Sunday, April 26, 2026
ZINGATIENI DIRA YA MAENDELEO
WIZARA ya Elimu Sayansi na Teknolojia imezitaka Shule za Kimataifa nchini kujisajili kwenye mifumo na miongozo ya elimu na kiserikal ili kukidhi matakwa ya kisheria.Hayo yalisemwa na Dk Maulid Maulid aliyemwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara Caroline Nombo wakati wa kufunga mafunzo ya siku nne kwa wamiliki wa shule hizo juu ya namna ya uendeshaji wa shule hizo mafunzo yaliyofanyika kwenye Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere Kibaha.
Maulid alisema kuwa ili elimu inayotolewa na shule hizo za kimataifa lazima zihakikishe zinafanya usajili wao kupitia mifumo iliyowekwa ili kuendana na mfumo wa elimu wa nchi.
"Wamiliki wa shule hizi wanapaswa kufanya usajili kwenye mifumo ya elimu ili elimu inayotolewa itambulike na iwe na ubora unaotambulika na ushindani kimataifa kwa kuzingatia mitaala ya nchi yetu,"alisema Maulid.
Alisema kuwa shule hizo zinapaswa kujisajili kwenye mamlaka mbalimbali za taasisi za elimu ili ziweze kuendana na mifumo iliyopo ikiwemo kwenye Baraza la Mitihani NACTE na mamlaka za serikali.
"Lazima wafuate mifumo yote ya kiithibati na ubora bila kusahau kuzingatia sera ya elimu ambayo ndiyo inayotoa mwongozo wa elimu kwa taasisi za kielimu,"alisema Maulid.
Aidha alisema kuwa pia mitaala yao iendane na Dira ya Taifa ya Maendeleo ili wanafunzi wawe na uelewa wa juu ya Dira hiyo ambapo kwa sasa ni ya 2050.
"Mitaala yao iendane na Dira ya Maendeleo kwani inazingatia utoaji elimu bora ambayo inaangalia viaumbele vya nchi katika kuleta maendeleo kwa wananchi,,'alisema Maulid.
Kwa upande wake moja ya washiriki wa mafunzo hayo ambaye ni mhasibu wa shule ya kimataifa ya Renie Joshua John alisema kuwa mafunzo hayo yatakuwa chachu kwa shule yake kwani amepata elimu ya namna ya kuweka vizuri masuala ya fedha.
John alisema kuwa wamepata uelewa mzuri wa namna ya kuendesha shule zao na kwa kuzingatia taratibu na miongozo ya kisheria ambayo wanapaswa kuifuata.
Mafunzo hayo yaliandaliwa na Tanzania School Leadership Institute (TSLI) na kusimamiwa na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia waliwahusisha wamiliki, walimu wakuu, wahasibu na viongozi wa shule za kimataifa hapa nchini
SHULE ZA KIMATAIFA ZATAKIWA KUJISAJILI KIKIDHI MATAKWA YA KISHERIA
WIZARA ya Elimu Sayansi na Teknolojia imezitaka Shule za Kimataifa nchini kujisajili kwenye mifumo na miongozo ya elimu na kiserikal ili kukidhi matakwa ya kisheria.
Hayo yalisemwa na Dk Maulid Maulid aliyemwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara Caroline Nombo wakati wa kufunga mafunzo ya siku nne kwa wamiliki wa shule hizo juu ya namna ya uendeshaji wa shule hizo mafunzo yaliyofanyika kwenye Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere Kibaha.
Maulid alisema kuwa ili elimu inayotolewa na shule hizo za kimataifa lazima zihakikishe zinafanya usajili wao kupitia mifumo iliyowekwa ili kuendana na mfumo wa elimu wa nchi.
"Wamiliki wa shule hizi wanapaswa kufanya usajili kwenye mifumo ya elimu ili elimu inayotolewa itambulike na iwe na ubora unaotambulika na ushindani kimataifa kwa kuzingatia mitaala ya nchi yetu,"alisema Maulid.
Alisema kuwa shule hizo zinapaswa kujisajili kwenye mamlaka mbalimbali za taasisi za elimu ili ziweze kuendana na mifumo iliyopo ikiwemo kwenye Baraza la Mitihani NACTE na mamlaka za serikali.
"Lazima wafuate mifumo yote ya kiithibati na ubora bila kusahau kuzingatia sera ya elimu ambayo ndiyo inayotoa mwongozo wa elimu kwa taasisi za kielimu,"alisema Maulid.
Aidha alisema kuwa pia mitaala yao iendane na Dira ya Taifa ya Maendeleo ili wanafunzi wawe na uelewa wa juu ya Dira hiyo ambapo kwa sasa ni ya 2050.
"Mitaala yao iendane na Dira ya Maendeleo kwani inazingatia utoaji elimu bora ambayo inaangalia viaumbele vya nchi katika kuleta maendeleo kwa wananchi,,'alisema Maulid.
Kwa upande wake moja ya washiriki wa mafunzo hayo ambaye ni mhasibu wa shule ya kimataifa ya Renie Joshua John alisema kuwa mafunzo hayo yatakuwa chachu kwa shule yake kwani amepata elimu ya namna ya kuweka vizuri masuala ya fedha.
John alisema kuwa wamepata uelewa mzuri wa namna ya kuendesha shule zao na kwa kuzingatia taratibu na miongozo ya kisheria ambayo wanapaswa kuifuata.
Mafunzo hayo yaliandaliwa na Tanzania School Leadership Institute (TSLI) na kusimamiwa na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia waliwahusisha wamiliki, walimu wakuu, wahasibu na viongozi wa shule za kimataifa hapa nchini
Thursday, April 23, 2026
MITAALA YA SHULE ZA KIMATAIFA YAVUTIA WANAFUNZI KUTOKIMBILIA KUSOMA NJE YA NCHI
KWA kipindi cha miaka ya nyuma baadhi ya wazazi walikuwa na kasumba ya kupeleka watoto wao kusoma nje ya nchi kwa imani huko ndiko kuna elimu bora tofauti na hapa nchini.
Aidha baada ya maboresho mbalimbali kwenye shule za kimataifa hapa nchini kwa sasa wazazi wanawapeleka watoto wao kwenye shule za hapa nchini ambazo zinatoa elimu bora.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Elimu ya Ualimu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Mathias Mvula akimwakilisha Naibu Waziri wa Elimu Wanu Ameir wakati akifungua mafunzo ya wadau wa Shule za Kimataifa nchini kwenye Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Kibaha.
Mvula amesema kuwa Shule hizo zinafundisha kwa kuzingatia mitaala ya nchi na ile ya kimataifa ili elimu inayotolewa kuwa na ushindani na ile inayotolewa nje.
Naye Hassan Masawe kutoka Tanzania School Leadership Institute (TSLI) amesema kuwa mafunzo hayo yana lengo la kuboresha elimu inayotolewa na shule hizo kuwa na ubora baina ya elimu ya nchini na ile ya nje ya nchi.
Kwa upande wake Calista Mungwe Mkurugenzi wa shule ya Renie International ya Jijini Dar es Salaam amesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kuboresha uendeshaji wa Shule zao.
Wednesday, April 22, 2026
VIJANA WASEMA BENKI YA VIJANA ITAKUZA MITAJI YAO YA BIASHARA
MPANGO wa kuanzisha benki ya vijana ni jambo zuri kwani watanufaika na kuweza kukuza mitaji na biashara zao hivyo wataweza kujiajiri na kuajiriwa kwa wingi.
Hayo yamesemwa Mjini Kibaha na Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Kata ya Tangini Lazaro Benjamin Wilayani Kibaha Mkoani Pwani akizungumzia kuhusu bajeti ya vijana iliyowasilishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana Dk Joel Nanauka Jijini Dodoma.
Benjamin amesema kuwa benki hiyo itatoa mikopo rahisi na yenye masharti nafuu ikiambatana na riba ndogo pamoja na dhamana rahisi.
"Benki hiyo itaenda kuondoa changamoto za mitaji kwa vijana na itasaidia kuongeza nafasi ya kufadhiliwa,"amesema Benjamin.
Aidha amesema kuwa benki hiyo itasaidia kuwapatia vijana elimu ya biashara na uwekezaji na matumizi sahihi ya fedha.
"Itapunguza vijana kutokuwa na ajira kwani watajiajiri kupitia mikopo ambayo itawapatia mitaji na kupata elimu ya matumizi ya fedha,"amesema Benjamin.
Saturday, April 18, 2026
MWENGE KUPITIA MIRADI YA MAENDELEO 68 YENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 263.1
MWENGE wa Uhuru umeanza mbio zake Mkoani Pwani ambapo utapitia miradi ya Maendeleo 68 yenye thamani ya shilingi bilion 263.1 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge aliyasema hayo Mapinga Wilayani Bagamoyo wakati akiupokea Mwenge huo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila.
Kunenge alisema kuwa kati ya hiyo miradi 23 itawekewa mawe ya Msingi miradi 21
itazinduliwa na miradi 24 itakaguliwa.
"Miradi hiyo imechangiwa na Serikali Kuu bilioni 16.2 Halmashauri za Wilaya zimechangia kiasi cha shilingi bilioni 1.62,"alisema Kunenge.
Alisema kuwa wananchi na wawekezaji wamechangia kiasi cha shilingi bilioni 180.7 wadau wa Maendeleo bilioni 64.3 na michango ya Mwenge milioni 38.8.
"Ujumbe Mkuu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2026 unalenga katika ujenzi wa Amani Umoja na Mshikamano wa Kitaifa chini ya Tanzania ni yetu sote tushikamane pamoja kuleta maendeleo,"alisema Kunenge.
Alisema kuwa kauli mbiu hiyo inalenga kujenga na kuimarisha Umoja wa Kitaifa na kuutumia Mwenge wa Uhuru kuwaenzi na kuwatia moyo wazalendo wa kweli na makundi mbalimbali.
"Makundi haya yana mchango mkubwa katika kulinda Amani, Umoja na Mshikamano wa Kitaifa katika kuijenga Tanzania imara kimaadili, kidiplomasia na kiuchumi ndani na nje ya mipaka,"alisema Kunenge.
Aidha alisema Mkoa unachukua hatua kupitia ujumbe wa kudumu katika mapambano dhidi ya Vvu/Ukimwi, dawa za kulevya, malaria, rushwa na changamoto za lishe.
Naye kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Wazo Mwangonda alisema kuwa taarifa zinazoonyesha namna wanawake na makundi maalumu namna gani wanavyonufaika na zabuni.
Mwangonda kuwa Mwenge ni wawananchi yapangwe maeneo ambayo wananchi wataukimbiza.
Saturday, April 4, 2026
MKIMBIZA MWENGE KITAIFA AIPONGEZA STAMICO KWA KUIBEBA AGENDA YA KITAIFA YA NISHATI SAFI
*STAMICO YASHIRIKI UZINDUZI WA MWENGE WA UHURU KITAIFA PEMBA.*
▪️Mkimbiza Mwenge Kitaifa aipongeza STAMICO kwa kuibeba ajenda ya kitaifa ya Nishati Safi.
▪️Atoa msisitizo kwa Taasisi na Shule Mkoani Kusini Pemba kutumia Nishati ya Rafiki Briquettes
▪️Nishati Safi ya Rafiki Briquettes kuanza kuuzwa Kisiwani Pemba
▪️Dkt. Mwasse: STAMICO kuwawezesha kontena wanawake na Samia Mkoa wa Kusini Pemba
Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limeshiriki katika uzinduzi wa Mbio za Mwenge ambazo umefanyika katika viwanja vya Gombani Kisiwani Pemba.
Mgeni Rasmi katika Uzinduzi huo alikuwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Tukio hilo pia lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
STAMICO imewakilishwa na Dkt Venance Mwasse, Mkurugenzi Mtendaji ambaye aliambatana na baadhi ya maafisa kutoka kitengo cha Masoko na Mahusiano.
Katika mbio za mwaka huu za Mwenge wa Uhuru, kauli mbiu ni: “Tanzania ni Yetu Sote, Tushikamane kwa Maendeleo.” Kauli mbiu hiyo inalenga kuhamasisha umoja, ushirikiano na mshikamano wa Watanzania katika kuchangia maendeleo ya Taifa. Mbio hizi zinatarajiwa kuendelea katika mikoa mbalimbali ya nchi, Tanzania Bara na Visiwani.
Sambamba na uzinduzi huo, pia kumefanyika maonesho ya Taasisi mbalimbali za Serikali na sekta binafsi yaliyolenga kutoa elimu na kuonesha huduma mbalimbali kwa wananchi.
Katika maonesho hayo, Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) nalo limeshiriki kwa kuonesha bidhaa na huduma zake kwa Wananchi.
Awali, Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake na Samia Mkoani Kusini Pemba Bi Sabra Masoud Ally alimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO kwa ulezi na ushirikiano unaotolewa na STAMICO katika kuwawezesha kushiriki katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na usambazaji wa nishati safi ya Rafiki briquettes.
Akizungumza katika kikao hicho, Dkt. Mwasse aliahidi kuendelea kusaidia kikundi hicho kwa kuwapatia kontena mwezi huu wa nne, ili yaweze kutumika kama vituo vya kuuzia nishati safi ya kupikia ya Rafiki Briquettes. Aidha, alisisitiza kuwa STAMICO itaendelea kufanya uhamasishaji mkubwa wa matumizi ya nishati hii safi katika mikoa ya Kaskazini na Kusini Pemba, kwa lengo la kulinda mazingira na kupunguza matumizi ya kuni na mkaa wa kawaida.
Akitembelea banda la STAMICO,Mkimbiza Mwenge kitaifa,Ndugu Wazo Mwangonda aliipongeza STAMICO kwa kubeba kikamilifu ajenda ya Kitaifa ya nishati safi na Kusisitiza taasisi na Shule za Mkoa wa Kusini Pemba kutumia Nishati ya Rafiki Briquettes.
STAMICO inaendelea na azma yake ya kuwa kinara katika kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi kwa kutekeleza kwa vitendo ajenda muhimu za Serikali.
Subscribe to:
Posts (Atom)




