Na John Gagarini,
Kibaha
BONDIA Zumba Kukwe
wa Maili Moja wilayani Kibaha Mkoani Pwani ambaye leo anapambana na bondia
Sweet Kalulu amesema kuwa lengo lake kubwa ni kupambana na Thomas Mashali au
Kalama Nyilawila.
Akizungumza na
waandishi wa habari jana mjini Kibaha wakati wakipima uzito na kupima afya
kwenye ukumbi wa Container Bar alisema kuwa leo atamshinda mpinzani wake raundi
ya tatu.
Kukwe alisema kuwa
kwenye pambano lake la leo anatarajia kufanya vizuri kwa kumpiga mpinzani wake
na kuwapa raha wapenzi wa ngumi wa mkoa wa Pwani.
“Nimejipanga vizuri
kwenye pambano langu na sitawaangusha wapenzi wangu kwani niko kwenye uwanja wa
nyumbani, naangalia mbele zaidi ninaowataka ni Mashali au Nyilawila,” alisema
Kukwe.
Aidha alisema kuwa
anatarajia kuiweka Pwani kwenye ramani ya mchezo huo wa ngumi hivyo malengo
yake ni kupambana na mabingwa wa Tanzania.
“Najiamini kuwa
nina uwezo na baada ya pambano la leo safari yangu ya kuanza kutamba kwenye
ulimwengu wa ngumi itaanza na nitahakikisha ngumi inakuwa juu mkoani Pwani,” alisema
Kukwe.
Kwa upande wake
Kalulu alisema kuwa yeye hana maneno mengi anachosubiri ni muda tu ufike na
kila mtu atajua nini kilichomleta Kibaha
kwnai anauwezo.
Naye muandaaji wa
pambano hilo George Nyasulu alisema kuwa lengo la kuandaa pambano hilo ni
kuwahamasisha vijana wanaopenda mchezo huo kujitokeza ili kucheza mchezo huo.
Nyasulu alisema
kuwa huo ni mwanzo kwani baadaye ataandaa mapambano mengi zaidi na nia ni kutoa
bingwa wa ngumi Taifa kwani vijana wana uwezo.Jumla ya mapambano saba ya
utangulizi yatachezwa.
No comments:
Post a Comment