Na
John Gagarini, Kibaha
MBUNGE wa Viti Malumu Zainab Vulu ameshinda
kwenye uchaguzi wa Viti Maalumu kupitia Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa
wa Pwani kwenye uchaguzi kwa kupata kura 342.
Uchaguzi
huo ambao ulifanyika juzi mjini Kibaha ulishuhudia Mbunge mwingine wa viti
maalumu wa mkoa huo Subira Mgalu naye alifanikiwa kushinda kwa kujipatia kura
296.
Nafasi
ya tatu ilichukuliwa na Nancy Mtalemwa aliyejinyakulia kura 145 huku Alice
Mwangomo kura 45, Dk Zainab Gama kura 43, huku Katibu wa CCM mkoa wa Pwani
Joyce Masunga na wengine watano wakiambulia kura saba kila mmoja.
Mbunge
wa zamani wa Jimbo la Kibaha Mjini Dk Zainab Gama alishinda kupitia mashirika
yasiyo ya Kiserikali (NGO) ambaye alijinyakulia kura 394 akifuatiwa na
Elizabeth Maya 37 na Esta Juma kura 15.
Nafasi
ya ubunge kupitia nafasi ya ulemavu mshindi alikuwa ni Sita Sakawa aliyepata
kura 262 ambaye alimshinda Tungi Mwanjala aliyepata kura 178, kwa upande wa
ubunge wafanyakazi Hawa Chakoma alishinda kwa kupata kura 354 akimshinda
Julieth Mjale aliyepata kura 82.
Upande
wa Vyuo vikuu mshindi alikuw ani Dk Alice Kaijage ambaye hakuwa na mpinzani
alipata kura 453 ambapo jumla ya wapiga kura walikuwa zaidi ya 450.
Moja
ya wasimamizi wa uchaguzi huo mkuu wa mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo ambaye
alitangaza matokeo hayo alisema kuwa uchaguzi huo umefanyika kwa kuzingatia
taratibu zilizowekwa na chama.
Ndikilo
alisema kuwa uchaguzi ulikwenda vizuri na kutokana na ukomavu wa wagombe
ahakukutokea matatizo yoyote kwani kila upande uliridhika na matokeo hayo bila
ya kupinga.
Kwa
upande wake Zainab Vullu aliwashukuru wapiga kura kwa kuweza kumchagua kuwa
mwakilishi wao na kusem akuwa atahakikisha anakabiliana na changamoto hususan
kwa akinamama kwa kuwawezesha kwa mafunzo ya ujasiriamali.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment