Thursday, October 22, 2015
johngagariniblog: DK MAGUFULI KUUFANYA MJI WA CHALINZE KUWA WA KISAS...
johngagariniblog: DK MAGUFULI KUUFANYA MJI WA CHALINZE KUWA WA KISAS...: Na John Gagarini, Chalinze MGOMBEA Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk John Magufuli emesema kuwa endapo atachaguliwa kuwa R...
DK MAGUFULI KUUFANYA MJI WA CHALINZE KUWA WA KISASA
Na John Gagarini, Chalinze
MGOMBEA Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk John
Magufuli emesema kuwa endapo atachaguliwa kuwa Rais atahakikisha mji wa
Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani unakuwa moja ya miji ya kisasa na wa
uwekezaji ambapo utakuwa na barabara za juu Fly Over.
Aidha ujenzi huo ambao utakuwa wa barabara sita hadi jijini
Dar es Salaam utagharimu kiasi cha shilingi trilioni 2.3 na Chalinze itakuwa
kiunganishi cha njia hizo kwenda mikoa ya Kasakazini na mikoa ya Kati ambapo
tayari wataalamu wa upembuzi wa ujenzio huo wamelipwa kiaisi cha shilingi billion
7.7.
Aliyasema hayo kwenye mkutano wa kampeni kwenye Jimbo la
Chalinze mkoani humo ambapo alisema kuwa atahakikisha mji huo unakuwa wa kisasa
na huduma zote muhimu zinapatikana hapo na kuwa mji mbadala wa Dar es Salaam.
Dk Magufuli ambaye ni Waziri wa Ujenzi na Miundombinu alisema
kuwa mji huo utakuwa kituo kikubwa cha uwekezaji hapa nchini kwani faida
nyingine iliyopo ni kugunduliwa gesi eneo la Ruvu hivyo kufanya uchumi wa mji
huo kuwa juu na wananchi wataboresha maisha yao na kuwa na maisha bora.
“Msiuze kiholela maeneo yenu kwani baadhi ya watu wanauza
maeneo kwa bei ndogo lakini watakao nunua watakuja kuuza kwa bei kubwa hivyo
huu ni moja ya miji itakayokuwa ya kisasa hapa nchini na sasa maisha bora
yanakuja na sitawaangusha naomba mnipigie kura nyingi za kutosha ili niweze
kuwa Rais,” alisema Dk Magufuli.
Alisema kuwa kuhusu changamoto ya maji kwenye mji huo alisema
kuwa atahakikisha suala hilo linakwisha ambapo aliipongeza awamu ya tatu na nne
ambazo zimejitahidi angalau maji yanapatikana kwani mji huo ulikuwa na tatizo
kubwa la maji.
Katika hatua nyingine amesema anashangazwa na baadhi ya
wanasiasa kusema kuwa fedha zilizokuwa zijenge bandari ya Tanga zimepelekwa
Bagamoyo kisa ni wilaya anayotoka Rais Dk Jakaya Kikwete.
“Kauli kama hizo ni za uchonganishi kwani kila eneo
limetengewa fedha zake kwa ajili ya ujenzi wa Bandari kuanzia Tanga, Mtwara na
Mwanza kote kutajengwa bandari hizo na Bagamoyo ni uwekezaji wa watu binafsi
hivyo hakuna sababu ya kuwachonganisha watu kwa maneno ya uongo,” alisema Dk
Magufuli.
Alibainisha kuwa hizo ni hoja hafifu na hazina msingi wowote
zaidi ya kuleta uchonganishi kwani wanapaswa kutangaza sera zao na si kuongopa
hali ambayo inajenga chuki baina ya wananchi wa eneo fulani na eneo jingine.
Alisisitiza kuwa endapo atapata
ridhaa ya kuongoza atahakikisha ushuru mdogomdogo unaondolewa ili kuwaondolea
kero wananchi ambao wanataka kujiongezea kipato kutokana na shughuli zao za
ujasiriamali.
Kwa upande wake mgombea Ubunge wa
Jimbo hilo la Chalinze Ridhiwani Kikwete alimshukuru Dk Magufuli kwa mipango
hiyo na kusema kuwa changamoto iliyopo ni ujenzi wa kituo cha afya kikub wa ili
kukabiliana na uwingi wa wagonjwa pamoja na majeruhi kwenye kituo cha afya chya
Chalinze.
Ridhiwani alisema kuwa changamoto
nyingine ni maji ambayo licha ya kupatikana bado kuna baadhi ya maeneo hayapati
maji hasa kwenye makmao makuu ya vitongoji ambapo kwa makao makuu ya vijiji
yote yanapata maji kwa asilimia 94 ambapo Dk Magufuli alisema atashughulikia
changamoto hizo endapo atachaguliwa kuwa Rais.
Mwisho
Mgombea Ubunge Jimbo la Chalinze CCM Ridhiwani Kikwete kulia akisalimiana na moja ya wanachama waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni wa Dk John Magufuli kwenye uwanja wa Miembe Saba Chalinze |
Ridhiwani Kikwete akisalimiana na mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Josia Jackson |
Add caption |
Ridhiwani Kikwete na Dk John Magufuli wakiteta kabla ya kuanza mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa Miembe Saba Chalinze |
Ridhiwani Kikwete katikati akiteta jambo na mgombea Urais CCM Dk John Magufuli kushoto ni Amoud Jumaa mgombea ubunge Jimbo la Kibaha Vijijini |
Dk Magufuli katikati wakitetea na Ridhiwani Kikwete kushoto na mjumbe wa kampeni Taifa CCM Abdala Bulembo |
Abdala Bulembo akiwaonyesha wananchi wa Chalinze hawapo pichani namna ya kuwapigia kura wagombea wa CCM ngazi ya Urais |
Ridhiwnai Kikwete akizungumza kwenye mkutano huo wa kampeni |
Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dk John Magufuli akiongea |
Baadhi ya wagombea udiwani wa CCM kwenye Majimbo ya Chalinze na Bagamoyo wakitambulishwa kwenye mkutano huo wa kampeni |
Dk John Magufuli akifurahi jambo na Ridhiwani Kikwete wakifurahia jambo wakati wa mkutano wa kampeni |
Baadhi ya wanachama wa CCM wakiwa wamejazana kwenye uwanja wa Miembe Saba Chalinze kumsikiliza mgombea Urais wa chama hicho Dk John Magufuli |
Sehemu ya umati wa wanachama na wananchi wa Chalinze wakiwa wanawasikiliza wagombea mbalimbali wa CCM |
Wanachama wa CCM wakiwa wamefurika uwanja wa Miembe Saba Chalinze |
Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dk John Magufuli kulia na Ridhiwani Kikwete kushoto wakiombewa duwa mara baada ya mkutano wa kampeni kwenye uwanja wa Miembe Saba Chalinze |
Monday, October 19, 2015
WANAFUNZI HATARINI KUOZWA
Na John Gagarini, Chalinze
WANAFUNZI wawili wa kidato cha tatu waliokuwa wakisoma shule ya sekondari Msata wilayani Bagamoyo mkoani Pwani ambao mwanzoni mwa mwaka jana walilamikiwa na wanafunzi wenzao kuwa wanajihusisha na vitendo vya ushirikina shuleni hapo hali iliyosababisha washindwe kuendelea na masomo wako katika hatari ya kukatishwa masomo kufuatia taarifa kuwa mmoja kaozeshwa kwa mwanaume na mwingine yuko kwenye mipango ya kuolewa.
Wanafunzi hao ambao wanatoka kijiji cha Mkoko kata ya Msata wilayani humo wanadaiwa kuwa wako kwenye hatua hizo baada ya wazazi wao na walezi kushindwa kuwafanyia uhamisho kwenda shule nyingine baada ya wanafunzi wenzao kuwakataa kutokana na madai hayo ya ushirikina.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi moja ya wakazi wa kijiji hicho ambaye hakutaka kutajwa jina lake kutajwa alisema kuwa mwanafunzi wa kwanza (17) anaishi na mwanaume baada ya baba yake kumwoza.
Alisema kuwa baba wa mwanafunzi huyo Damian Joseph alifikia hatua hiyo baada ya mwanae kugoma kuendelea kusoma kwenye shule hiyo na kutaka ahamishiwe shule nyingine kutokana na wenzake kumtuhumu kuwa ni mshirikina.
Baba wa mwanafunzi huyo Joseph alipoulizwa juu ya suala hilo alikanusha na kusema kuwa hajamwoza mwanaye na hana mpango wa kumwozesha kwa kuwa bado ni mwanafunzi ila tatizo lilikuwa ni uhamisho na kufiwa na mkewe.
Akielezea juu ya tatizo la mwanae alisema kuwa mwanawe alikuwa ni mnyonge na kukata tamaa ya kusoma kutokana na wanafunzi wenzake kumtuhumu kuwa ni mchaawi na anawaloga wanafunzi wenzake yeye na mwenzake ambao wanatoka Kijiji kimoja hivyo walishindwa kwenda shule na yeye alikataa kurudi shuleni vinginevyo ahamishiwe shule nyingine.
Joseph alisema kuwa jambo lililomfanya ashindwe kumhamisha mwanae ni kutokana na msiba wa mkewe uliomfanya achanganyikiwe hivyo kusimamisha taratibu za kumhamisha shule hata hivyo amesema kuwa atahakikisha mwanae anawekwenda shule.
Kwa upande wa mwanafunzi (17) ambaye alidaiwa yuko kwenye mchakato wa kutolewa mahari na mwanaume kaka wa mwanafunzi huyo Ramadhan Ndege alikanusha taarifa hizo na kusema kuwa mdogo wake yuko kwa bibi yake mzaa mama ambapo kwa sasa anazaidi ya miezi sita hajaenda shule kutokana na kuwa na matatizo ya mapepo.
Ndege alisema kuwa si kweli kuwa mdogo wake yuko kwenye mpango wa kuozeshwa ila yuko kwa bibi yake akipatiwa matibabu ambapo akienda shule hali inakuwa mbaya kutokana na mapepo kumsumbua.
“Changamoto nyingine ni kukosa fedha kwa ajili ya kumfanyia uhamisho kiasi cha shilingi 250,000 ambazo ni gharama zote kuanzia ufuatiliaji pamoja na sare, vitabu na vifaa vinavyotakiwa kwenye shule anayokwenda ya Changarikwa ambayo ni jirani na kijiji hicho,” alisema Ndege.
Alisema kuwa tatizo kubwa linalowasumbua ni ukosefu wa fedha kwani kipato chao ni kidogo na hawawezi kupata fedha hizo kwa mara moja na msaada ni mdogo kwani wazazi wao walishafariki nakuomba kama kuna wafadhili wanaoweza kuwasaidia wajitokeze ili kuwasaidia kumpeleka shule ndugu yao.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Kijiji hicho Hamis Buzoza alisema kuwa mambo hayo yalikuwa yakifanywa kifamilia zaidi lakini masuala hayo hayajapelekwa ofisini kwake ila aliwataka wazazi wa familia hizo kutofanya hivyo kwani hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Mwisho.
WAFUGAJI WALIOINGIA KINYEMELA BAGAMOYO KUONDOLEWA
Na John
Gagarini, Chalinze
WILAYA
ya Bagamoyo imesema kuwa itawaondoa wafugaji wote walioingia kinyemela kwenye wilaya
hiyo ili kuepusha migogoro ya wakulima na wafugaji.
Hayo yalisemwa
na mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Hemed Mwanga, wakati akizungumza na wakazi wa
Kijiji cha Kihangaiko wilayani humo.
Mwanga
alisema kuwa kuna baadhi ya wafugaji wameingia kinyemela kwenye wilaya hiyo
jambo ambalo ni kinyume cha taratibu.
“Tuna
taarifa tunazo kuwa kuna baadhi ya wafugaji wanaingia kinyume cha taratibu hali
ambayo inaweza kusababisha vurugu baina ya wakulima na wafugaji,” alisema
Mwanga.
Alisema
kuwa wafugaji wote walioingia kwa njia za panya wataondolewa kwani kila mahali
kuna taratibu zake na kama walikuwa wanataka kuingia walipaswa kufuata
taratibu.
“Wafugaji
walioingia kinyume cha utaratibu wataondolewa na tumepata taarifa kuwa baadhi
ya mgambo wamekuwa wakihusika kuwaingiza wafugaji hao kinyume cha utaratibu
pale Mto Wami,” alisema Mwanga.
Aidha alisema
kuwa wale wote wanaohusika kuwaingiza wafugaji hao kinyume cha utaratibu
watashughulikiwa kwani wanataka kutoletea matatizo.
Mwisho.
WAOMBWA KULIPWA FIDIA UPANUZI WA BARABARA
Na John
Gagarini, Chalinze
WAKAZI
wa Kijiji cha Misani kata ya Kiwangwa wilayani Bagamoyo mkoani Pwani wameiomba
serikali kuibana kampuni Eco Energy kuwalipa fidia ya mali zao ili kupisha
upanuzi wa barabara ya kuelekea kwenye mradi wa umwagiliaji.
Wakizungumza
kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia Chama Cha
Mapinduzi (CCM) Ridhiwani Kikwete ambapo wakazi wa Kijiji hicho walisema kuwa tathmini
ya upanuzi huo haukuwashirikisha wananchi na utaathiri mali zao.
Mkazi wa
Kijiji hicho aliyejitambulisha kwa jina la Ally Hemed alisema kuwa mradi huo
ambao ni wa kampuni hiyo ambapo imeweka alama za kupita barabara hiyo na kusema
kuwa hakutakuwa na fidia yoyote itakayotolewa kwa uharibifu wa mali zao.
“Wamekuja
hapa kijijini na kuweka alama za kuonyesha barabara itapita wapi ambapo katika
maeneo hayo kuna mali zetu zitaathiriwa ikiwa ni pamoja na nyumba, mazao ya
nanasi, miti na vitu vingine ambapo tumeambiwa kuwa hatutalipwa chochote jambo
ambalo tunaona kuwa hatutatendewa haki mara zoezi hilo litakapoanza,” alisema
Hemed.
Alisema
kuwa kutokana na kutolipwa wao hawako tayari kuruhusu greda la kuchonga
barabara kupita kwenye maeneo yao hadi watakapolipwa fidia za mali zao.
“Hatuna
tataizo na kuchongwa barabara yetu lakini tunachoomba tulipwe kwanza fidia
ndipo upanuzi ufanyike kama unavyoona mananasi yetu karibu yatakomaa na nyumba
zetu zinaonekana zipo kwenye eneo la upanuzi wao watulipe kwanza ndipo wafanye
upanuzi huo,” alisema Hemed.
Kwa upande
wake mgombea udiwani kata ya Kiwangwa Malota Kwaga alisema kuwa jambo hilo
limekuwa ni kero kubwa kwa wakazi hao hivyo ni vema suala lao likaangaliwa
kabla ya utekelezaji wake.
Kwaga alisema
kuwa wananchi wametoa malalamiko yao kwa wahusika lakini hawajaonesha nia ya
kutoa fidia kwa watu ambao wataathiriwa na zoezi hilo.
Naye
Ridhiwani alisema kuwa wahusika hao wanapswa kulipa fidia kabla ya kutekeleza
mradi huo kwani haipendezi watu kuharibiwa mali zao bila ya kulipwa fidia.
Ridhiwani
alisema kuwa tayari amewasiliana na wahusika na kuwaambia kuwa walipe kwanza
fidia kabla ya kuanza upanuzi huo wa barabara hiyo inayoelekea kwenye mradi
huo.
“Sheria haisemi hivyo lazima unapofanya suala
la maendeleo kwenye ardhi lazima ulipe fidia kwenye maeneo ambayo unayaendeleza,”
alisema Ridhiwani.
Aidha alisema
kuwa jambo hilo ni la maendeleo lakini pia liangalie haki za wananchi ambao
mali zao zitaathiriwa na maendeleo hayo hivyo kwa sasa hakutafanyika chochote
hadi malipo yatakapofanyika.
Mwisho.
Sunday, October 18, 2015
HABARI MOTO MOTO ZA KAMPENI ZA UCHAGUZI UCHAGUZI JIMBO LA CHALINZE
Na John Gagarini, ChalinzeMGOMBEA Ubunge Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ridhiwani Kikwete amekanusha kumtuma mgombea wa Chama Cha (SAU) Shaban Maulid kugombea Udiwani Kata ya Talawanda.Akizungumza kwenye mikutano ya kampeni iliyofanyika kwenye Vijiji vya Kisanga, Vundumu na Talawanda kwenye kata hiyo alisema kuwa yeye hajamtuma mtu huyo wala hajawahi kukutana naye.Ridhiwani alisema kuwa yeye hawezi kumtuma mtu kwenda kugombea na kama ni kumtaka mtu basi angependekeza kutoka chama chake na si chama kingine kwani hakuna ushirikiano na vyama vingine.“Huyo mtu kwanza na mshangaa kwani sijawahi kumuona wala sijawahi kukutana naye wala sijawahi kumtuma mtu namshangaa unajua wagombea wengine hawana sera hivyo wanatumia majina ya watu kujipatia umaarufu,” alisema Ridhiwani.Alisema kuwa huo ni uzushi na wananchi hawapaswi kumsikiliza mtu huyo kwani chama chake hakina uhusiano na CCM wala na yeye na hajawahi hata kukutana naye.“Achaneni na maneno ya kutuvuruga kwani kwa sasa sisi tunafanya kampeni ili kuhakikisha chama cehtu kinashinda kwenye nafasi zote ikiwemo Urais, Ubunge na Udiwani hivyo wasituvurge wakati huu wa kampeni kama hawana sera wakae pembeni,” alisema Ridhiwani.Kwa upande wake meneja wa kampeni Jimbo la Chalinze Alhaj Amir Mkangata alisema kuwa anamshangaa mgombea huyo kwani hakuna muungano baina ya CCM na SAU kama ilivyo kwa muungano wa vyama vya upinzani vinavyounda UKAWA.Alhaj Mkangata alisema kuwa wagombea kama hao hawana uwezo hivyo wanatafuta njia ya kujipenedekeza ili kuonyesha kuwa wametumwa kugombea.“CCM haijaungana na chama kingine sasa mgombea huyo anavyojitapa kuwa ametumwa na CCM atuambie umoja huo unaitwaje atuambie hapa na tunamshangaa aache kabisa kutengeneza maneno ya uongo,” alisema Mkangata.Kwa upande wake mgombea udiwani kata ya Talawanda Said Zikatimu alisema kuwa endapo atachaguliwa atahakikisha kuwa changamoto zilizopo kwenye kata hiyo zikiwemo za Afya, Elimu na Maji.Mwisho.Na John Gagarini, ChalinzeWAKULIMA na Wafugaji kwenye Kijiji cha Lulenge Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani wametakiwa kuheshimiana ili kuepusha migogoro inayoweza kujitokeza na kusababisha vurugu zinazopelekea kuvunja amani baina ya wananchi.Hayo yalisemwa na mgombea Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ridhiwani Kikwete wakati wa mkutano wa kampeni kwenye kijiji cha Lulenge kata ya Ubena.Ridhiwani alisema kuwa tatizo kubwa la migogoro linatokana na pande mbili hizo kutoheshimu mipaka yao kwani kuna baadhi ya maeneo yametengwa kwa jamii hizo mbili.“Mnaweza kuepusha migogoro kwa kuheshimiana na kuheshimu mipaka iliyopo kwani kila mmoja akimweshimu mwenzake migogoro haitakuwepo na watu wataishi kwa Amani na upendo,” alisema Ridhiwani.Alisema kuwa serikali inajitahidi kuhakikisha inaondoa migogoro ikiwa ni pamoja na kutenga maoeneo kwa ajili ya mipango ya matumizi bora ya ardhi wakulima na wafugaji kwa baadhi ya maeneo huku mengine yakiwa yanaandaliwa kufanywa hivyo.“Nyie ni ndugu hakuna sababu ya kugombana na kuingia kwenye migogoro isiyokuwa ya lazima kwani mtashindwa kufanya shughuli za maendeleo kutokana na migogoro hiyo,” alisema Ridhiwani.Naye mgombea udiwani kupitia chama hicho Nicholaus Myuwa alisema kuwa atatumia taaluma yake ya kuwa Mwanasheria kuikabili migogoro hiyo kwa kuziweka pamoja jamii hizo.Myuwa alisema kuwa endapo atachaguliwa kuwa diwani watahakikisha changamoto za maji, zahanati na barabara zinatatuliwa kwa kuwashirikisha wananchi.Mwisho.Na John Gagarini, ChalinzeWANANCHI wa Jimbo la Chalinze wametakiwa kutowachagua wagombea wa vyama vya upinzani kwani wengi wao ni viongozi wa msimu ambao wanajitokeza nyakati za uchaguzi.Hayo yalisemwa na meneja wa kampeni wa Jimbo hilo Alhaj Amir Mkangata wakati wa mikutano ya kampeni ya mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ridhiwani Kikwete kwenye kata ya Miono.Alhaj Mkangata alisema kuwa chama chenye uwezo wa kuwaletea maendeleo wananchi ni CCM na vyama vingine viongozi wao hawana uwezo hivyo ni vema wakaendelea kukiamini chama.“Msiwachague wapinzani kwani wengi wao wanajitokeza wakati wa uchaguzi lakini uchaguzi ukishaisha hawaonekani hivyo mkiwachagua hamtawapata kwani wengine hawajulikani hata wanapoishi lakini wa CCM wanafahamika na wanatambulika,” alisema Alhaj Mkangata.Alisema kuwa CCM imechagua wagombea wenye uwezo na wanasifa za kuongoza lakini wagombea wa upinzani hawana uwezo wa kuongoza hivyo hakuna sababu ya kuwachagua.“CCM imefanya kazi kubwa ya kuwaletea wananchi maendeleo hivyo hakuna sababu ya kuchagua chama kingine kutawala hivyo msihadaike na wapinzani ambao wanaongopa kuwa wataleta maendeleo msikubali kudanganyika,” alisema Alhaj Mkangata.Aidha alisema kuwa kwa mwaka huu chama kimejipanga kuhakikisha kinapata ushindi wa kishindo ili kiweze kuongoza na kuleta maendeleo kwa wananchi.Aliwataka wananchi kuichagua CCM kwani ina uwezo wa kuongoza na wagombea walioingia kwenye kinyanganyiro cha ugombea kwenye ngazi mbalimbali wana uwezo kwani wamechaguliwa kwa uwezo wao.Mwisho.Na John Gagarini, ChalinzeKIJIJI cha Lulenge kata ya Ubena Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo kinatarajia kuanza ujenzi wa zahanati Desemba mwaka huu ili kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa huduma za afya.Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mwenyekiti wa Kijiji hicho Lucas Sultan alisema kuwa ujenzi huo utaanza baada ya kukamilika michango ya kila kaya.Sultan alisema kuwa walikubaliana kwenye mkutano wa Kijiji kila kaya itoe kiasi cha shilingi 20,000 kwa ajili ya kujenga zahanati kwa ajili ya kuwapatia huduma ya afya.“Tayari tuna eneo la ukubwa wa hekari tano kwa ajili ya kufanya ujenzi huo kwani ndani ya miezi michache ijayo tutakuwa tumekamilisha michango hiyo ili kuanza ujenzi,” alisema Sultan.Alisema kuwa kwa kaya itakayoshindwa kutoa mchango huo atapaswa kufanya shughuli za kijamii kama sehemu ya mchango wake ili kila mtu atoe jasho lake kwenye kijiji.Alisema kuwa kwa sasa wanapata huduma ya afya kwenye zahanati binafsi ambako ni mbali kwani usafiri uliopo ni wa pikipiki ambapo gharama yake ni shilingi 8,000 kwenda na kurudi.“Gharama za kwenda kupata matibabu ni kubwa sana hivyo ndiyo maana tuliona kuwa kuna haja ya kweza kuanzisha ujenzi wa zahanati ili kukabiliana na changamoto hiyo,” alisema Sultan.Aidha alisema kuwa changamoto nyingine ni kwamba sehemu kubwa ya kijiji iko kwenye hifadhi ya Wami Mbiki hivyo kushindwa kufanya shughuli za kimaendeleo.“Suala la Kijiji kuwa kwenye hifadhi linafanyiwa kazi na tunaamini tutapata majibu mazuri na tunaamini mipaka itatengenezwa na tutaishi kwa utaratibu mzuri,” alisema Sultan.Alisema kuwa Kijiji hicho kina jumla ya wakazi wapatao 2,700 huku kukiwa na mifugo mbalimbali ngombe wakiwa 17,000, mbuzi 4,000 na mbuzi 2,000 ambapo wakazi wake ni wakulima na wafugaji.Mwisho.Na John Gagarini, ChalinzeMGOMBEA Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ridhiwani Kikwete amesema kuwa endapo atafanikiwa kuwa mbunge atahakikisha anasimamia upelekwaji wa fedha pensheni za wazee kwa wakati.Aliyasema hayo katika kijiji cha Tukamisasa kata ya Ubena na kusema kuwa wazee wanapaswa kuheshimiwa na kupewa stahiki zao kwani wamefanya kazi kubwa ya kuifanya nchi ifikie hapa ilipo.Ridhiwani alisema kuwa kwa kuwa sera ya chama inaonyesha kuwa kuanzia mwaka 2016 wazee watakuwa wanapata pensheni zao kwa ajili ya kuwasaidia katika maisha yao.“Wazee wetu wamefanya kazi kubwa hivyo kuna haja ya kuhakikisha wanapata stahiki zao kwani walifanya kazi kubwa kuikomboa nchi na kuifanya iwe kama ilivyo sasa moja ya vitu nitakavyovisimamia ni kuhakikisha fedha zao zinakuja kwa wakati,” alisema Ridhiwani.Alisema kuwa wazee wanakabiliwa na changamoto nyingi hivyo wakipata pensheni zao zitawasaidia kuweza kujikimu na kumudu mambo madogomadogo tofauti na ilivyo sasa.“Wazee wakilipwa pensheni zao zitawasaidia kumudu maisha yao kwani walikuwa wakiishi kwenye hali ngumu kutokana na kukosa fedha hata za kununua vitu vidogovidogo ambavyo vingewasaidia kumudu maisha,” alisema Ridhiwani.Aidha wazee wamehudumia nchi ya Tanzania na kutumia nguvu zao na jasho lao hivyo ni haki yao sasa kupata pensheni ambayo itawafanya wajisaidie kwenye maisha yao.“Mbali ya kusimamia malipo hayo pia nitahakikisha wanapata huduma mbalimbali ambao ni fursa kwao ikiwa ni pamoja na matibabu pamoja na mikopo ambayo itawasaidia kwenye ujasiriamali,” alisema Ridhiwani.Mwisho.
Wednesday, October 14, 2015
RIDHIWANI AMWAGIA SIFA DK MAGUFULI
Na John Gagarini, Chalinze
MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk John
Magufuli amepongezwa kwa kuuachia mkoa wa Pwani hususani wilaya ya Bagamoyo
miradi mikubwa ambayo itakapokamilika itasaidia kuinua kipato cha wakazi wa
mkoa huo.
Miradi hiyo ambayo inatoka kwenye Wizara Ujenzi na
Miundombinu aliyokuwa akioongoza Dk Magufuli kabla ya kuteuliwa na chama chake
kuwa mgombea Urais kwenye kinyanganyiro kitakachofanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Pongezi hizo zimetolewa na mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze
kupitia chama hicho Ridhiwani Kikwete, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika
kwenye Kijiji cha Miono wilayani Bagamoyo na kusema kuwa mgombea huyo kila mkoa
ameupatia miradi ambayo itachochea maendeleo.
Ridhiwani alisema kuwa Dk Magufuli ni kiongozi ambaye
anastahili kuongoza nchi hii kwani wakati akiwa waziri alihakikisha kila mkoa
unatumia rasilimali zake viuzuri ili kujiletea maendeleo hali ambayo
imesababisha nchi kupiga hatua.
“Sisi wakazi wa wilaya ya Bagamoyo tunamshukuru kwani ametuachia
miradi mikubwa ikiwa ni pamoja na ule wa Barabara ya Afrika Mashariki
itakayoanzia Bagamoyo, Makuruge, Saadani hadi mkoa wa Tanga hadi Mombasa nchini
Kenya,” alisema Ridhiwani.
Alisema kuwa mradi mwingine ni ule wa Bandari ambayo itakuwa
ni kubwa ambao utaanza wakati wowote kuanzia sasa kwani mipango tayari
imekamilika huku mradi wa barabara tatu zitakazoanzia Jijini Dar es Salaam hadi
mkoani Morogoro pia mzaini wa kisasa uliopo Vigwaza ambao tayari unafanya kazi.
“Mradi mwingine ni ule wa upanuzi wa Daraja la Mto Wami ili
kupunguza ajali zinazotokea kwenye daraja hilo ambapo kwa sasa magari hayawezi
kupishana, hakika miradi hii ni mikubwa na itafungua fursa za maendeleo kwa
kukuza uchumi wao kutumia fursa zilizopo na zitakazokuwepo kwenye miradi hiyo,”
alisema Ridhiwani.
Aidha alisema Dk Magufuli ni kiongozi ambaye hana kashfa
yoyote na ameonyesha kuwa anafaa kuliongoza Taifa la Tanzania kutokana na
uchapa kazi wake pamoja na uadilifu aliokuwa nao ukilinganisha na viongozi
wengine wanaowania nafasi hiyo.
Aliwataka watanzania kumchagua kwa kumpiga kura nyingi za
kishindo ili awe Rais wa awamu ya tano na anaamini kuwa uwezo wa kuongoza nchi
anao akiwa chini ya CCM ambao kwa wakati huu imechagua viongozi wenye sifa na
wanaopendwa na wananchi.
Mwisho.
Mgombea Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia CCM Ridhiwani Kikwete akizindua huku akiwa amekaa kwenye kigoda tawi la vijana wa Boda boda kwenye Kijiji cha Pongwemnazi |
Mgombea Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia CCM Ridhiwani Kikwete akizindua tawi kwa kupandisha bendera kwenye moja ya matawi wakati wa kampeni kuwania kiti hicho. |
Mgombea Udiwani kata ya Kimange kwa tiketi ya CCM Husein Hadingoka akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Kikwazu wakati wa mkutano wa kampeni |
Mama Mwenye ulemavu ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja akiwa kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea wa CCM Ridhiwani Kikwete kwenye Kijiji cha Pongwemnazi kata ya Kimange. |
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea wa CCM Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete kwenye kijiji cha pongwekiona kata kimange wilayani bagamoyo |
wananchi wa kijiji cha pongwekiona wakiwa wanamsikiliza mgombea ubunge jimbo la chalinze ridhiwani kikwete hayupo pichani wakati wa mkutano wa kampeni |
Mwigizaji aitwaye Puto akitoa burudani kwa wananchi waliohudhuria mkutano wa kampeni kwenye kijiji cha Pongwemnazi kata ya Kimange wilayani Bagamoyo |
Mwimbaji Sam wa Ukweli akiimba na moja ya wananchi kwenye mkutano wa kampeni wa CCM kwenye kijiji cha Pongwemnazi |
Wagombea Ridhiwani Kikwete kushoto akicheza na mgombea Udiwani kata ya Kimange Hussein Hadingoka wakati wa uzinduzi wa kampeni za udiwani kwenye kijiji cha Pongwekiona |
Mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akimkabidhi moja ya wanachama wapya kwenye Kijiji cha Pongwekiona |
Subscribe to:
Posts (Atom)