Na John Gagarini, Kibaha
Mkuu wa mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza amewataka wakazi wa
mkoa huoa kujitokeza kwenye zoezi la uandikishaji wa vitambulisho vya Taifa
linaloanza leo mkoani humo kwani zoezi
hilo ni muhimu sana linasaidia na ni
mfumo mkuu wa utambuzi na usajili wa watu na mifumo mingine ya serikali.
Mahiza amesema kuwa vitambulisho vitasaidia kupunguza riba ya
mikopo ya benki, kuondoa ukiritimba wa kufungua akaunti, kutambua wakwepaji wa
kurejesha mikopo ya benki, kupunguza wafanyakazi hewa, kupata malipo ya
pensheni, haki za matibabu, kuwatofautisha wageni na wakimbizi na rai wa
Tanzania.
Ameyasema hayo mjini Kibaha wakati wa uzinduzi wa zoezi la
usajili na utambuzi wa watu mkoa wa Pwani uliowahusisha wakuu wa wilaya,
wakurugenzi wa halmashauri, wanasiasa na viongozi wa dini.
Kutokana na kutotambulika wananchi hao kumesababisha wameshindwa
kujiongezea uwezo wa kipato chao pamoja na cha Taifa hali ambayo imefanya
uchumi kushindwa kukua.
Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya vitambulisho
vya Taifa Dickson Maimu amesema kuwa Maimu amesema kuwa kutokana na wananchi
hao kutokuwa na utambulisho imesababisha kushindwa kunufaika na rasilimali
fedha na fursa zingine kutokana na kutotambuliwa rasmi na mifumo husika.
Amesema Kutokana na hali hiyo serikali imaenza kutoa vitambulisho
vya Utaifa ambavyo sasa vitawafanya wananchi wa Tanzania kutambulika na wale
wasio raia nao watatmbuliwa hivyo kila kundi litajulikana.
Aidha amesema kuwa wananchi hao endapo watapatiwa
vitambulisho wataweza kujijengea uwezo wao wenyewe kupitia taasisi za kifedha
na sehemu nyingine hivyo kufanya uchumi wan chi kukua pia kwa wale wanaokopa
mkopo utachukua muda mfupi.
Amebainisha kuwa Wananchi wanapaswa kujitokeza kutoa taarifa
zao ili waweze kupata vitambulisho hivyo vya utaifa kwani mtu kama utaifa wako
hautambuliki basi inakuwa ni tatizo na kushindwa kupata fursa mbalimbali.
Zoezi hilo lilianza mkoa wa Dar es Salaam na Zanzibar na sasa
limeanza mkoa wa Pwani tangu Julai Mosi mwaka huu na na baadaye Lindi, Mtwara,
Morogoro, Tanga na Kilimanjaro ambapo wananchi wanatakiwa kutoa taarifa sahihi
ili kuweza kupatiwa vitambulisho vya Utaifa.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment