MWENGE wa Uhuru umeanza mbio zake Mkoani Pwani ambapo utapitia miradi ya Maendeleo 68 yenye thamani ya shilingi bilion 263.1 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge aliyasema hayo Mapinga Wilayani Bagamoyo wakati akiupokea Mwenge huo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila.
Kunenge alisema kuwa kati ya hiyo miradi 23 itawekewa mawe ya Msingi miradi 21
itazinduliwa na miradi 24 itakaguliwa.
"Miradi hiyo imechangiwa na Serikali Kuu bilioni 16.2 Halmashauri za Wilaya zimechangia kiasi cha shilingi bilioni 1.62,"alisema Kunenge.
Alisema kuwa wananchi na wawekezaji wamechangia kiasi cha shilingi bilioni 180.7 wadau wa Maendeleo bilioni 64.3 na michango ya Mwenge milioni 38.8.
"Ujumbe Mkuu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2026 unalenga katika ujenzi wa Amani Umoja na Mshikamano wa Kitaifa chini ya Tanzania ni yetu sote tushikamane pamoja kuleta maendeleo,"alisema Kunenge.
Alisema kuwa kauli mbiu hiyo inalenga kujenga na kuimarisha Umoja wa Kitaifa na kuutumia Mwenge wa Uhuru kuwaenzi na kuwatia moyo wazalendo wa kweli na makundi mbalimbali.
"Makundi haya yana mchango mkubwa katika kulinda Amani, Umoja na Mshikamano wa Kitaifa katika kuijenga Tanzania imara kimaadili, kidiplomasia na kiuchumi ndani na nje ya mipaka,"alisema Kunenge.
Aidha alisema Mkoa unachukua hatua kupitia ujumbe wa kudumu katika mapambano dhidi ya Vvu/Ukimwi, dawa za kulevya, malaria, rushwa na changamoto za lishe.
Naye kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Wazo Mwangonda alisema kuwa taarifa zinazoonyesha namna wanawake na makundi maalumu namna gani wanavyonufaika na zabuni.
Mwangonda kuwa Mwenge ni wawananchi yapangwe maeneo ambayo wananchi wataukimbiza.
No comments:
Post a Comment