Na John Gagarini, Kibaha
ZOEZI la uandikishaji Daftari la Kudumu
kutumia mfumo mpya wa (BVR) wilayani Kibaha mkoani Pwani limekumbwa na
changamoto ikiwemo wananchi kutumia muda mwingi kuandikishwa.
Baadhi ya wakazi wa mtaa wa Ungindoni Kata
ya Kongowe waliozungumza na Wapo Radio leo wamesema kuwa zoezi hilo linakwenda
taratibu sana kutokana na waandikishaji.
Wananchi hao ambao ni Leonard Mhina na
Seleman Kumchaya wamesema kuwa wanasiku mbili lakini hadi leo siku ya tatu bado
hawajafanikiwa kuandikishwa.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Mtaa wa
Ungindoni Juma Njwaka amesema kuwa wananchi wanaoshindwa kuandikishwa ni wale
ambao wanashindwa kufuata utaratibu.
Naye Ofisa Mtendaji wa Mtaa huo wa
Ungindoni Magesa Lukale amesema kuwa maopareta wa mashine hizo wanafanya kazi
vizuri labda tatizo ni kwa wazee ndiyo wanaochukua muda mrefu kutokana na
kujieleza.
No comments:
Post a Comment