Wadau wa zao la korosho wakiptia taarifa mbalimbali juu ya uuzaji wa zao la korosho mkoani Pwani
Na John
Gagarini, Mkuranga
MKUU wa Mkoa
wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo amewataka wakuu wa Polisi wa wilaya kuwakamata
wafanyabiahara ambao watanunua zao la korosho la msimu huu kinyume cha
utaratibu ikiwemo wale wanaonunua kwa njia ya “Kangomba”.
Ndikilo
aliyasema hayo wilayani Mkuranga wakati wa mkutano na viongozi wa vyama vya
wakulima wa zao la Korosho mkoani humo na kusema kuwa kwa msimu huu hataki
kuona walanguzi wa zao hilo kwani wanawanyonya wakulima.
Alisema kuwa
ununuzi kwa njia ya Kangomba ni marufuku na atakayekamatwa ananunua kwa njia
hiyo ambayo inawanyonya wakulima haitakiwi.
“Ununuzi kwa
njia ya Kangomba ni marufuku mauzo yote yafanyike kwa njia yam nada kwa kutumia
stakabadhi ghalani hayo ndi maelekezo ya serikali atakayenunua tofauti na
utaratibu huo akamatwe wakuu wa polisi wa wilaya fanyeni kazi msiwaonee huruma
walanguzi wawekeni ndani,” alisema Ndikilo.
Aliitaka bodi
ya korosho kuhakikisha inakabili changamoto za upatikanaji wa magunia ili
korosho zilizovunwa zisiharibike na kuuzwa kwa bei ndogo kwenye soko la korosho
ambapo unuzi unaanza Novemba 8 mwaka huu.
Kwa upande
wake meneja wa bodi ya Korosho tawi la Dar es Salaam Mangile Malegesi alisema
kuwa msimu wa zoa hilo kwa mkoa wa Pwani utazinduliwa wiki ijayo ambapo kwa
mikoa ya Lindi na Mtwara msimu umeshazidnuliwa.
Malegesi
alisema kuwa magunia yatapatikana kwa wakati ili wakulima waweze kuhifadhi
korosho zao ambapo bei elekezi ni shilingi 1,460 kwa daraja la kwanza na 1,160
kwa daraja la pili.
Naye
mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Pwani (CORECU) Rajabu Ngonema
alisema kuwa changamoto kubwa iliyopo ni magunia na wakulima kutaka kuuza
korosho zao kwenye maghala ya vyama vya msingi badala ya kuuza kwenye maghala
makuu yaliyopitishwa na bodi ya Korosho.
Ngonema
alisema kuwa maghala ni changamoto kubwa kwani wakulima wanahofia gharama na
usumbufu na kutaka wauzie kwenye maghala ya vyama vya msingi.
Mwisho.
|
No comments:
Post a Comment