Na John Gagarini,
Msoga
JUMLA ya watu milioni
11,248,194 wameandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura zoezi ambalo
linaendelea kwa sasa hapa nchini likiwa limeingia mkoani Pwani.
Hayo yalisemwa leo kwenye
Kijiji cha Msoga kata ya Msoga wilayani Bagamoyo na mwenyekiti wa Tume ya
Uchaguzi ya Taifa Damian Lubuva alipokuwa anampa taarifa Rais Dk Jakaya Kikwete
mara baada ya kujiandikisha.
Lubuva alisema kuwa
malengo ni kuandikisha watu milioni 21 hadi 23 kote nchini mara zoezi hilo
litakapokamilika kati ya Julai mwishoni au Agosti mwanzoni kama hakutatokea matatizo.
“Hadi sasa ni mikoa 11
inaendelea na zoezi ambayo ni Mwanza Shinyanga, Geita, Simiyu, Mara, Manyara,
Arusha, Kilimanjaro Morogoro na jana ulianza mkoa wa Pwani,” alisema Lubuva.
Aidha alisema kuwa
changamoto zilizojitokeza ni za kawaida hasa kutokana na mfumo huu kuwa ni mpya
kwani kila jambo jipya lina changamoto zake.
“Mfumo huu ni mpya
hivyo lazima kuwe na changamoto za hapa na pale lakini zoezi linakwenda vizuri
na tunaamini kuwa tutafanikiwa kama tulivyopanga,” alisema Lubuva.
Mkoa wa Pwani una
jumla ya vituo 1,752 na mashine za BVR 932 ambapo kata ya Msoga kuna jumla ya
vituo 17 zoezi hilo kwa mkoa wa Pwani lilianza jana na litamalizika Julai 20.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment