Friday, July 24, 2015

HARAKATI ZA UCHAGUZI ZAENDELEA

Na John Gagarini, Kibaha
WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Kibaha Mjini wametakiwa kuacha tabia ya kukumbatia makundi mara baada ya uchaguzi wa ndani kumalizika kwani yanasababisha chama kushinda kwa tochi.
Hayo yalisemwa juzi na mwenyekiti wa CCM Kibaha Mjini Maulid Bundala wakati akiwanadi watia nia waliojitokeza kuwania kuchaguliwa na chama hicho kupeperusha bendera kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Bundala alisema kuwa makundi hayo yanachangia kwa kiasi kikubwa chama kushindwa kutokana na mshikamano na ushirikiano kutokuwepo kwenye chaguzi mbalimbali ambazo zinahusisha vyama vingi vya siasa.
“Kipindi hichi ni kigumu sana kuwa na kundi siyo tatizo lakini mara atakapopatikana mgombea mmoja wa ubunge makundi yanatakiwa kwisha na kubakia kundi moja tu la CCM ambalo linatakiwa lipambane na wapinzani,” alisema Bundala.
Alisema kuwa kwanini chama kishindwe kwa mbinde kwa ushindi wa tochi wakati kina wanachama wengi ukilinganisha na vyama vya upinzani lakini inaonekana kushindwa kunatokana na kukumbatiwa kwa makundi hayo.
“Makundi yanatakiwa yaishe mara uteuzi wa mwanachama mmoja ambaye atawakilisha chama kwenye uchaguzi tatizo linguine ni wanachama kumpenda mtu badala ya kukipenda chama na kuachana na tabia ya kuwasema vibaya wagombea kwani wote ni Wanaccm,” alisema Bundala.
Aliwataka wanaccm ambao wanasifa ya kupiga kura za maoni za kuchagua mbunge kwenye kura za maoni wanapaswa kuwa hai kwa kulipia kadi za chama, wawe wameorodheshwa kwenye daftari la tawi na wawe na kadi ya kupigia kura.
Mwisho.
 Na John Gagarini, Kibaha
WATIANIA wanne wa Jimbo la Kibaha Mjini wilayani Kibaha mkoani Pwani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameendelea kumwaga sera zao kwa wanachama ili waweze kupata fursa ya kuchaguliwa na chama hicho kwa kupigiwa kura za maoni kupata mgombea mmoja zinazotarajiwa kufanyika Agosti Mosi mwaka huu. 
Wagombea hao ambao ni Silvestry Koka ambaye anatetea kiti chake Rugemalila Rutatina, Idd  Majuto, Abdala Bagdela na Abdulaziz Jab wakiwa kwenye kata ya Kibaha na Kongowe wote kila mmoja alijinadi kwa staili ya aina yake ikiwa ni njia ya kuomba kuchaguliwa kwenye kura za maoni ili kukiwakilisha chama hicho kwenye nafasi ya Ubunge wa Jimbo hilo.
Kwa upande wake Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa NEC CCM, Rugemalila Rutatina alisema kuwa ilani ya chama ni nzuri sana lakini tatizo ni kwamba wasimamiaji ndiyo chanzo cha kushindwa kufikiwa kwa maendeleo.
Rutatina alisema kuwa endapo atachaguliwa athakikisha anaisimamia ilani ya chama ambayo ina majibu ya changamoto zote zinazowakabili wananchi na atakuwa kiongozi na si mtawala na kuwa ubunge ni ajira huku wananchi wakiwa ndiyo waajiri wa wabunge.
Silvestry Koka alisema kuwa katika uongozi wake amefanya mambo makubwa ikiwa ni pamoja na kukabiliana na changamoto ya maji ambapo ameweza kuhakikisha maji yanapatikana mitaa 14 ambapo kwa sasa kuna mradi mkubwa ambao utafanya Jimbo hilo kutokuwa na tatizo la maji.
Alisema anaomba achaguliwe tena ili aweze kukamilisha mipango iliyobaki kwani anauwezo wa kuongoza na kufanikisha maendeleo ya Jimbo hilo ambalo kwa sasa liko kwenye mchakato wa kuwa manispaa.
Abdulaziz Jaab alisema kuwa endapo atachaguliwa kwenye nafasi hiyo ya Ubunge kupitia CCM yeye atasimamia maendeleo endelevu na si uongozi wa nadharia ya kuongoza kwa msimu kama baadhi ya viongozi wanavyofanya.
Jab alisema kuwa kwa kushirikiana na wananchi atahakikisha anawashirikisha wananchi kwenye suala zima la maendeleo na si kujikita zaidi kwa vipindi huku muda mwingi wanachi wakiwa hawafikiwi hadi msimu wa uchaguzi.
Idd majuto yeye alisema kuwa wanCCM wanatakiwa kuacha kuchagua viongozi ambao wanatumia rushwa kupata uongozi kwani wanachangia kuzorotesha maendeleo ya wananchi kwani wanawanunua wananchi kama nyanya.
Alisema kama mgombea anatoa rushwa wao wale lakini wakati wa kuchagua waangalie nani anayefaa kuwa kiongozi na kuacha kuchagua viongozi wanaofanya rushwa kama kigezo cha kuwa kiongozi kwani hawafai.
Abdala Bagdela alisema kuwa endapo atachaguliwa atahakikisha kila mwananchi anamiliki nyumba ili aweze kuishi kwenye makazi bora huku fedha za ujenzi zikitokana na vyama vya kuweka na kukopa VICOBA.
Alisema kuwa atahakikisha anaweka mazingira mazuri kwa wajasiriamali wadogo kwa kuwaondolea kero za sheria zinazowabana ili waweze kufanya kazi zao bila ya usumbufu wanaoupata lengo wafanikiwe kujikwamua na hali ngumu.
Mwisho.
Na John Gagarini, Mufindi
WATIA nia watatu wamejitokeza kupambana na Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini ambaye ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mahmoud Mgimwa ambaye anattetea kiti chake kwenye Jimbo hilo ambalo limeganywa na kutoka Jimbo lingine la Mafinga Mjini .
Katibu wa CCM Jimson Mhagama alisema kuwa kwa sasa watia nia wote wanapitishwa kwa wanachama ili waeleze sera zao kwa wanachama ambao watawapigia kura za maoni zinazotarajiwa kufanyika Agosti Mosi mwaka huu ili kupata Mbunge atakayepambana na vyama vya upinzani.
Mhagama aliwataja wagombea wengine kuwa ni Dk Godfrey Kalinga, Godfrey Ngupula na Exaud Kigahe ambao kwa sasa wako kwenye zoezi la kunadi sera zao kwa wanachama ili wawachague mmoja aweze  kupeperusha bendera ya chama.
Kwa upande wa Jimbo la Mafinga Mjini ambalo limemegwa kutoka Jimbo la Mufindi Kaskazini jumla ya wagombea watano watachuana kwenye kinyanganyiro hicho ambao ni Zuber Ngullo, Cosato Chumi, Paul Myinga, Benjamin Balali, James Mgimwa.
Aidha alisema kuwa Jimbo la Mufindi Kusini jumla ya watia nia 15 wamejitokeza kuwania nafasi hiyo ambao ni Dickson Lutevele, Mary Miho, Golden Ally, Dionis Myinga, Frank Mng’olage, Dk Prosper Mfilinge, Anton Mpiluka, Charles Sanga, Menrad Kigola, Wende Ngahala, Faustin Mhapa, Marcelin Mkini, Dk Alex Sanga, Albert Chalamila na Robert Malangalila.   
Mhagama alisema kuwa wagombea wote ni wa CCM na wana sifa za kuwa wabunge kinachotakiwa ni wanachama kuchagua mmoja ambaye wataona anafa

Na John Gagarini, Bagamoyo

WAJUMBE wa mkutano mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake  Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (UWT) Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani wamechagua madiwani wake wa viti maalumu baada ya kufanyika kwa uchaguzi wa nafasi hiyo.

Kwenye uchaguzi huo  ulihudhuriwa na wajumbe wapiga kura 958 kutoka Tarafa saba zilizomo katika wilaya hiyo,uchaguzi ambao ulisimamiwa na Pilli Augostino ,aliyesaidiwa na Husna Ally huku mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya Almasi Masukuzi na katibu wake Kamote Kombo wakifuatilia mchakato mzima.

Katika kinyang’anyiro hicho kilikuwa na jumla ya wagombea 22 waliojitokeza kuwania nafasi hiyo kutokea kwenye Tarafa saba zilizomo wilayani humo ambazo ni Msoga, Chalinze, Msata, Miono, Kwaruhombo, Mwambao na Yombo.

Pilli alisema kutoka Tarafa ya Chalinze kura za washindi katika mabano ni Mwanakesi Madega (555) dhidi ya Nuru Mhami (78), Tarafa ya Kwaruhombo Asha Mtunye (35), Tatu Mpongo (443) na Tunu Mpwimbwi (476). Tarafa ya Msoga Zaituni Kawogo (57), Matha Patel (400) na Maria Moreto (426).

Tarafa ya Msata Sophia Issa (89), Anzeni Rajabu (294), Rehema Mno (484). Tarafa ya Miono Tukae Kilo (321), Sijali Mpwimbwi (612). Tarafa ya Mwambao Nuru Abdallah (5), Leonia Fransic (11), Shumina Sharifu (172) Sinasud Onelo (199) Hapsa Kilingo (563). Tarafa ya Yombo Togo Omary (205), Nuru Mohamed (260)na Elizabeth Shija (458).

Katika mchakato huo ngazi ya kapu Togola alipata  (81), Sinasud (175), Sophia (118), Zaituni (31), Tukae (103), Leonia (140), Magazin (210), Shumina (308), Tatu (274), Nuru Mohamed (18), Asha (5), Nuru (4), Mhami (49), Matha (289), Anzeni (45). Hivyo Shumina Sharifu na Martha Patel.

Baada ya kutangaza matokeo hayo,Pilli aliwataka madiwani hao kwenda kufanyakazi ili kuhakikisha wagombea wote wanaotokea ndani ya CCM wanashinda kwa kishindo kwani kinyume chake ushindi huo ni kazi bure.

Mwisho.
 Na John Gagarini, Kibaha
WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Kibaha Mjini wametakiwa kuacha tabia ya kukumbatia makundi mara baada ya uchaguzi wa ndani kumalizika kwani yanasababisha chama kushinda kwa tochi.
Hayo yalisemwa juzi na mwenyekiti wa CCM Kibaha Mjini Maulid Bundala wakati akiwanadi watia nia waliojitokeza kuwania kuchaguliwa na chama hicho kupeperusha bendera kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Bundala alisema kuwa makundi hayo yanachangia kwa kiasi kikubwa chama kushindwa kutokana na mshikamano na ushirikiano kutokuwepo kwenye chaguzi mbalimbali ambazo zinahusisha vyama vingi vya siasa.
“Kipindi hichi ni kigumu sana kuwa na kundi siyo tatizo lakini mara atakapopatikana mgombea mmoja wa ubunge makundi yanatakiwa kwisha na kubakia kundi moja tu la CCM ambalo linatakiwa lipambane na wapinzani,” alisema Bundala.
Alisema kuwa kwanini chama kishinde kwa mbinde kwa ushindi wa tochi wakati kina wanachama wengi ukilinganisha na vyama vya upinzani lakini inaonekana kushindwa kunatokana na kukumbatiwa kwa makundi hayo.
“Makundi yanatakiwa yaishe mara uteuzi wa mwanachama mmoja ambaye atawakilisha chama kwenye uchaguzi tatizo linguine ni wanachama kumpenda mtu badala ya kukipenda chama na kuachana na tabia ya kuwasema vibaya wagombea kwani wote ni Wanaccm,” alisema Bundala.
Aliwataka wanaccm ambao wanasifa ya kupiga kura za maoni za kuchagua mbunge kwenye kura za maoni wanapaswa kuwa hai kwa kulipia kadi za chama, wawe wameorodheshwa kwenye daftari la tawi na wawe na kadi ya kupigia kura.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment