Monday, February 16, 2026

GOOD NEWS FOR TANZANIA DIGITAL CONTENT CREATORS AS NEW LICENCE FEES ANNOUNCED

The Government has announced a historic measure that could significantly transform the landscape of Tanzania’s digital content industry.

Speaking at the Annual Broadcasting Service Providers Conference (ABC 2026) in Dodoma, the Deputy Minister for Information, Culture, Arts and Sports, Hamisi Mwinjuma, revealed that the licence fee for online content creators has been reduced from TSh 500,000 to just TSh 50,000, with an application fee of only TSh 10,000.

This represents a reduction of more than 90 per cent — a move widely interpreted as opening a new door for young innovators, bloggers, and digital creators who had previously struggled with the high cost of compliance.

The decision follows nearly a year of strategic consultations between the Tanzania Bloggers Network (TBN) and the Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA), aimed at addressing financial barriers that had constrained the growth of digital journalism and online content production in the country.

In addition, licence fees for Online Content Aggregators have been reduced from TSh 1,000,000 to TSh 100,000.

A new “Amateur” category has also been introduced specifically for emerging young creators, enabling them to formalise their activities and nurture their talents without heavy financial burdens.

Within the broader context of a rapidly expanding digital economy, this decision is expected to stimulate employment, creativity, and tax revenue generation — in line with the development vision championed by President Samia Suluhu Hassan.

If effectively implemented, these reforms may well mark the beginning of a new chapter for Tanzania’s digital creative sector.

NEEMA KWA WATENGENEZA MAUDHUI YA KIDIJITALI ADA MPYA ZA LESENI ZIKITANGAZWA

 

Serikali imetangaza hatua ya kihistoria inayoweza kubadili sura ya tasnia ya maudhui ya kidijitali nchini. Kupitia tamko lililotolewa katika Mkutano wa Mwaka wa Watoa Huduma za Utangazaji (ABC 2026) jijini Dodoma, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma, amesema ada ya leseni kwa watoa maudhui mtandaoni imeshushwa kutoka Sh500,000 hadi Sh50,000, huku ada ya maombi ikiwa Sh10,000 pekee.

Ni punguzo la zaidi ya asilimia 90, hatua ambayo wengi wameitafsiri kama mlango mpya kwa vijana wabunifu, wanablogu na watengeneza maudhui waliokuwa wakikwama kwa gharama.

Hatua hiyo imekuja baada ya mazungumzo ya karibu mwaka mzima kati ya Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), yakilenga kuondoa vikwazo vilivyokuwa vikizuia ukuaji wa sekta hii.

Zaidi ya hayo, ada ya wakusanyaji wa maudhui (Online Content Aggregators) imeshuka kutoka Sh1,000,000 hadi Sh100,000. 

Aidha, kundi jipya la “Amateur” limeanzishwa mahsusi kwa vijana wanaochipukia, likiwawezesha kujisajili rasmi bila mzigo wa kifedha.

Kwa muktadha wa uchumi wa kidijitali unaokua kwa kasi, uamuzi huu unaweza kuwa kichocheo kikubwa cha ajira, ubunifu na mapato ya kodi kwa taifa, kama yalivyo maono ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Saturday, February 14, 2026

NEEMA YA KIDIJITALI: Serikali Yashusha Ada kwa Wanablogu, TCRA Yazindua Redio ya Kisasa 'DSB'

 

SERIKALI imetangaza neema ya kihistoria kwa wanablogu, vijana wabunifu, na watoa maudhui mtandaoni nchini kwa kupunguza ada za leseni kwa kiwango kikubwa, hatua inayolenga kuchochea ukuaji wa uchumi wa kidijitali na kurasimisha shughuli za wahabarishaji wa mitandao.

Hatua hiyo imekuja kufuatia utafiti wa kina na mikutano ya kimkakati ya takribani mwaka mzima kati ya mtandao wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), ikielezea vikwazo vya gharama vilivyokuwa vikikwaza uandishi wa habari za kidijitali nchini.

Akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Watoa Huduma za Utangazaji (ABC 2026) jijini Dodoma leo, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamisi Mwinjuma, amesema ada ya leseni kwa watoa maudhui mtandaoni imeshushwa kutoka Sh500,000 hadi Sh50,000 tu, huku ada ya maombi ikiwa ni Sh10,000 pekee.

Mageuzi hayo pia yamegusa kundi la wakusanyaji wa maudhui (Online Content Aggregators), ambao ada yao imeshushwa kutoka Sh1,000,000 hadi Sh100,000 pekee. Aidha, kundi la "Amateteur" limeanzishwa kwa ajili ya vijana wanaochipukia ili waweze kujitambulisha rasmi na kukuza vipaji vyao bila vikwazo vya kifedha.

Mapinduzi ya Teknolojia ya DSB

Wakati neema hiyo ikitangazwa, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dkt. Jabiri Bakari, ametangaza kuanza kwa teknolojia mpya ya utangazaji wa redio ya kidijitali nchini inayojulikana kama Digital Sound Broadcasting (DSB).

Teknolojia hiyo itaanza kufanya kazi katika mikoa mitano ya majaribio ya Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Arusha, na Mbeya, lengo likiwa ni kuongeza ubora wa sauti na huduma za utangazaji nchini.

"Tumekamilisha maandalizi yote ya kiudhibiti na watoa huduma wa miundombinu wameshapatikana. Hii ni hatua kubwa ya kuendana na mabadiliko ya teknolojia duniani na kuimarisha utangazaji, hususan maeneo ya vijijini," alisema Dkt. Bakari.

Utafiti: Redio Bado ni Kinara

Katika mkutano huo, Injinia Andrew Kisaka wa TCRA amewasilisha matokeo ya utafiti wa hali ya utangazaji kwa mwaka 2025/2026, ukionyesha kuwa redio inaendelea kuwa chanzo kikuu cha habari kwa asilimia 85 ya Watanzania. Hata hivyo, utafiti huo umebaini ukuaji mkubwa wa matumizi ya intaneti miongoni mwa vijana, ambapo asilimia 45 hupata habari kupitia mitandao ya kijamii kabla ya kusikiliza redio au kutazama televisheni.

Upande wa televisheni, utafiti unaonyesha asilimia 65 ya watazamaji wanatumia ving'amuzi, huku maudhui ya ndani yakipendwa zaidi kwa asilimia 70. Serikali imewahimiza watoa huduma za kienyeji kuwekeza zaidi kwenye majukwaa ya kidijitali (OTT) ili kukidhi mahitaji ya soko la sasa.

Ulinzi wa Hakimiliki na Mikopo

Ili kuhakikisha wanahabari wa kidijitali wanufaika na kazi zao, Serikali imezielekeza taasisi za COSOTA na TCRA kuandaa mpango wa kulinda hakimiliki na kudhibiti uharamia mtandaoni. Aidha, Serikali imeanza kutoa mikopo ya masharti nafuu kwa watengeneza maudhui kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kisasa vya kufanyia kazi.

Hadi kufikia Desemba 2025, TCRA imetoa jumla ya leseni 707 za utangazaji, zikiwemo 318 za maudhui mtandaoni, jambo linaloashiria kukua kwa uhuru wa habari na demokrasia nchini chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Monday, February 9, 2026

RAIS DK SAMIA SULUHU HASSAN APELEKA TABASAMU SIKONGE

Na Allan Kitwe, Sikonge

RAIS wa Awamu ya Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amepeleka tabasamu kwa wakazi wa Wilaya ya Sikonge Mkoani Tabora baada ya maji safi na salama kutoka Ziwa Viktoria kufika Wilayani humo.

Shangwe na furaha za wananchi zimelipuka kwenye hafla ya kufungulia maji hayo iliyofanyika juzi katika Kata ya Misheni Mjini Sikonge kwenye eneo lilipojengwa tanki kubwa la kupokelea maji hayo ili yaanze kusambazwa kwa wananchi.

Akizungumza na mamia ya wananchi, wadau wa maendeleo na viongozi mbalimbali wa chama na serikali kwenye hafla hiyo, Waziri wa Maji Mheshimiwa Jumaa Aweso ameeleza kufurahishwa na kazi nzuri ya utekelezaji mradi huo.

Amesema kuwa mradi huo ambao unatekelezwa na Mkandarasi kutoka China kwa gharama ya shilingi bilioni 143 umelenga kufikisha huduma ya maji safi na salama katika Wilaya tatu za Urambo, Kaliua na Sikonge yenyewe.

‘Ndugu zangu wana Sikonge, Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameleta tabasamu kwenu, alipoingia madarakani, aliahidi kumaliza kero yenu ya maji ili akinamama wasitembee na ndoo kichwani umbali mrefu na leo hii maji yamefika’, amesema.

‘Kazi iliyobakia sasa ni kuyasambaza kwa wananchi, katika hili Wataalamu ongezeni kasi, na kila wananchi atakayetaka kuunganishiwa maji nyumbani kwake hakikisheni ndani ya siku 7 awe amepata maji, si vinginevyo’, ameonya.

Aidha Waziri Aweso amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Mwajuma Waziri kuleta timu ya Wataalamu katika Wilaya hiyo ili kushughulikia mradi wa Bwawa la Utyatya ili uanze kufanya kazi ili kusaidiana na mradi huo.

Ameongeza kuwa kila Mtendaji wa Wizara hiyo anapaswa kuwa mwadilifu na mchapa kazi, Mtendaji mbabaishaji hana nafasi, hivi karibuni tutafanya tathmini ya Utendaji wa kila mmoja na kuchukua hatua kwa wanaozembea.

Amempongeza Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Tabora  (TUWASA) Mhandisi Mayunga Kashilimu, RUWASA Mhandisi Hatari Kapufi, Mkuu wa Wilaya Thomas Myinga na Mbunge Amos Maganga kwa kusimamia vizuri utekelezaji mradi huo.       

                                                                                                                                                              

MAFUNZO YA ITIFAKI KWA TAASISI YA SMAUJATA



Wapatiwa mafunzo ya Protocol and Etiquette (Ustarabu na Itifaki za Viongozi) Maadili na Uzalendo kwa watumishi. 

Katika kuhakikisha  taasisi  zinajengewa uwezo wa kiimadili katika kazi 

Mtaalamu wa Kidiplomasia, Uongozi na maadili Ndugu Omary Abdull Punzi amewelekeza  na kuwakumbusha taasisi ya SMAUJATA  katika mafunzo yaliyoandaliwa na taasisi hiyo kufanyika  Februari 7 hadi 8 mwaka 2026  katika Ukumbi wa Chuo Cha VETA Keko Dar es Salaam.


Mafunzo hayo yaliyofunguliwa na Ndugu Salehe Omary Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA  akimwakilisha mkuu wa chuo hiko na kufungwa na Ndugu Fredrick Nelson Rwegasira - Makamu Mwenyekiti   SMAUJATA.

Aidha katika mafunzo hayo yalijikita katika 
Itifaki na Ustarabu wa Viongozi sambamba na maadili

Wednesday, February 4, 2026

JUMUIYA YA WAZAZI PWANI YAADHIMISHA MIAKA 49 YA CCM KWENYE KATA YA TANGINI

JUMUIYA ya Wazazi Mkoa wa Pwani imeadhimisha miaka 49 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa  kupanda miti kwenye eneo la Shule mpya ya Msingi Tangini.

Aidha Jumuiya hiyo pia ilikabidhi vifaa kwa wagonjwa kwenye Zahanati mpya ya Tangini pamoja na kutoa fedha kiasi cha shilingi 180,000 kwa familia mbili zenye watu wenye ulemavu.

Akizungumza wakati wa kupokea ugeni kutoka Jumuiya hiyo ambapo sherehe hizo zimefanyika kimkoa kwenye Kata ya Tangini Mwenyekiti wa CCM na Diwani wa Kata ya Tangini Antony Mlao amesema kuwa anashukuru kwa kupewa heshima hiyo.

Milao amesema kuwa anaishukuru serikali kwa kuwapatia miradi hiyo ambayo ni muhimu ndani ya jamii kwani imewapunguzia wanafunzi na wananchi kwenda kupata huduma mbali.

"Tunamshukuru Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia miradi hii na tunaahidi kuitunza ili iendelee kuhudumia wananchi na wanafunzi kwenye Kata yetu na Halmashauri ya Manispaa nzima ya Kibaha,"amesema Milao.

Mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo kimkoa Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Pwani Yusufu Masombola amesema kuwa lengo ni kuwaweka wananchi wote karibu na chama kwa kutembelea sekta mbalimbali.

Masombola amesema kuwa viongozi waweke taratibu za kusikiliza kero za wananchi ili kujenga imani kwao na kila mmoja afanye kazi kulingana na eneo lake.

Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Kibaha Mjini Yahaya Mtonda amesema kuwa viongozi kwa kushirikiana na wananchi wanapaswa kuendelea kuleta maendeleo ili kumuunga mkono Rais Dk Samia Suluhu Hassan.

Mtonda amesema kuwa viongozi na waccm wanapaswa kuendelea na shughuli za chama kama ilivyokuwa zamani kwani huu ni wakati wa kufanya kazi za chama kujiandaa na chaguzi za jumuiya za chama mwaka 2027.

Kwa upande wake Juma Nziajose mratibu wa chakula na lishe kutoka ofisi ya Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha alishukuru kwa msaada uliotolewa na jumuiya hiyo.

Nziajose alisema kuwa vifaa hivyo vitafikishwa kwa walengwa kama ilivyodhamiriwa na jumuiya licha ya kuwa Zahanati hiyo bado haijaanza kufanya kazi lakini watapeleka kwenye Hospitali mbalimbali za Manispaa.

MAADHIMISHO MIAKA 49 YA CCM YAFANYIKA WAZAZI KIMKOA KATA YA TANGINI

JUMUIYA ya Wazazi Wilaya ya Kibaha Mjini imeadhimisha miaka 49 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa  kupanda miti kwenye eneo la Shule mpya ya Msingi Tangini.

Aidha Jumuiya hiyo pia ilikabidhi vifaa kwa wagonjwa kwenye Zahanati mpya ya Tangini pamoja na kutoa fedha kiasi cha shilingi 180,000 kwa familia mbili zenye watu wenye ulemavu.

Akizungumza wakati wa kupokea ugeni kutoka Jumuiya hiyo ambapo sherehe hizo zimefanyika kimkoa kwenye Kata ya Tangini Mwenyekiti wa CCM na Diwani wa Kata ya Tangini Antony Mlao amesema kuwa anashukuru kwa kupewa heshima hiyo.

Milao amesema kuwa anaishukuru serikali kwa kuwapatia miradi hiyo ambayo ni muhimu ndani ya jamii kwani imewapunguzia wanafunzi na wananchi kwenda kupata huduma mbali.

"Tunamshukuru Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia miradi hii na tunaahidi kuitunza ili iendelee kuhudumia wananchi na wanafunzi kwenye Kata yetu na Halmashauri ya Manispaa nzima ya Kibaha,"amesema Milao.

Mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo kimkoa Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Pwani Yusufu Masombola amesema kuwa lengo ni kuwaweka wananchi wote karibu na chama kwa kutembelea sekta mbalimbali.

Masombola amesema kuwa viongozi waweke taratibu za kusikiliza kero za wananchi ili kujenga imani kwao na kila mmoja afanye kazi kulingana na eneo lake.

Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Kibaha Mjini Yahaya Mtonda amesema kuwa viongozi kwa kushirikiana na wananchi wanapaswa kuendelea kuleta maendeleo ili kumuunga mkono Rais Dk Samia Suluhu Hassan.

Mtonda amesema kuwa viongozi na waccm wanapaswa kuendelea na shughuli za chama kama ilivyokuwa zamani kwani huu ni wakati wa kufanya kazi za chama kujiandaa na chaguzi za jumuiya za chama mwaka 2027.

Kwa upande wake Juma Nziajose mratibu wa chakula na lishe kutoka ofisi ya Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha alishukuru kwa msaada uliotolewa na jumuiya hiyo.

Nziajose alisema kuwa vifaa hivyo vitafikishwa kwa walengwa kama ilivyodhamiriwa na jumuiya licha ya kuwa Zahanati hiyo bado haijaanza kufanya kazi lakini watapeleka kwenye Hospitali mbalimbali za Manispaa.