Sunday, July 7, 2013

PIMENI MAENEO YA SHULE ILI YAPATE HATI MILIKI

Na John Gagarini, Kibaha
HALMASHAURI kote nchini zimetakiwa kupima maeneo ya shule ili kuepuka
kuvamiwa kwani hazina hati za kumiliki maeneo hayo kisheria na kuepuka
wavamizi.
Akizungumza wakati wa kufunga mashindano ya Umoja wa Michezo na
Taaluma kwa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) Waziri wa Tawala za
Mikoa n Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Hawa Ghasia alisema kuwa maeneo
mengi ya shule hayajapimwa.
Ghasia asliema kuwa anashangaa ni kwa nini halmashauri hazipimi maeneo
ya shule hivyo kuwa rahisi kuvamiwa na watu kwa ajili ya kuyatumia kwa
shughuli za kimaendeleo.
“Inashangaza kuona kuwa maeneo mengi ya shule hayajapimwa na
halmashauri zinaangali tu hali hii ni mbaya kwani mtu anaweza kuvamia
bila ya woga na kwa kuwa hakuna hati miliki hivyo ni rahisi kuichukua
ardhi ya shule,” alisema Ghasia.
Alisema kuwa maeneo hayo nayo yanapaswa kuwa na hati miliki kama
ilivyo umiliki wa watu binafsi au taasisi za serikali.
“Nawaomba wakurugenzi kutekeleza hili ili kuondoa uporwaji wa maeneo
ya shule kwani kwa sasa migogoro ni mingi baina ya mashule na wananchi
ambao wanavamia maeneo hayo,” alisema Ghasia.
Aidha alsiema kuwa halmashauri ziepukane na mawazo ya kuyatoa maeneo
hayo kwa wawekezaji kwa ajili ya kufanyia shughuli za biashara au
matumizi mengine.
“Maeneo kwenye halmashauri yako mengi kwa nini waone maeneo ya shule
ndiyo sehemu ya kuwekeza hilo ni kosa kama wanahitaji maeneo wapewe
maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji,” alisema Ghasia.
Alizitaka halmashauri kuyalinda maeneo ya shule ambayo yamekuwa
yakivamiwa na watu bila ya kuwa na woga wowote licha ya kuwa ni
kinyume cha sheria.
Mwisho.

Monday, July 1, 2013

TAPELI AWACHIMBISHA KABURI WATU, ATOWEKA NA SIMU ZAO NA KAMERA

Na John Gagarini, Kibaha
MTU mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Abdul Ramadhan (35) amewatapeli baadhi ya wakazi wa Kwa Mathias wilayani Kibaha mkoani Pwani kwa kuwachimbisha kaburi kisha kutoweka na kuwaachia kaburi tupu bila ya kuzikwa marehemu kama alivyowaomba azike ndugu yake.
Tukio hilo lilitokea juzi kwenye mtaa huo baada ya mtu huyo kufika hapo na kuomba kusaidiwa kumzika mfanyakazi wake ambaye alidai kuwa hana uwezo wa kumsafirisha kwani kwao ni mbali.
Mbali ya kuwachimbisha kaburi wakazi hao pia alifanikiwa kuwaibia simu mbili pamoja na kamera moja pamoja na kuacha deni kwenye vyakula ambavyo vilitumiwa na wachimba kaburi huku kingine kikiwa kimeandaliwa bila ya kuliwa.
Akielezea mkasa huo Ustaadhi wa Masjid Kadiriya uliopo Kwa Mathias Said Omary alisema kuwa mtu huyo alifika msikitini hapo na kukutana na kiongozi kasha kuomba kuwa asaidiwe kuzikiwa mfanyakazi wake, msikiti ukamkubalia na taratibu zikaanza kufanyika.
Omary alisema kuwa baada ya kuelekezwa na mkuu wake alitakiwa ashughulikie suala hilo na kwenda na mtu huyo kwenye makaburi ya mambo akiwa na watu wengine watatu kwa ajili ya kuchimba kaburi kwa ajili ya kumsitiri marehemu.
“Tulikwenda makaburini na wachimbaji wakaanza kazi ya kuchimba kaburi akawaletea chain a maandazi 20 wakanywa wakaendelea na kazi yao mimi akaniambia twende hospitali ya Tumbi aliko marehemu kwa ajili ya kumwandaa,” alisema Omary.
Alisema wakiwa njiani alimwambia kuwa anaomba simu yake ili awasiliane na ndugu zake kwani ya kwake imeisha chaji pia amtafutie mpiga picha kwa ajili ya tukio hilo kwa ajili ya kuwaonyesha ndugu juu ya mazishi hayo.
“Tulikwenda kwa mpiga picha wakakubaliana apige picha akasema kabla ya kwenda Tumbi wakachukue nyama na vitu vingine kwa ajili ya msiba huo na walipofika Maili Moja wakachukua nyama kilogramu 25 na,”alisema Omary.
Aliongeza kuwa  wakati wameshapima nyama aliwaambia ngoja akanunue viungo vingine lakini hakurudi tena na kutoweka kusikojulikana huku kaburi likiwa limeshachimbwa na liko wazi hadi sasa.
Kwa upande wake mpiga picha Jum Said ambaye yeye aliibiwa kamera na simu alisema kuwa walikubaliana apige picha 36 hadi 40 ambazo gharama yake ni sawa na shilingi 36,000 au 40,000.
Alisema wakati wako kwenye harakati ya kunua nyanya alimwachia begi likiwa na kamera na simu lakini aliporudi hakumkuta akiwa yeye na Ustaadhi na dereva wa teksi ambayo aliikodisha kwa shughuli za mazishi hayo.
“Alituacha mimi na ustaadhi tukiwa na nyama huku tukimsubiria hali amabyo ilitufanya tuingie matatani kwani wauzaji nyama ilibidi watubana ndipo tulipowaelewesha juu ya hali halisi ndiyo ikawa salama kwetu na kuondoka,” alisema.
Watu waliokumbwa na hali hiyo walisema kuwa mbali ya kudanganya mambo yote hayo pia aliweka oda ya chakula sahani 20 kwenye hoteli lakini hakuonekana tena, katika kufuatilia walibaini jina la mtu huyo kwani siku moja kabla ya tukio hilo alilala kwenye nyumba ya kulala wageni ya Iwawa iliyopo mtaa wa Kwa Mbonde jirani na hapo wakazi hao walitoa taarifa kwenye kituo cha polisi Kwa Mathias juu ya tukio hilo.
Mwisho.

