamu ili waone wawekeze kwenye masuala gani.
Mwakilishi wa wawekezaji hao Liv Ming alisema kuwa wamefurahishwa na nchi ya Tanzania na kikubwa ni uhusiano mzuri uliokuwepo tangu enzi za marais Julius Nyerere na Mao Tse Sung.
“Tumeona fursa nyingi za uwekezaji na tunatarajia kuwatuma wataalamu wetu kujua kuangalia na kutupa ushauri lakini baadhi ya vitu ni uwekezaji kwenye sekta ya umeme, vipuri vya magari na uhifadhi wa mazao,” alisema Ming.
Alisema kuwa wameona maeneo mbalimbali kwa njia ya video ambayo wanaweza kuwekeza na wataendelea kufanya mawasiliano na mkoa kwa ajili ya masuala ya uwekezaji kwenye sekta mbalimbali.
“Tumevutiwa na mambo mengi pia kuna baadhi ya makampuni ya wenzetu kutoka China wamewekeza viwanda mengine yanazaidi ya miaka 20 hivyo tutaendelea kuhamasisha wenzetu nao waje kuwekeza,” alisema Ming.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo alisema kuwa ujio wa wageni hao ni faraja kwa mkoa pamoja na nchi kwa ujumla kwani itasaidia azma ya serikali ya kuwa nchi ya viwanda.
Ndikilo alisema kuwa mkoa utaendelea kuhamasisha wawekezaji wa nje na ndani ya nchi ili wawekeze kwenye sekta mbalimbali ikiwemo viwanda ili kufikia malengo ya serikali ya awamu ya tano ya nchi ya viwanda na uchumi wa kati.
Ujio wa wawekezaji hao ni kufuatia ziara ya wiki mbili iliyofanywa na timu ya mkoa wa Pwani ya Viongozi pamoja na wataalamu walioifanya mwezi Oktoba mwaka huu ambapo waliweza kuzungumza na makampuni 106 na 30 kukubali kuja mkoani Pwani kwa ajili ya kuja kuangalia maeneo ya uwekezaji.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment