Katibu wa CCM Kibaha Mjini Abdala Mdimu akitoa taarifa fupi ya marehemu wakati wa kuaga kwenye ofisi za CCM Kibaha Mjini
Na John Gagarini,
Kibaha
KATIBU wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Pwani Anastazia Amas juzi aliwaongoza
wanachama na wananchi wa wilaya ya Kibaha kuaga mwili wa Mjumbe wa Mkutano Mkuu
wa CCM mkoa wa Pwani kuwakilisha Kata ya Pangani Albert Ngwada kwa ajili ya
mazishi mkoani Iringa ambaye alifariki dunia Novemba 13 mwaka huu.
Akiongea wakati
wa kuaga mwili wa marehemu Ngwada kwenye ofisi za CCM Kibaha Mjini Amas alisema
kuwa chama kimepata pigo kutokana na kifo hicho cha mjumbe wa CCM.
Amas alisema
kuwa ili kumkumbuka marehemu wanachama wanapaswa kufanya kazi za chama kwa
uaminifu na uadilifu ili kuleta maendeleo ndani ya chama na kwa wananchi wa
Kibaha kama alivyokuwa Ngwada.
“Natoa pole
kwa ndugu na wote walioguswa na msiba huu ambao umewagusa watu wengi na ndiyo
maana watu wamejaa hii yote inaonyesha jinsi gani mlivyokuwa mnamkubali
kutokana na utendaji wake kikubwa ni kuenzi utendaji wake,” alisema Amas.
Awali akitoa
maelezo mafupi juu ya marehemu katibu wa CCM Kibaha Mjini Abdala Mdimu alisema
kuwa kutokana na utendaji wake kazi mzuri marehemu alipandishwa cheo kutoka Katibu
msadizi wa kata ya Pangani na kuwa kaimu katibu msaidizi wa CCM Kibaha Mjini
mwaka 2015
Mdimu alisema
kuwa marehemu alitumikia nafasi hiyo kama msiadizi wake hadi mwaka 2017 baada
ya kuletwa katibu msaidizi toka Magu ambapo Aprili alichaguliwa kuwa mjumbe wa
mkutano mkuu wa mkoa toka kata ya Pangani nafasi aliyokuwa nayo hadi anafariki
dunia.
Awali
marehemu alianza kukitumikia chama mwaka 2007 hadi mwaka 2012 alipochaguliwa
kuwa katibu kata Pangani hadi 2017 Juni 2015 alipanda daraja na kuwa Kaimu
katibu Msaidizi hadi Aprili 2017.
Alisema kuwa
mwaka huu mwezi Mei alichaguliwa kuwa Mjumbe wa mkutano mkuu wa mkoa kupitia
kata ya Pangani na tarehe 4 Oktoba alipata
ajali ya Pikipiki huko eneo la Kidimu majira ya saa 1:30 usiku na kupelekwa
Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Pwani ya Tumbi na baadaye alihamishiwa Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili.
Aidha marehemu
alifariki dunia wakati akiendelea na kliniki baada ya kutolewa Hospitali na
alitarajiwa kuzikwa jana kwao mkoani Iringa na alizaliwa mwaka 1982.
Mwisho.
|
No comments:
Post a Comment