Na John Gagarini, Kibaha
CHAMA cha Waamuzi wa Soka Tanzania (FRAT) mkoa wa Pwani
kimemchagua Jeremia Komba kuwa
mwenyekiti wa chama hicho kwa kupata kura 15 huku mpinzani wake Kassim Safisha akipata
kura tano.
Uchaguzi huo ambao ulifanyika mjini Kibaha na
kusimamiwa na mwamuzi mkongwe Hussein Magoti na kuwashiriki waamuzi ambao ni
wanachama wa chama hicho cha waamuzi.
Komba alikuwa akichuana na mwamuzi mwenzake Kassim
Safisha nakumshinda kwa tofauti ya kura tano hivyo kumfanya Komba kuwa bosi wa
waamuzi wilaya ya Kibaha.
Nafasi ya makamu mwenyekiti ilikwenda kwa Sayenda
Lubisa ambaye hata hivyo hakuwa na mpinzani na kujipatia kura 17 huku tatu
zikiharibika.
Upande wa katibu mkuu Endrew Kayuni alikuwa mshindi
kwa kupata kura 15 huku Mohamed Juaji akipata kura tano, nafasi ya katibu
msaidizi ilikwenda kwa Hamis Mpangwa ambaye alijinyakulia kura 11 akimshinda
Mohamed Msengi aliyepata kura tisa.
Nafasi ya mweka hazina ilikwenda kwa Kassim Naroho
aliyepata kura 16 akimshinda Nickson Haule aliyepata kura nne, kwa upande wa
mwakilishi wa mkutano mkuu ilikuwa na mgombea mmoja Hamad Seif ambaye alipata
kura 19..
Kwa upande wa kamati ya utendaji nafasi tatu
walioshinda ni Kasule Ambogo kura 18, Leah Petro kura 16, Gabriel Kinyogoli
kura 15 na Sultan Singa kura nane ambapo mwenyekiti mpya Komba aliwataka waamuzi
kuwa na mshikamano.
Komba alisema kuwa jambo kubwa ili waweze kufikia
malengo ni kuwa nidhamu na kuzingatia sheria kwa kuzitafsiri wawapo uwanjani
ili kuondoa malalamiko dhidi yao kwani baadhi wamekuwa wakienda kinyume na sheria
za mchezo huo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment