Na John Gagarini,
Kibaha
WANANCHI wa Maili
Moja wilayani Kibaha mkoani Pwani wametakiwa kujiunga na klabu za mazoezi kwa
ajili ya kuboresha afya zao pamoja na kuinua vipaji vya michezo.
Hayo yalisemwa mjini
Kibaha na mke wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Selina Koka alipokuwa
akizindua klabu ya mazoezi ya Makapalo Jogging Club ya Maili Moja Shuleni chini
ya chama cha msalaba Mwekundu.
Koka alisema kuwa
mazoezi ni sehemu ya kujenga afya bora kukabiliana na maradhi yanayotokana na
kutofanya mazoezi.
“Ufanayaji wa
mazoezi unasaidia kukabiliana na magonjwa ambayo endapo mtu akifanya mzaoezi
anaweza kuyaepuka kama vile kisukari, uzito na homa,” alisema Koka.
Alisema kuwa baadhi
ya watu wamekuwa hawana utamaduni wa kufanya mazoezi lakini mazoezi ni dawa ya
kukabiliana na magonjwa ambayo wanaweza kuyamudu kama watafanya mazoezi.
“Mazoezi kwa sasa
ni kila kitu hivyo watu wakijiunga na vilabu hivi vya mazoezi itasaidia
kukabiliana na maradhi pia tutawajengea vijana kupenda michezo na kuinua vipaji,”
alisema Koka.
Aidha aliwataka
wananchi kujijengea utamaduni wa kufanya mazoezi kila wakati hasa nyakati za
asubuhi na jioni.
Awali akimkaribisha
Koka mwenyekiti wa klabu hiyo Tekla Clemence alisema kuwa changamoto kubwa
inayowakabili ni vifaa vya mazoezi ambapo walipatiwa kiasi cha shilingi 150,000
kwa ajili ya ununuzi wa vifaa.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment