Na John Gagarini, Kibaha
JESHI la Polisi mkoani Pwani linamshikilia Fikiri Mwinyimvua (35)
mkazi wa Mfuru Kivukoni kata ya Marumbo Tarafa ya Maneromango wilaya ya
Kisarawe mkoani Pwani kwa tuhuma za kumlawiti bibi kizee mwenye umri wa miaka (60)
kisha kumwua kwa kumnyonga shingo.
Kabla ya kumwua mtuhumiwa alikuwa akinywa pombe za kienyeji na marehemu lakini aliwahi kuondoka eneo la
kinywaji kisha kumvizi marehemu na kumfanyia vitendo hivyo ambavyo
vilisababisha kifo chake.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Polisi mkoani
Pwani, kamanda mwandamizi msaidizi wa jeshi la polisi (SACP) Ulrich Matei
alisema kuwa tukio hilo limetokea Kijiji cha Mfuru Kivukoni wilayani humo.
Kamanda Matei alisema kuwa tukio hilo Julai 10 mwaka huu
majira ya saa 1:30 usiku Kijijini hapo ambapo mtuhumiwa alimvizia marehemu
kwenye eneo la kichaka kisha kufanya unyama huo.
Katika tukio lingine Nuran Hamis (31) kwa tuhuma ya
kusafirisha bangi kilo 12 akiwa kwenye basi dogo la abiria aina ya Toyota Coaster
lenye namba za usajili namba T 618 CMU.
Kamanda Matei alisema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa jana
majira ya saa 2:00 usiku kwenye kizuizi cha Maliasili cha Kibiti kata na Tarafa
ya Kibiti wilayani Rufiji.
Aidha watu watano wakazi wa Kidongo Chekundu kata ya Magomeni
Tarafa ya Mwambao wilaya ya Bagamoyo wanshikiliwa na jeshi hilo kwa tuhuma za
kukutwa na pombe ya Moshi maarufu kama Gongo lita 21 kwenye matukio tofauti.
Aliwataja wathumiwa hao kuwa ni Hadija Shaban (37), Rajabu
Michael (37), Msafiri Ramadhan (38), Seif Omary (35), Asha Ramadhan (40) pia
wakazi watatu wa Ikwiriri wilayani Rufiji nao walikamatw awakiwa na lita 4 za
pombe hiyo ambao ni Tabia Salehe (31), Hamis Rwambo (27) na Abdul Rwambo (40).
Mwisho.
No comments:
Post a Comment