Wednesday, June 3, 2026

DK SAMIA SULUHU HASSAN KUTUNUKIWA SHAHADA YA UZAMIVU YA CHUO KIKUU CHA RUDIN URUSI

Na Mwandishi Wetu ,TBN, Moscow

Rais Dkt  Samia Suluhu Hassan ambaye yupo hapa shirikisho la Urusi kwa ziara ya kitaifa anatarajiwa kutunukiwa shahada ya uzamivu na Chuo Kikuu cha Rudin nchini hapa.

Tuzo hiyo inatokana na kutambua kazi yake na mchango wake katika jami ya Tanzania na dunia katika masuala ya msingi yanayohusu Maisha ya binadamu.

Chuo cha RUDIN chenye wanafunzi wa kitanzania 570 kufikia mwaka 2025 katika miaka zaidi ya 65 ya RUDIN, watanzania 1,132 wamepitia chuo hicho.

RUDIN kimesomesha zaidi ya wataalamu 200,000 duniani na sasa ina watu 44,000 kutoka nchi 160 duniani.

Chuo hiki ni cha 367 kwa ubora duniani kwa mujibu wa QS World University Ranking ya mwaka 2025.

Rais Dkt Samia ambaye amepokelewa jana na Waziri wa maendeleo ya Uchumi wa Russia Maxim Reshetnikov anatarajiwa kukutana na mwenyeji wake Rais Vladimir Putin na kufanya mazungumzo ya ana kwa ana kwa ajili ya kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kiuchumi.

Aidha akiwa nchini hapa, akiwa kiongozi wa pili wa Tanzania kutembelea Urusi, ziara ya kwanza ikiwa imefanywa na baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere, atashiriki Jukwaa la uchumi la St Petersburg ambapo tanzania itanadi fursa za uwekezaji, na diplomasia ya Uchumi  kwa viongozi, wawekezaji na watunga sera wa kimataifa.

Katika kufanikisha dira ya Maendeleo 2050 ziara hii ni kikolezo cha utekelezaji kwa mafanikio ya dira hiyo ambayo inahitaji raslimali watu wenye utaalamu na upeo mkubwa kusimamia na kuendesha miradi ya kimkakati itakayopelekea ajira, viwanda na biashara zitakazoingiza dola trilioni moja na kuwa katika uchumi wa kati wa juu.

Katika WhatsApp yake Rais Samia amesema Ziara hiyo ni muhimu hasa taifa linapoelekea kuanza utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050 ambayo inataka ushiriki mkubwa wa sekta binafsi.

 "Tutafanya mazungumzo na wenyeji wetu yanayolenga kuimarisha ushirikiano katika sekta za kimkakati zinazogusa maisha ya wananchi." 

"Aidha, tutashiriki majukwaa ya biashara na uwekezaji na kutatangaza fursa zilizopo nchini, pamoja na kufungua zaidi fursa za masoko kwa bidhaa za Tanzania nchini Urusi."

RAIS DK SAMIA SULUHU HASSAN AWASILI URUSI


Na Mwandishi Wetu, TBN, Moscow

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Vnukovo, uliopo Jijini Moscow kwa ajili ya Ziara ya Kitaifa, nchini Urusi

Katika ziara hii ya kihistoria ikifanywa kwa mara ya pili katika historia ya uhusiano wa Tanzania na Urusi, ya kwanza ilikuwa ni miaka ya 1960 iliyofanywa na baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Rais Samia anaendeleza kampeni kubwa ya kuhakikisha Tanzania inanufaika pia kiuchumi na uhusiano mzuri na mataifa mbalimbali

Kwa mujibu wa shughuli atakazofanya Rais Samia akiwa hapa nchini kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa Kidiplomasia, kisiasa, kiuchumi na kihistoria baina ya Tanzania na Urusi,Rais amekuja kuiweka Tanzania katika ramani ya uwekezaji kwa ushiriki wake katika mkutano mkubwa wa uwekezaji jijini St Petersburg na pia kuona namna ya kutengeneza raslimali watu ambayo taifa inahitaji sana katika kufanikisha utekelezaji wa dira ya maendeleo ya 2050. 

