Na John Gagarini, Kibaha
HUKU zoezi la kuandikisha usajili na utambuzi wa watu mkoa wa
Pwani kuanza zoezi hilo Julai 2 mwaka raia 11 wa Ethiopia wanashikiliwa na
Jeshi la Polisi mkoani humo kwa kuingia nchini bila ya kibali.
Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi mkoani humo kamishna msaidizi
mwandamizi wa polisi (SACP) Ulrich Matei alisema kuwa raia hao walikamatwa kwa
kushirikiana na rai wema.
Kamanda Matei alisema kuwa tukio hilo lilitokea Julai Mosi
mwaka huu majira ya saa 3 usiku Kijiji cha Ukuni kata ya Dunda Tarafa ya
Mwambao wilaya ya Bagamoyo.
Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Amoree Achem (22), Worko
Hule (26), Basiad Tekiara (38), Anamaiyo Ramri (21), Fekri Angole (23), Kassa
Dewenj (28) na Antiosogaso Suraj (20).
Wengine ni Abara Charkiso (30), Mmbarak Diljigab (30),
Nichacho Abiche (32) na Kafasa Serecho (40).
Aidha alisema kuwa watuhumiwa hao watakabidhiwa idara ya
uhamiaji kwa taratibu zingine za kisheria ili wajibu tuhuma zinazowakabili za
kuingia nchini bila ya kibali.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment