Wednesday, April 22, 2026

VIJANA WASEMA BENKI YA VIJANA ITAKUZA MITAJI YAO YA BIASHARA


MPANGO wa kuanzisha benki ya vijana ni jambo zuri kwani watanufaika na kuweza kukuza mitaji na biashara zao hivyo wataweza kujiajiri na kuajiriwa kwa wingi.

Hayo yamesemwa Mjini Kibaha na Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Kata ya Tangini Lazaro Benjamin Wilayani Kibaha Mkoani Pwani akizungumzia kuhusu bajeti ya vijana iliyowasilishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana Dk Joel Nanauka Jijini Dodoma.

Benjamin amesema kuwa benki hiyo itatoa mikopo rahisi na yenye masharti nafuu ikiambatana na riba ndogo pamoja na dhamana rahisi.

"Benki hiyo itaenda kuondoa changamoto za mitaji kwa vijana na itasaidia kuongeza nafasi ya kufadhiliwa,"amesema Benjamin.

Aidha amesema kuwa benki hiyo itasaidia kuwapatia vijana elimu ya biashara na uwekezaji na matumizi sahihi ya fedha.

"Itapunguza vijana kutokuwa na ajira kwani watajiajiri kupitia mikopo ambayo itawapatia mitaji na kupata elimu ya matumizi ya fedha,"amesema Benjamin.

No comments:

Post a Comment