VIONGOZI wanaowania nafasi za uongozi wametakiwa kuacha kuwa na imani kuwa viungo vya watu wenye Ualbino vinasaidia kupata uongozi.
Tuesday, July 16, 2024
WATAKIWA KUACHA IMANI ZA KISHIRIKINA KUPATA UONGOZI
VIONGOZI wanaowania nafasi za uongozi wametakiwa kuacha kuwa na imani kuwa viungo vya watu wenye Ualbino vinasaidia kupata uongozi.
VIONGOZI WA DINI WAHAMASISHA WANAWAKE KUSHIRIKI CHAGUZI NA KUJIINUA KIUCHUMI
VIONGOZI wa Dini Halmashauri ya Mji Kibaha wamekuja na mkakati wa kuhamasisha ushiriki wanawake na wasichana katika uongozi na haki za kiuchumi.
Aidha wametakiwa kuwania nafasi za uongozi kwani nao wanauwezo wa kuwa viongozi na haki yao washiriki ili walete maendeleo ndani ya jamii na nchi kwa ujumla.
Hayo yamesemwa Mjini Kibaha na Mchungaji James Machage wa Kanisa la Sabato Visiga wakati wa mafunzo ya Ushiriki wa wanawake na Wasichana katika Uongozi na Haki za Kiuchumi kwa Viongozi wa Dini yaliyofadhiliwa na UN WOMEN.
Mchungaji Machage amesema kuwa licha ya changamoto kubwa ya mila na baadhi ya imani lakini wataendelea kutoa elimu ya ushiriki kwenye uchaguzi na fursa za kiuchumi kwani wanauwezo wa kuwa viongozi.
Amesema kuwa watahakikisha wanasaidia wanawake ili waweze kupata haki zao na kuwatia moyo ili wajue fursa zilizopo kwani uongozi wa nchi unajali wanawake kwa kuwapatia fursa mbalimbali zikiwemo za mikopo kupitia vikundi.
Naye Julieth Faustine katibu wa Kanisa la Katoliki Pangani amesema kuwa mafunzo hayo yamemsaidia kujua masuala ya uwiano kila linalofanyika lizingatie haki kwa wote na utendaji wa kazi bila ya kubagua kuwa baadhi ya kazi ni za wanawake na wanaume.
Faustine amesema kuwa kuna baadhi ya mila zinamkandamiza mwanamke ikiwa ni pamoja na ukeketaji kwa watoto wa kike, kunyimwa elimu, kunyimwa urithi wa ardhi na kutothaminiwa jambo ambalo atalipigia kelele ili jamii iachane na mila hizo.
Kwa upande wake Abdala Ngulengule amesema kuwa mafunzo hayo yamewaongezea chachu ya kwenda kuwahamasisha wanawake kushiriki kwenye fursa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mweishoni mwa mwaka huu.
Ngulengule amesema kuwa mfano kwenye Kata ya Pangani kuna mitaa nane lakini yote ilikuwa ikiongozwa na wanaume hivyo wanatarajia kuwa na mabadiliko makubwa kwenye uchaguzi huo kwani wanawake wengi wamehamasika kushiriki uchaguzi huo ili wapatikaneviongozi wanawake angalau wawili au watatu.
Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Mji Kibaha Leah Lwanji amesema kuwa wanaendelea kuwahamasisha wanawake kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ili waweze kuingia kwenye vyombo vya maamuzi na kuwa na usawa katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo ili waweze kujiinua kiuchumi na kupata fursa zilizopo ndani ya jamii.
Lwanji amesema kuwa Halamshauri inachokifanya ni kuwandaa wanawake kuwa na miradi mbalimbali ya kiuchumi kwa kuanzisha vikundi na kuwaunganisha katika taasisi za kifedha ambazo hutoa fursa za mikopo, mitaji, mafunzo na masoko.
“Wanawake wengi wanakuwa na unyonge hivyo kushindwa kujiamini hivyo kupitia mradi huu tunawajengea uwezo kwani wakiwa na uwezo wa kiuchumi watakuwa na uwezo wa kujiamini na kushiriki kwenye masuala mbalimbali ya kijamii ikiwa ni pamoja na kuwania nafasi za uongozi ndani ya jamii,”amesema Lwanji.
Naye mratibu wa mradi wa (WLER) Maria Nkangali amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwapa uelewa viongozi hao wa dini ili wakatoe elimu juu ya ushiriki wa wanawake katika uongozi kuleta maendeleo kwa wananchi.
Nkangali amesema kuwa wanatoa mafunzo hayo kwa makundi mbalimbali ili yatambue mchango wa wanawake na wasichana kwenye suala la maendeleo bila ya kujali jinsi.
Mafunzo hayo siku moja yamewahusisha Viongozi wa Dini kwenye Kata mbalimbali na wataalamu wa idara mbalimbali za Halmashauri hiyo.
Tuesday, July 9, 2024
YODAMEFO YAHITAJI MILIONI 10 UJENZI KITUO
SHIRIKA lisilokuwa la Kiserikali la (YODAMEFO) la Picha ya Ndege Wilayani Kibaha linahitaji kiasi cha shilingi milioni 10 kwa ajili ya kujenga kituo cha ufundi kwa vijana.
Saturday, July 6, 2024
WATUMISHI WA HALMASHAURI WATOA MISAADA MAKAO TISA YA WATOTO
WATUMISHI wa Halmashauri ya Mji Kibaha kwa kushirikiana na Watumishi wa Shirika la Elimu Kibaha pamoja na wadau wa maendeleo ikiwemo Benki ya CRDB wametoa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 4.2 kwa makao tisa ya vituo vya kulea yatima.
Friday, July 5, 2024
KPC YATAKA WATOTO KUJILINDA
MAREKANI YAADHIMISHA SIKU YA UHURU WAKE
Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe Dkt Michael Battle akitoa hotuba yake kwa Kiswahili jana jioni katika hafla ya kuadhimisha siku ya Uhuru wa Marekani maarufu kama Julai 4, katika makazi yake Oysterbay jijini Dar es salaam.
Julai 4 ndio siku kuu ya nchini Marekani, ikiadhimisha kupitishwa kwa Tamko la Uhuru mnamo Julai 4, 1776 na Rais Thomas Jefferson, alipottangaza kupatikana kwa uhuru wa koloni kumi na tatu za Marekani kutoka utawala wa Uingereza.
Umuhimu wa Julai 4 kwa Wamarekani unatokana na sababu kadhaa kuu. Katika siku hii, Kongresi yao ilipitisha rasmi Tamko la Uhuru, ambalo lilielezea matamanio ya koloni kuunda taifa tofauti lililo huru kutoka utawala wa Uingereza.
Tamko hilo la Uhuru lilikuwa alama ya uhuru kamili na demokrasia. Liliainisha misingi ya msingi ya uhuru, usawa, na kutafuta furaha, ambayo ina maana kubwa kwa maadili ya Marekani.
Kupitishwa kwa Tamko kuliweka msingi wa Vita vya Mapinduzi, hatimaye kupelekea kuanzishwa kwa Marekani kama taifa huru. Ushindi katika vita na mkataba wa amani uliofuata na Uingereza ulithibitisha Julai 4 kama tarehe muhimu katika historia ya Marekani.
Kwa Wamarekaniu, kuadhimisha siku ya Uhuru Julai 4 kumekuwa jadi ya muda mrefu, ikitia nguvu umoja wa kitaifa na uzalendo.
Siku hiyo huadhimishwa na sherehe mbalimbali, ikiwemo fataki, gwaride, matamasha, na mikusanyiko ya familia, ambayo huleta watu pamoja kusherehekea urithi wao wa pamoja.
Ingawa tarehe nyingine, kama vile kusainiwa kwa Katiba au kumalizika kwa Vita vya Mapinduzi, pia ni muhimu, Julai 4 ina umuhimu wa kipekee wakati ambapo koloni za Marekani zilichukua msimamo thabiti kwa uhuru wao. Siku hii tangu hapo imekuwa sikukuu ya kitaifa inayoheshimu misingi ya nchi na roho ya kudumu ya watu wake.
Thursday, July 4, 2024
UMAUKI WAPANDA MITI KWENYE MAENEO YALIYOCHIMBWA MCHANGA
Hayo yamesemwa na Meneja wa chama hicho Hay Mshamu wakati wa unzinduzi uliofanyika Mwendapole Kibaha.
Mshamu amesema kuwa chama kimeendelea na shughuli za kudhibiti uharibifu wa Mazingira unaotokana na sababu mbalimbali zikiwemo uchimbaji wa mchanga kiholela, ukataji wa miti hovyo na uharibifu wa vyanzo vya maji.
"Tulitekeleza mradi wa upandaji wa miti ya kivuli na matunda kuzunguka katika mipaka na katikati mwa eneo la shule ya Msingi Muungano,"amesema Mshamu.
Amesema kuwa mradi ambao umekamilika kwa 100 na sasa watoto wetu wananufaika na uwepo wa miti hiyo tumeendelea kufanva kazi mbalimbali rafiki wa mazingira hadi kufikia sasa.
Aidha amesema kuwa pia wanajihusisha na uvuvi, ufugaji wa nyuki lengo likiwa ni kulinda mazingira ili yawe salama na kurejesha uoto wa asili ambao umetoweka kutokana na uharibufu wa mazingira.
"Tunahitaji kiasi cha shilingi milioni 6.5 kwa ajili ya mradi wa kilimo cha matunda ya pasheni na papai ambapo tulianzisha kuanzia miche hadi kupanda lakini nguvu imeishia hapo huku tukihitaji kupata uzalishaji mzuri,"amesema Mshamu.
Kwa upande wake Kaimu Ofisa Kilimo Halmashauri ya Mji Kibaha Suzana Mgonja amesema kuwa chama hicho kinapaswa kutumia wataalam wa kilimo ili waweze kuzalisha kwa ubora.
Mgonja amesema kuwa wao wako tayari kushirikiana na wakulima ili kuhakikisha wanainuka na kulima kilimo bora na chenye manufaa siyo kilimo kisicho na tija.