Alipowasili nchini hapa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Vnukovo, Jijini Moscow  majira ya saa mbili na dakika 25 usiku , japo jua bado lilikuwa linawaka,  Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alipokea heshima ya wimbo wa Taifa pamoja na gwaride.

Rais Samia alipokewa uwanjani na Waziri wa Maendeleo ya Uchumi wa Shirikisho la Urusi Mhe. Maxim Reshetnikov. 

Kwa mujibu wa ratiba leo asubuhi ataanza na kuweka shada ka maua kwa kaburila askari asiyejulikana kabla ya kwenda Ikuku ya Kremlin kwa mazungumzo na Rais Vladmir Putin.

Sunday, May 31, 2026

WAZIRI KAPINGA AITAKA TBPL KUZALISHA MBOLEA HAI YENYE UBORA

WAZIRI wa Viwanda na Biashara Judith Kapinga ametaka kiwanda cha Tanzania Biotech Production Ltd (TBPL) kuzalisha Mbolea hai kwa kuzingatia ubora.

Kapinga aliyasema hayo Mjini Kibaha wakati wa hafla ya utiaji saini za makubaliano baina ya TPBL kampuni tanzu ya NDC na TFC, TARI, TFRA na TPHPA juu ya ushirikiano wa pamoja.

Alisema kuwa mbolea hiyo inasoko kubwa kwani haina kemikali na pia inatunza mazingira hivyo ni salama kwa afya za binadamu hivyo izingatiwe ubora wake.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Mwendeshaji wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) ambayo ndiyo wasimamizi wa kiwanda hicho Nicolaus Shombe alisema kuwa uzalishaji wa mbolea hiyo utaleta mapinduzi ya kilimo.

Mkurugenzi Mkuu wa TBPL Mhandisi Rafael Moya alisema kuwa mbolea itasaidia wakulima kutumua kemikali kwani kiupaumbele cha Taifa ni kulinda afya za watu.


Wednesday, May 27, 2026

WATAKIWA KUWA NA UTII KAMA WA IBRAHIM

WATANZANIA wametakiwa kufuata maandiko ya vitabu vya dini vinavyoelezea juu ya utii wa Ibrahim ambaye alimuamini Mungu na kumbariki katika maisha yake.

Hayo yalisemwa na Ustaadh Mahamudu Lipambila ambaye ni katibu wa Msikiti wa Masjid Hadharaj Mzimuni Maili Kibaha Mkoani Pwani wakati wa Maadhimisho ya Sikukuu ya Kuchinja (EIDY L ADHUHAA) inayoadhimishwa ulimwenguni kote.

Lipambila alisema kuwa hadhithi ya Ibrahim ambayo ilimtaka amchinjie mwanae ili awe sadaka ambapo ndiyo chimbuko la sikukuu hiyo kubwa kwa imani ya Kiislamu.

"Ibrahim alionyesha utii kwa Mungu kwa kutaka kumtoa mwanae wa pekee ili awe sadaka ya kuchinjwa na alipokubali Mungu kwa kupitia Malaika alimletea kondoo na ndiyo akachinjwa kuwa sadaka,"alisema Lipambila.

Alisema kuwa hadithi hiyo inafundisha jinsi gani watu wanapaswa kuwa na utii juu ya imani zao na kufuata mafundisho ya Mwenyezi Mungu ambayo yatafanya watu waishi kwa kuthaminiana.

"Pia hadithi inafundisha wazazi kuwa na kiasi katika upendo juu ya watoto wao ambapo wengine wamekuwa chanzo cha mmomonyoko wa maadili kwa kutaka kuwafurahisha badala ya kumpenda zaidi Mungu kwa kufuata mafundisho yake,"alisema Lipambila.

Aidha alisema kuwa sikukuu hiyo ni ya furaha kwa kuhakikisha jamii yote inakuwa na furaha kwa kuwa na utii juu ya Mwenyezi Mungu na wanapaswa kumpenda Mungu zaidi.

"Watu waishi kama ilivyokuwa makusudio ya Mungu kutuumba na wakizingatia hayo wataishi kwa amani na upendo na hakutakuwa na tofauti za kimitazamo hasi ya kimaendeleo,"alisema Lipambila.

Aliongeza kuwa viongozi wanapaswa kuwa na hekima na utii kama aliokuwa nao Ibrahim ambaye dini zote zinamuona kama kielelezo cha imani zao kwa Mwenyezi Mungu.

Tuesday, May 26, 2026

WATENDAJI KATA WATAKIWA KUPAMBANA KUONGEZA MAPATO

WATENDAJI wa Kata Mkoani Pwani wametakiwa kumsadia Rais kwenye suala la ukusanyaji wa mapato ili yaweze kuleta maendeleo kwa wananchi ili kufikia Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050.

Hayo yalisemwa Mjini Kibaha na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge wakati wa Kikao kazi cha watendaji wa Kata wa Mkoa huo kilichofanyika Kibaha.

Kunenge alisema kuwa Mkoa kwa sasa unafanya vizuri kwenye suala la ukusanyaji wa mapato hapa nchini kutokana na kuweka mazingira mazuri kwa kwenye maeneo ya vyanzo vya mapato.

"Nyie ni watu muhimu sana na serikali ingependa kuona mnaendana na Dira ya Maendeleo ya Taifa ambayo inataka pato la mtu lifikie dola 7,000 kwa mwaka na la nchi trilioni 1 hadi ifikapo mwaka 2050,"alisema Kunenge.

Alisema wakati anafika kwenye Mkoa huo ulikuwa ni moja ya mikoa iliyokuwa chini kimapato ikiwa ni Mkoa wa 23 lakini kwa sasa umeweza kuinuka kimapato.

"Mnapofanya shughuli zenu mhakikishe mnazingatia Dira ya Maendeleo ya Taifa inaweka mazingira mazuri kwa sekta binafsi ili iendeshe uchumi kuzalisha ajira kuongeza thamani ya mazao na kuuza nje ya nchi,"alisema Kunenge.

Alisema kuwa sekta binafsi ni ya kimageuzi ili kuwe na mabadiliko ambapo asilimia 70 ya maendeleo inatokana na sekta binafsi hivyo lazima kuweka mazingira mazuri hasa ikizingatiwa Mkoa wa Pwani ni moja ya mikoa yenye viwanda vingi.

"Watendaji wa kata ni muhimu kwani ni sehemu muhimu ya maendeleo na mabadiliko hivyo hawapaswi kufanya kazi kwa mazoea kwani dunia inabadilika,"alisema Kunenge.

Aidha alisema kuwa wasiamini kwenye kushindwa bali waamini kwenye kushinda kwani wanatakiwa kuongeza thamani na  hawapaswi kulala kama anavyofanya Rais Dk Samia Suluhu Hassan ambaye halali ili kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo.

Alibainisha kuwa watendaji hao wanapaswa kupunguza kero na rasilimali zinazopatikana zitumike kwa kuzingatia vipaumbele vya eneo husika na waongeze mapato ya ndani ili nchi iweze kujitegemea.

Nao watendaji hao walisema kuwa watahakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa kushirikiana na viongozi wao na wadau ili kufikia malengo hayo yaliyowekwa ili kuleta maendeleo.

Monday, May 25, 2026

PWANI YAONGEZA MAPATO YA MKOA

MKOA wa Pwani umeongeza ukusanyaji wa mapato kutoka asilimia 87.9 Juni kwa mwaka 2025 na kufikia asilimia 106 Machi mwaka 2026.

Hayo yamesemwa Mjini Kibaha na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge wakati wa Kikao kazi cha watendaji wa Kata wa Mkoa huo.

Kunenge amesema kuwa Mkoa unafanya vizuri kwenye suala la ukusanyaji wa mapato hapa nchini kutokana na kuweka mazingira mazuri.

"Nyie ni watu muhimu sana na serikali ingependa kuona mnaendana na Dira ya Maendeleo ya Taifa ambayo inataka pato la mtu lifikie dola 7,000 kwa mwaka na la nchi trilioni 1 hadi ifikapo mwaka 2050,"amesema Kunenge.

Amesema wakati anafika kwenye Mkoa huo ulikuwa ni moja ya mikoa iliyokuwa chini kimapato ikiwa ni Mkoa wa 23 lakini kwa sasa umeweza kuinuka kimapato.

