Na John
Gagarini, Chalinze
WILAYA
ya Bagamoyo imesema kuwa itawaondoa wafugaji wote walioingia kinyemela kwenye wilaya
hiyo ili kuepusha migogoro ya wakulima na wafugaji.
Hayo yalisemwa
na mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Hemed Mwanga, wakati akizungumza na wakazi wa
Kijiji cha Kihangaiko wilayani humo.
Mwanga
alisema kuwa kuna baadhi ya wafugaji wameingia kinyemela kwenye wilaya hiyo
jambo ambalo ni kinyume cha taratibu.
“Tuna
taarifa tunazo kuwa kuna baadhi ya wafugaji wanaingia kinyume cha taratibu hali
ambayo inaweza kusababisha vurugu baina ya wakulima na wafugaji,” alisema
Mwanga.
Alisema
kuwa wafugaji wote walioingia kwa njia za panya wataondolewa kwani kila mahali
kuna taratibu zake na kama walikuwa wanataka kuingia walipaswa kufuata
taratibu.
“Wafugaji
walioingia kinyume cha utaratibu wataondolewa na tumepata taarifa kuwa baadhi
ya mgambo wamekuwa wakihusika kuwaingiza wafugaji hao kinyume cha utaratibu
pale Mto Wami,” alisema Mwanga.
Aidha alisema
kuwa wale wote wanaohusika kuwaingiza wafugaji hao kinyume cha utaratibu
watashughulikiwa kwani wanataka kutoletea matatizo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment