Wednesday, July 1, 2026

NASHUKURU SANA MTANDAO NAJUKWAA KUBWA BELLE NAIJA

ALHAMDULILAH ALLAH NDIYO SHAHIDI WA KILA JAMBO 

Jukwaa kubwa la kidijitali nchini Nigeria linalojihusisha na masuala ya burudani, mitindo, mitindo ya maisha (lifestyle), na harusi za Kiafrika. Ilianzishwa mnamo mwezi Julai mwaka 2006 na mjasiriamali wa Nigeria anayeitwa Uche Pedro (jina la kuzaliwa Uche Eze).

NASHUKURU KUPOSTI PICHA YANGU NA STAA MKUBWA NCHINI NIGERIA NI HESHIMA KUBWA KUTAMBUA MCHANGO WANGU KATIKA AFRIKA 

Layi Wasabi (jina lake halisi ni Isaac Ayomide Olayiwola) ni mchekeshaji, mwigizaji, na mtengeneza maudhui maarufu wa mtandaoni kutoka nchini Nigeria. 

Anajulikana sana kwa uchekeshaji wake wa kipekee na wa akili (philo-comedy) kupitia video fupi (skits) kwenye mitandao ya kijamii

MKUTANO (AFRICA'S CREATIVE FUTURE TAKES CENTRE STAGE IN LUSAKA- (MUSTAKABALI WA UBUNIFU WA AFRIKA WACHUKUA KITUO KIKUU LUSAKA)

ALHAMDULILAH ALLAH NDIYO SHAHIDI WA KILA JAMBO 
LEO TAREHE 29 JUNE 

NIMESHIRIKI  MKUTANO (AFRICA'S CREATIVE FUTURE TAKES CENTRE STAGE IN LUSAKA- (MUSTAKABALI WA UBUNIFU WA AFRIKA WACHUKUA KITUO KIKUU LUSAKA)

Mkutano huu utachukua siku 7 kuanzia tarehe 29 Juni  hadi 5 Julai 

Mkutano huo ulioandaliwa na Wizara ya Vijana, Michezo na Sanaa nchini Zambia Kwa siku tano takribani vijana 3000 kushikiriki 
Kuanzia watengenezaji filamu na wanamuziki hadi wabunifu wa mitindo, wawekezaji na watunga sera, mamia ya wajumbe kutoka kote barani wamekusanyika katika 

Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mulungushi kwa ajili ya Mkutano wa Biashara wa Viwanda vya Ubunifu wa 2026, Soko la Ubunifu la Afrika (ACM) na Tamasha la Sanaa la Kitaifa la Kwimbo, wakiwa wameunganishwa na lengo moja la kugeuza ubunifu wa Afrika kuwa biashara, ajira na fursa za kimataifa.

Akifungua rasmi mkutano huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Vijana, Michezo na Sanaa, Bw. Kangwa Chileshe, 

Alisema Zambia imepiga hatua kubwa katika kuiweka sekta ya ubunifu katika nafasi nzuri ya kuchangia uchumi wa nchi.

Alitaja mfululizo wa mageuzi yaliyotekelezwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa Sanaa kama idara ndani ya Wizara, uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Sanaa ya kwanza ya nchi, mapitio ya Sera ya Taifa ya Filamu, marekebisho ya sheria iliyopitwa na wakati, kuondolewa kwa ushuru wa uagizaji wa vifaa vya filamu na muziki, na Zambia kujiunga na mfumo wa ATA Carnet ili kurahisisha usafirishaji wa vifaa vya ubunifu kuvuka mipaka.

Bw. Chileshe alisema serikali pia imewekeza kwa wasanii wenyewe, ambapo zaidi ya wabunifu 3,000 wamepatiwa mafunzo ya kusoma na kuandika kuhusu fedha na maendeleo ya biashara, huku zaidi ya 2,000 wameandikishwa kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii ambao hutoa pensheni, mafao ya uzazi, msaada wa mazishi na upatikanaji wa mikopo.

Monday, June 29, 2026

POLISI MKOANI PWANI LINACHUNGUZA VIFO VYA MWANAMKE NA MTOTO

JESHI la Polisi Mkoani Pwani linafanya uchunguzi wa tukio la mauaji ya mwanamke mmoja na mtoto ambao hawakufahamika yaliyotokea Mbwewe Wilaya ya Kipolisi Chalinze Mkoa wa Pwani.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani Salim Morcase kwa vyombo vya habari zilisema kuwa tukio hilo la mauaji ya watu wawili lililotokea Juni 2 mwaka huu  majira ya saa 9:00 alasiri huko Kitongoji cha Nung'uli Kijiji cha Kwang'andu Kata ya Mbwewe Halmashauri ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo.

Taarifa hiyo ilibainika kuwa watu hao ni mwanamke
mmoja anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka (20-25) na mtoto ambaye hakufahamika jinsia yake kutokana na kuungua sana na moto mwenye
umri unaokadiriwa kuwa miaka (3-6) ambao mpaka sasa bado hawajafahamika wala watu waliosababisha mauaji hayo.

"Ikumbukwe katika eneo la tukio hilo zilikutwa tiketi mbili za basi la Passion Video Coach linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam kwenda Miono kupitia Chalinze zilizokatwa tarehe Mei 31 mwaka huu,"alisema taarifa hiyo.

Taarifa zilisema kuwa tiketi hizo zilikiwa na majina ya Adela na Modest ambapo Jeshi bado linachunguza chanzo cha mauaji hayo wakati miili ya wahanga imehifadhiwa katika Hospitali ya Msoga Halmashauri ya Chalinze.

Kutokana na mauaji hayo Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linaendelea kutoa wito kwa mtu yeyote anayewafahamu watu hao au mwenye taarifa zozote zinazoweza kusaidia kuwatambua wafike Ofisi ya kamanda wa Polisi Mkoa
wa Pwani.

 "Au wapige simu namba 073900995, 065837601 0 na 0753855570 ili kuendelea kusaidia uchunguzi na kuwapata ndugu wa marehemu kwa wakati,"iliongeza taarifa hiyo.

AKINAMAMA WATAKIWA KUWAKUMBUKA VIJANA WAKIUME

MWANASIASA mkongwe na aliyewahi kuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Sophia Simba ameitaka jamii kuwawezesha kiuchumi vijana wa kiume ambao wamesahaulika.

Simba ameyasema hayo Mjini Kibaha wakati wa kuadhimisha miaka 10 ya Kikundi cha Super Women 2017 na kuwa baada ya wanawake kufanikiwa vijana wakiume nao waangaliwe.

Amesema kuwa kwa muda mrefu jamii iliwekeza kudai haki za wanawake ambapo kwa sasa wamepiga hatua ya kimaendekeo baada ya nguvu kubwa kutumika huku wale wa kiume wakiwa wamesahaulika.

Simba ambaye pia aliwahi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora alisema kuwa kwa sasa vijana wa kiume wana hali mbaya kiuchumi.

"Tumshukuru Mungu kwani kwa sasa wanawake angalau wamepiga hatua kiuchumi tuwaangalie na vijana wakiume ili nao kwa kuwajengea uwezo wa kiuchumi,"amesema Simba.

Aidha alikipongeza kikundi hicho kwa mafanikio waliyoyapata kwa muda huo tangu kuanzishwa kwake kwani baadhi ya vikundi vinaanzishwa na havichukui muda mrefu vinakufa.

Naye mwanzilishi wa kikundi hicho Beth Msimbe amesema kuwa wamepata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kukopeshana fedha kwa riba nafuu kupitia mfuko wa kikundi kwa fedha wanazoweka ambapo mkopo ni mara tatu ya fedha waliojiwekea.

Msimbe amesema kuwa wameweza kukuza biashara zao na kuwa wafanyabiashara wakubwa pia wamekuwa wakifanya matendo ya huruma kwa watu wenye uhitaji na kuwataka wanawake wawe na wavumilivu kwa kufuata sheria na taratibu.

Kwa upande wake mwenyekiti kikundi hicho Betha Kimambo amesema kuwa wanatarajia kuanzisha mradi wa kukodisha vyombo ili kuongeza kipato ndani ya kikundi.

Kimambo amesema kuwa mbali ya kupata mafanikio kuna baadhi ya changamoto ikiwa ni pamoja na baadhi ya wanachama kujitoa.





Sunday, June 28, 2026

VIJANA WENYE VIPAJI VYA MICHEZO WATAKIWA KUWA NA NIDHAMU

VIJANA wenye vipaji vya michezo nchini wametakiwa kusoma kwabidii na kuwa na nidhamu ili waweze kufikia viwango vya juu na kuwa tegemeo kwa Taifa.

Hayo yamesemwa na Gilbert Maregesi ambaye alimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kibaha wakati wa kufunga tamasha la michezo lililoandaliwa na Compassion Kanda ya Mashariki lililofanyika kwenye Viwanja vya Shirika la Elimu Kibaha Tumbi.

Maregesi amesema kuwa serikali imekuwa ikiwekeza kwenye sekta ya michezo kwa vijana ili kuendeleza vipaji vyao na kuwa tegemeo kwa Taifa kwenye sekta hiyo ambayo pia ni ajira kwa vijana.

"Ili kulinda vipaji vyenu mnapaswa kuwa na nidhamu ili muweze kufika mbali kwani mbali ya kunufaika binafsi pia mtaliwezesha Taifa kuwa na wachezaji wazuri watakaoliwakilisha Taifa kwenye michezo mbalimbali,"amesema Maregesi. 

Naye mwakilishi wa meneja wa Compassion Kanda ya Mashariki Daudi Lawi inayoundwa na mikoa ya Pwani Morogoro na Dar es Salaam amesema tamasha hilo la awamu ya nne limeshirikisha wanamichezo 430 kutoka mikoa hiyo.

Lawi amesema kuwa baada ya kukamilisha tamasha hilo lilobeba ujumbe wa Kipaji changu Mtaji wangu watachaguliwa wachezaji bora ambao watawakilisha Kanda hiyo kwenye mashindano ya Taifa.

Kwa upande wake James Mhina Kanda ya Mlandizi ambao walikuwa wenyeji wa mashindano hayo amesema kuwa michezo hiyo inajenga mahusiano na kipaji ni msaada katika maisha.

Mwenyekiti wa Mashindano hayo Lucas Kiluwasha amesema kuwa vipaji vyao ndiyo mtaji wao hivyo wavitumie vizuri na kuwataka wadau wa michezo kushuhudia michezo ili wachukue vipaji na kuviendeleza.

Rais wa Vijana Kanda ya Mashariki amesema kuwa michezo hiyo imewasaidia kuwaongezea ujuzi na kukuza vipaji vyao na kujumuika na kufahamiana kwani hiyo ndiyo njia ya mafanikio.

Mgeni rasmi ametoa fursa ya vijana Milovan Kilingo kutoka Gairo na Joshua Joakim wa Mkuza Kibaha kujiunga na bendi ya Jkt Ruvu ili waendeleze vipaji vyao.

Baadhi ya michezo iliyochezwa ni pamoja na mpira wa miguu, pete, riadha na michezo ya ndani ikiwemo sanaa ya uimbaji, upigaji wa vyombo vya muziki, maonyesho ya mavazi na sarakasi na yalishirikisha vijana wenye umri chini ya mi 17 na 22.

MWANADIPLOMASIA OMARY PUNZI ATEULIWA KUSHIRIKI MKUTANO WA CREATIVE

Mwanadiplomasia na Mchambuzi wa Masuala ya Kidiplomasia Siasa , Itifaki na Maadili Omary Punzi ateuliwa kushiriki katika mkutano wa Creative Convergence 2026 . 

Mkutano huu unaojumuisha Africa Creative Market (ACM), Creative Industry Business Summit (CIBS), na Kwimbo National Arts Festival, unafanyika kuanzia Juni 29 hadi Julai 4, 2026 jijini Lusaka, Zambia.

Mkutano huo unaisimamiwa na Wizara ya Vijana, Michezo na Sanaa nchini Zambia 

Utafanyika katika  kumbi za mikutano zilizopo Mulungushi International Conference Centre kuanzia Juni 29 hadi Julai 2, 2026 na kuanzia tarehe 3 hadi 4 Julai 

Tamasha la Sanaa,  tamasha la Kwimbo  huko Polo B, Lusaka Showgrounds. 

Mkutano huo utakutanisha Vijana zaidi 10000  kutoka Bara la Afrika.

kushiriki  Programu na Warsha (Sessions & Masterclasses)

Mijadala ya Biashara, Mijadala inayohusu biashara ya sanaa, filamu, muziki, teknolojia (kama AI), na mitindo.

Mafunzo ya Kitaalamu, Ufikiaji wa masterclasses zinazoendeshwa na washirika wa sekta, mfano mafunzo ya upigaji picha au uigizaji.

Kuunganisha Mtandao wa Biashara (Networking & Deal Rooms)

Ushirikiano wa Kibiashara, mikutano ya kibiashara (kama vile Deal Rooms au Creative Pitch Zone) ambapo wabunifu wanakutana na wawekezaji, wafadhili, na watengeneza sera ili kugeuza mawazo kuwa mikataba ya kazi.

MAWAZO YA VIJANA




SERIKALI imesema kuwa itatumia mawazo ya vijana walioshiriki shindano la Vijana Uchumi Challenge kuwa mpango ambao utaleta suluhisho la namna ya kutatua baadhi ya changamoto ndani ya jamii.

Hayo yalisemwa Kibaha na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana Jenifa Omollo wakati wa kufunfa mafunzo ya siku nne kwa vijana 100 walioandika mawazo juu ya masuala ya uchumi kupitia jukwaa la Vijana Uchumi Challenge.

Omollo alisema kuwa mawazo yaliyoandikwa na vijana yameonyesha kuwa yakiboreshwa yanaweza kuwa mpango mzuri ambao unaweza kukabili changamoto mbalimbali ndani ya jamii na Taifa kwa ujumla.

"Mawazo yote yaliyowasilishwa hayataachwa badala yake yataboreshwa na kupatiwa fursa ili yawe mpango ambao utakuwa suluhu kwa baadhi ya changamoto ili kuleta tija na kusaidia Taifa mojawapo likatoa ajira kwa vijana,"alisema Omollo.

Alisema kuwa mawqzo hayo ni bunifu ambazo zimeonyesha jinsi gani vijana walivyokuwa na vipaji ambavyo vitatoa ajira na kuwa na manufaa kwa watu wengi hivyo kulisaidia Taifa.

"Vijana wana fursa nyingi kiuchumi lakini wanakosa taarifa sahihi kwani mawazo kama haya wanaweza kuyapatia fedha za Halmashauri nchini kupitia manunuzi ya umma kwenye mfumo wa Nest au mpango wa yendelezaji vipaji,"alisema Omollo.

Aidha alisema moja ya sekta yenye fursa nyingi ni kilimo ambayo imeajiri asilimia 75 ya Watanzania vijana wanaweza kunufaika kiuchumi kupitia mnyororo wa thamani na fursa kupitia dijitali.

Naye mwenyekiti wa kamati ya Vijana Uchumi Challenge Joseph Malecela alisema kuwa jumla ya mawazo zaidi ya 7,000 ya vijana kote nchini wenye umri kati ya miaka 15 hadi 35 yaliwasilishwa na kuchujwa na kubaki 100 ambayo yatashindanishwa kupata mshindi.

 

Malecela alisema kuwa washiriki hao 100 ambao waliiingia kambini kwenye Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere wamechujwa na majaji wabobezi wa masuala ya uchumi na fedha na kubaki 10 watashindana ili kumpata mshindi wa shindano hilo.


Rais Dk Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye kilele cha kumpata kijana mwenye wazo zuri Julai 6 mwaka huu Jjiini Dar es Salaam  kwenye Ukumbi wa Julius Nyerere Internation Convention Centre (JNICC) Jijuni Dar es Salaam.



mwisho