Friday, June 7, 2013

SUMATRA KUDHIBITI MADEREVA PWANI

Na John Gagarini, Kibaha
MAMLAKA ya Udhibiti wa usafiri Majini na Nchini Kavu (SUMATRA) imefungua ofisi yake mkoani Pwani na kuwataka wananchi kutoa taarifa za mabasi yanayokatisha ruti na kutotoa tiketi kwa abiria.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ofisa mwandamizi wa SUMATRA wa mkoa Iroga Nashoni alisema kuwa abiria wanapaswa kukitumia chombo hicho ili kuondoa kero kwa wasafiri.
Iroga alisema kuwa ofisi hiyo imefunguliwa mwezi uliopita kwa lengo la kusogeza huduma kwa wateja wao ambapo inaendelea kujitanua kwenye mikoa, mingine ikiwa ni Singida, Iringa, Musoma na Rukwa.
Alisema kuwa changamoto kubwa waliyoiona ni mabasi mengi ya abiria kushindwa kumalizia safari zao Kukatisha Ruti) na kutotoa tiketi kwa abiria jambo ambalo ni kinyume cha sheria ambapo watawapiga faini hata ikibidi kuwafungia leseni madereva watukutu.
“Changamoto hiyo inakuwa kubwa kutokana na abiria wengi kutokuwa na elimu ya kujua haki zao za msingi wanapokuwa wanasafiri hivyo kuwapa mwanya madereva kufanya watakavyo,” alisema Iroga.
Aliongeza kuwa wataendelea kutoa elimu kwa pande zote ikiwa ni pamoja na abiria, madereva na wamiliki wa mabasi hayo ili waweze kufuata sheria bila ya kushurutishwa.
“Jana tulifanya operesheni kukamata magari yenye makosa mbalimbali ambapo magari manne yamekutwa na makosa na kupigwa faini kutegemea na makosa,” alisema Iroga.
Alibainisha kuwa wataendelea kufanya operesheni za kushtukiza za mara kwa mara ili kukabiliana na madereva wengi kukiuka sheria za barabarani na kuwataka wananchi kutoa taarifa na si kulalamika bali wachukue hatua.
Mwisho.

MBUNGE AMWAGA VIFAA TIMU YA UMISSETA

Na John Gagarini, Kibaha
MBUNGE wa Jimbo la Kibaha mkoani Pwani Silvestry Koka ametoa seti za
jezi kwa timu za mpira wa pete na soka za mkoa huo zinazojiandaa na
mashindano ya Umoja wa Michezo na Sanaa kwa Shule za Sekondari
Tanzania (UMISSETA) Kanda ya Mashariki inayotarajiwa kutimua vumbi
hivi karibuni mjini Kibaha.
Jezi hizo zimekabidhiwa kwa timu hiyo na mke wa mbunge huyo Selina
Koka kwenye kambi ya timu hiyo iliyopo kwenye shule ya Filbert Bayi
iliyopo wilayani Kibaha.
Mbali ya jezi hizo pia timu ya mkoa iliahidiwa kupatiwa mipira ya
michezo hiyo, mchele, kilogramu 100, mafuta ya kupikia, maji na sukari
pamoja na kumkabidhi mwalimu wa timu hiyo Loyd Mgombele kiasi cha
shilingi 100,000 kwa ajili ya shughuli za kuratibu timu hiyo.
Akiwakabidhi manahodha wa timu ya mpira wa pete na mpira wa miguu Koka
alisema kuwa lengo la kutoa vitu hivyo ni kuhamasisha timu hiyo ili
iweze kufanya vizuri kwenye michezo yake dhidi ya mkoa wa Morogoro ili
kuunda timu ya Kanda.
Koka alisema kuwa mkoa wa Pwani ni wenyeji wa mashindano hayo
wanapaswa kuwa na maandalizi mazuri ili kuweza kuwakilisha vema mkoa
na baadaye Taifa ambapo michuano hiyo itafanyika kwenye viwanja vya
Shirika la Elimu Kibaha Tumbi.
Aliwataka wachezaji hao kujituma kuzingatia yale wanayofundishwa na
walimu wao ili kuhakikisha wanafanya vyema na kutoa wachezaji wazuri
ili kuunda timu ya Kanda inayoundwa na mikoa ya Pwani na Morogoro.
Kwa upande wake ofisa elimu taaluma mkoa wa Pwani Godwin Mkaruka
ambaye aliwakilisha mkoa huo alisema kuwa ana mpongeza mbunge huyo kwa
kuisaidia timu ya mkoa ili iweze kuwakilisha vema mkoa huo.
Aliwataka wadau mbalimbali kujitokeza kuisaidia timu hiyo kwa hali na
mali kama alivyojitolea Mbunge huyo ili iweze kuuletea mkoa ushindi
katika michuano hiyo ambayo hufanyika wilayani humo kila mwaka.
Mwisho.
3 attachments — Download all attachments   View all images   Share all images  
E89A0881.jpgE89A0881.jpg
1311K   View   Share   Download  
E89A0882.jpgE89A0882.jpg
1162K   View   Share   Download  
E89A0874.jpgE89A0874.jpg
1

WANAFUNZI WATAKIWA KULALA ILI WASISIKILIZE WENZAO WAKIFUNDIHSWA

Na John Gagarini, Bagamoyo
SHULE ya Msingi Ludiga wilayani Bagamoyo mkoani Pwani inakabiliwa na uhaba wa madarasa hali ambayo inasababisha baadhi ya wanafunzi wa madarasa mawili kusoma chumba kimoja cha darasa huku wengine wakitakiwa kulala ili wasisikilize wanachofundishwa wenzao.
Akizungumza mbele ya mbunge wa Jimbo la Chalinze Said Bwanamdogo alipotembelea Kijiji cha Talawanda kata ya Talawanda, mwalimu mkuu  msaidizi wa shule hiyo Selestin Casian alisema kuwa shule hiyo ina madarasa matatu tu.
Casian alisema kuwa mbali ya wanafunzi wa madarasa mawili kusomea chumba kimoja pia wanafunzi wengine husomea nje kwenye miti kutokana na upungufu huo wa vyumba vya madarasa.
“Inabidi tuwaambie wanafunzi wa darasa moja walale ili wasisikilize kinachofundishwa na mwalimu ambaye yuko darasani hasa pale mwalimu mwingine anapokuwa bado hajaingia,” alisema Casian.
Aidha alisema kuwa licha ya shule hiyo kuwa na mwaka wa 10 sasa tangu kuanzishwa kwake shule hiyo ina walimu watano ambapo ina jumla ya wanafunzi 320.
“Kwa kweli tunachangamoto kubwa ya madarasa hali ambayo inasababisha wanafunzi kutopatiwa elimu ipasavyo hivyo tunaiomba halmashauri kutusaidia ili tuweze kuepukana na adha hii kwani wanafunzi wanashindwa kusoma vema,” alisema Casian.
Kwa upande wake mbunge wa Bwanamdogo alisema kuwa atapeleka suala hilo halmashauri ili iweze kutatua changamoto hiyo ambayo inakabili baadhi ya shule za Jimbo hilo.
“Changamoto ya madarasa na walimu ni kubwa katika Jimbo la Bagamoyo, lakini kama mnavyojua tatizo kubwa ni fedha kwani halmashauri yetu haina fedha za kutosha hata hivyo tutaendelea kuhimiza ujenzi kwa kushirikiana na wananchi,” alisema Bwanamdogo.
Aliitaka jamii kujitolea kwenye ujenzi wa madarasa na si kuisubiri serikali kwani nayo inakabiliwa na mambo mengi ya kimaendeleo hivyo wahimizane kuchangania kujenga madarasa.
Mwisho.

    

Sunday, May 26, 2013

DKT AISHI CHUMBA CHA KUZALISHIA



Na John Gagarini, Bagamoyo
 WANANCHI wa Kijiji cha Msinune kata ya Kiwangwa wilayani Bagamoyo mkoani Pwani wameiomba serikali kuwasaidia kujenga nyumba ya mganga ambaye anaishi kwenye chumba cha kuzalishia kwenye zahanati ya kijiji hicho.
Akizungumza mbele ya mbunge wa Jimbo la Chalinze Said Bwanamdogo wakati wa kikao cha Halamshauri ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Kiwangwa, mwenyekiti wa Kijiji hicho Kesi Hassan alisema mganga huyo inabidi afanye hivyo kutokana na kukosa nyumba.
Hassan alisema kuwa mganga pamoja na muuguzi wanatumia wanaishi humo kutokana na uhaba wa nyumba za watumishi katika kijiji hicho.
“Tunaiomba serikali na kwa kupitia kwako kutusaidia ujenzi wa nyumba za watumishi kwani kutumia chumba kinyume na matumizi si sawa na haipendezi mazingira ni magumu,” alisema Hassan.
Aidha alisema kuwa watumishi wengi hawana nyumba za kuishi hivyo kuwapa wakati mgumu katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku ya kuwahudumia wananchi.
“Suala la nyumba za watumishi ni changamoto ambayo inatukabili hivyo ni vema kukawa na nguvu ya ziada kutoka juu ili kutusaidia watumishi wetu waweze kukaa kwenye mazingira mazuri.
Kwa upande wake Bwanamdogo alisema kuwa suala hilo amelipata na ataangalia jinsi gani ya kuweza kulifanyia kazi ili mganga huyo na watumishi wengine waweze kuweza kuwa na nyumba.
Bwanamdogo aliwataka viongozi na wananchi kwenye vijiji vya Jimbo hilo kujitolea kwa kutumia nguvu zao ili kuanzisha ujenzi wa nyumba za watumishi na ofisi yake itachangia.
Mwisho.

DKT AISHI CHUMBA CHA KUZALISHIA



Na John Gagarini, Bagamoyo
 WANANCHI wa Kijiji cha Msinune kata ya Kiwangwa wilayani Bagamoyo mkoani Pwani wameiomba serikali kuwasaidia kujenga nyumba ya mganga ambaye anaishi kwenye chumba cha kuzalishia kwenye zahanati ya kijiji hicho.
Akizungumza mbele ya mbunge wa Jimbo la Chalinze Said Bwanamdogo wakati wa kikao cha Halamshauri ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Kiwangwa, mwenyekiti wa Kijiji hicho Kesi Hassan alisema mganga huyo inabidi afanye hivyo kutokana na kukosa nyumba.
Hassan alisema kuwa mganga pamoja na muuguzi wanatumia wanaishi humo kutokana na uhaba wa nyumba za watumishi katika kijiji hicho.
“Tunaiomba serikali na kwa kupitia kwako kutusaidia ujenzi wa nyumba za watumishi kwani kutumia chumba kinyume na matumizi si sawa na haipendezi mazingira ni magumu,” alisema Hassan.
Aidha alisema kuwa watumishi wengi hawana nyumba za kuishi hivyo kuwapa wakati mgumu katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku ya kuwahudumia wananchi.
“Suala la nyumba za watumishi ni changamoto ambayo inatukabili hivyo ni vema kukawa na nguvu ya ziada kutoka juu ili kutusaidia watumishi wetu waweze kukaa kwenye mazingira mazuri.
Kwa upande wake Bwanamdogo alisema kuwa suala hilo amelipata na ataangalia jinsi gani ya kuweza kulifanyia kazi ili mganga huyo na watumishi wengine waweze kuweza kuwa na nyumba.
Bwanamdogo aliwataka viongozi na wananchi kwenye vijiji vya Jimbo hilo kujitolea kwa kutumia nguvu zao ili kuanzisha ujenzi wa nyumba za watumishi na ofisi yake itachangia.
Mwisho.