"Mnapofanya shughuli zenu mhakikishe mnazingatia Dira ya Maendeleo ya Taifa inaweka mazingira mazuri kwa sekta binafsi ili iendeshe uchumi kuzalisha ajira kuongeza thamani ya mazao na kuuza nje ya nchi,"amesema Kunenge.

Amesema kuwa sekta binafsi ni ya kimageuzi ili kuwe na mabadiliko ambapo asilimia 70 ya maendeleo inatokana na sekta binafsi hivyo lazima kuweka mazingira mazuri hasa ikizingatiwa Mkoa wa Pwani ni moja ya mikoa yenye viwanda vingi.

"Watendaji wa kata ni muhimu kwani ni sehemu muhimu ya maendeleo na mabadiliko hivyo hawapaswi kufanya kazi kwa mazoea kwani dunia inabadilika,"amesema Kunenge.

Aidha amesema kuwa wasiamini kwenye kushindwa bali waamini kwenye kushinda kwani wanatakiwa kuongeza thamani na  hawapaswi kulala kama anavyofanya Rais Dk Samia Suluhu Hassan ambaye halali ili kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo.

Alibainisha kuwa watendaji hao wanapaswa kupunguza kero na rasilimali zinazopatikana zitumike kwa kuzingatia vipaumbele vya eneo husika na waongeze mapato ya ndani ili nchi iweze kujitegemea.

Sunday, May 24, 2026

MTAA WA MWENDAPOLE B MBIONI KUANZA ULINZI SHIRIKISH KUKABILI UHALIFUI

WANANCHI wa Mtaa wa Mwendapole B Wilayani Kibaha wamekubaliana kuanza kufanya ulinzi shirikishi ili kukabiliana na vitendo vya kihalifu ndani ya Mtaa huo..

Akizungumza na wananchi wakati wa kikao cha Mtaa kilichofanyika kwenye ofisi za Mtaa huo Mwenyekiti wa Mtaa Abubakar Matumla alisema kuwa kabla ya kuanza kamati itakaa ili kuangalia namna ya kufanya ulinzi huo.

Matumla alisema tayari wameshapata kibali cha kuwa na ulinzi shirikishi na kinachofuata ni kupanga namna ya kufanya zoezi hilo na namna wananchi watakavyo changia watu watakaokuwa wakilinda.

"Tunamshukuru Mkuu wa Wilaya tayari katoa kibali cha Mtaa kuwa na ulinzi shirikishi ili kukabiliana na vitendo vya uhalifu ambavyo vimekuwa vikijitokeza nyakati tofauti tofauti,"alisema Matumla.

Alisema kuwa watakaa na kamati ya Mtaa wiki hii ili kupanga utaratibu mzuri wa kuanza zoezi hilo na kiwango cha kila kaya kuchangia ili kuwalipa walinzi hasa ikizingatiwa michongo ya ulinzi shirikishi ni hayari.

Aidha alisema kuwa wenye nyumba nao wsnapaswa kuwa makini kwa kuwa na taarifa za kutosha za wapangaji wao kwani baadhi yao wanaweza kuwa wanajihusisha na uhalifu.

Naye Diwani wa Kata ya Kibaha Omary Bulla alisema kuwa ulinzi shirikishi ni muhimu sana kwani baadhi ya vijana ambao siyo waaminifu wamekuwa wakiiba vitu kwenye nyumba au kukaba watu.

Bulla alisema kuwa ili kufanikiwa wananchi wanapaswa kushiriki kikamilifu kwa kutoa michango ili iwezeshe walinzi waweze kufanya kazi zao bila ya vikwazo na kukabili uhalifu ndani ya Mtaa huo.

Kwa upande wake mmoja wa wananchi wa Mtaa huo Dago Mwombeki alisema kuwa baadhi ya vijana wamekuwa wakiwapora watu wanaokuwa wanakwenda kazini alfajiri au wanapokuwa wanatoka kazini.

Mwombeki alisema kuwa ulinzi shirikishi utasaidia kukabili changamoto hiyo ya uhalifu ndani ya Mtaa kwani wanasababisha watu wasiishi kwa amani na kurudisha nyuma maendeleo ya watu.