Moja ya Vijana wa UVCCM Kibaha Mjini akimvalisha skafu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Kheri James alipowasili wilayani Kibaha |
Baadhi ya Vijana wa UVCCM Mkoani Pwani wakishanglia jambo wakati wa mkutano huo |
Mbunge wa Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo akiongea kwenye mkutano huo. |
Na John Gagarini, Kibaha
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha
Mapinduzi (UVCCM) Taifa Kheri James amewataka viongozi wa serikali na
wale wa kuchaguliwa nchini kuhakikisha wanashiriki kwenye mikutano ya
viongozi wa kitaifa ili waweze kupokea maagizo mbalimbali.
Aliyasema
hayo mjini Kibaha wakati wa sherehe za kumpongeza kwa kuchaguliwa
kwenye nafasi hiyo zilizoandaliwa na Uvccm Kibaha Mjini na kusema kuwa
maagizo yanayotolewa hayawezi kufanyiwa kazi kutokana na wahusika
kutokuwepo.
James alisema kuwa viongozi na watendaji wa serikali ambao hawashiriki vikao kama hivyo hawafai waondoke kwani wameshindwa kazi.
"Hapa
tunatoa maagizo na wao hawapo kwani maelekezo hayo yanapotolewa watu wa
kuyapokea hawapo kuanzia ngazi ya halmashauri za wilaya, wilaya na Mkoa
wanapaswa kujirekebisha kama wanaona hawawezi kazi watupishe," alisema
James.
Alisema kuwa
maelekezo yanayotolewa ni kuzikabili changamoto ambapo atendaji wa
serikali wanaposhindwa kutatua kero za wananchi ambazo ni ilani ya chama
kuna sababisha chama kuwa na wakati mgumu nyakati za uchaguzi kwa
wagombea wa ccm.
"Watendaji wanaohujumu waondoke kwani wao ndiyo watekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa ajili ya wananchi," alisema James.
"Viongozi
hawapaswi kulewa madaraka ambayo ni kitu kibaya sana na ni sawa na
ulevi na hutafsiriwa baada ya muda wa kuwa madarakani kwisha ambapo watu
watakuhukumu kwa matendo yako na kuwa bakora ya kukuchapia," alisema
James.
Alisema kuwa
hataki uongozi wa mitandao wa fb,insta, WhatsApp anataka viongozi wa
kufanya kazi kwani kazi ya kuongoza ni ngumu sana hasa wakati wa
kuhakiki mali za jumuiya hiyo watapambana na watu wenye vyeo vikubwa na
fedha nyingi hivyo ni vita kubwa.
Aidha
aliwata viongozi wa chama kutowatumia tu vijana wakati wa uchaguzi
wasiwafanye kama ngazi ya kupandia na kama hawatawashirikisha vijana
wampe taarifa na suala la ajira liangaliwe kwani baadhi ya wafanyakazi
wanaajiriwa toka nje kwa kazi zinazowezwa kufanywa na watanzania.
"Wamiliki
waangalie maslahi ya wafanyakazi vitendea kazi kwani baadhi wanafanya
kazi kwenye viwanda ambvyo huzalisha kwa kutumia kemikali ambazo
zinaweza kuwa maafa endapo hawatapewa vifaa vya kuwakinga kwani inaweza
kusababisha vifo kwani viwanda si kwa ajili ya kusababisha vifo,"
alisema James.
Aliwataka
wabunge wasiwe wa mifukoni wakichaguliwa wanaondoka na kusubiri hadi
muda wa uchaguzi kwa sasa hawana nafasi wanajitokeza muda huo na kuanza
vurugu wakidai fulani anampinga kumbe hawakuwajibika na kujiweka mbali
na wananchi pia viongozi wa chama pamoja madiwani kuhakikisha kuwa
asilimia tano ya vijana inakuwa agenda ya kudumu kwenye vikao
mbalimbali.
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa ccm Mkoa Pwani Ramadhan Maneno alisema kuwa
watahikikisha wana hakiki mali za umoja huo wakiwa kama wasimamiaji wa
jumuiya zote za chama.
Awali
mwenyekiti wa umoja huo Chalangwa Seleman wa mkoa alitaka viongozi
kufuata maelekezo ya rais ili kufanya umoja huo kuwa kimbilio na
watayatrkeleza yale yote yaliyotolewa na mwenyekiti wao.
No comments:
Post a Comment