Thursday, April 23, 2026

MITAALA YA SHULE ZA KIMATAIFA YAVUTIA WANAFUNZI KUTOKIMBILIA KUSOMA NJE YA NCHI


KWA kipindi cha miaka ya nyuma baadhi ya wazazi walikuwa na kasumba ya kupeleka watoto wao kusoma nje ya nchi kwa imani huko ndiko kuna elimu bora tofauti na hapa nchini.

Aidha baada ya maboresho mbalimbali kwenye shule za kimataifa hapa nchini kwa sasa wazazi wanawapeleka watoto wao kwenye shule za hapa nchini ambazo zinatoa elimu bora.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Elimu ya Ualimu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Mathias Mvula akimwakilisha Naibu Waziri wa Elimu Wanu Ameir wakati akifungua mafunzo ya wadau wa Shule za Kimataifa nchini kwenye Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Kibaha.

Mvula amesema kuwa Shule hizo zinafundisha kwa kuzingatia mitaala ya nchi na ile ya kimataifa ili elimu inayotolewa kuwa na ushindani na ile inayotolewa nje.

Naye Hassan Masawe kutoka Tanzania School Leadership Institute (TSLI) amesema kuwa mafunzo hayo yana lengo la kuboresha elimu inayotolewa na shule hizo kuwa na ubora baina ya elimu ya nchini na ile ya nje ya nchi.

Kwa upande wake Calista Mungwe Mkurugenzi wa shule ya Renie International ya Jijini Dar es Salaam amesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kuboresha uendeshaji wa Shule zao.


No comments:

Post a Comment