Na John
Gagarini, Kibaha
MKUU wa
wilaya ya Kibaha mkoani Pwani Asumter Mshama amesikitrishwa na baadhi ya wakazi
wa mtaa wa Mwanalugali kata ya Tumbi wanaoshiriki kwenye vitendo vya
kishirikina kwa kufanya ngono kwenye makaburi ya Air Msae yaliyopo katika mtaa
huo na kusema kuwa serikali haitatoa fedha kwa ajili ya kuweka uzio kwenye
makaburi hayo ili kuzuia vitendo hivyo.
Makaburi hayo
ambayo yalianzishwa na halmashauri ya Mji wa Kibaha baada ya basi la Air Msae
kupata ajali kwenye barabara kuu ya Morogoro ambapo ili ua watu wengi na maiti
nyingi zilizikwa hapo baada ya kukosa ndugu.
Akizungumza
na wakazi wa mtaa huo alisema kuwa inasikitisha kuona watu wanafanya vitendo
hivyo juu ya makaburi kwani hiyo ni laana kwa watu wanaojihusisha na vietendo
hivyo na serikali haitapeleka fedha kwa ajili ya kuweka uzio badala yake fedha
hizo ni afadhali zipelekwe kwenye shughuli za maendeleo.
Mshama alitoa
kauli hiyo kufuatia uongozi wa kata hiyo ambapo mtendaji wa kata hiyo
Msemakweli Karia akisoma risala alisema kuwa moja ya changamoto zilizopo kwenye
kata ni baadhi ya watu kujihuisha na uovu huo nyakati za usiku juu ya makaburi
hayo pamoja na vitendo vingine viouvu ikiwa ni pamoja na uvuitaji wa bangi hivyo
kuomba kupewa fedha kwa ajili ya kuweka uzio kuzuia watu hao.
“Haiwezekani kuweka
uzio kwani watu wanaofanya vitendo hivyo wanajitafutia laana kwani hawawezi
kupata utajiri kwa kufanya vitendo hivyo kwenye makaburi hayo ya umma ambayo
yanatumika kuzika watu kwenye mji wa Kibaha na hiyo ni laana kwani wanaofanya
hivyo wanasema kuwa kwa kuwa ajali hiyo iliua watu wengi hivyo na wao watapata
utajiri mkubwa jambo ambalo ni dhana ambayo haipaswi kupewa nafasi kwani uchawi
unarudisha nyuma maendeleo na mji unaoendekeza imani hizo hauwezi kupiga hatua,”
alisema Mshama.
Aidha alisema
ili wananachi wa weze kujiletea maendeleo wanapaswa kufanya kazi kwa bidii na
si kuwa na imani za kishirikina ili kupata maendeleo suala hilo halipaswi
kupewa kipaumbele bali jitihada za kufanya kazi kwa bidii ndizo zitakazowafanya
wawe na maisha mazuri.
Awali akisoma
risala ya Kata ya Tumbi mtendaji wa kata hiyo Msemakweli Karia amesema kuwa
changamoto nyingine zilizopo katika eneo hilo ni ubovu wa barabara.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment