Na John Gagarini, Kibaha
HALMASHAURI kote nchini zimetakiwa kupima maeneo ya shule ili kuepuka
kuvamiwa kwani hazina hati za kumiliki maeneo hayo kisheria na kuepuka
wavamizi.
Akizungumza wakati wa kufunga mashindano ya Umoja wa Michezo na
Taaluma kwa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) Waziri wa Tawala za
Mikoa n Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Hawa Ghasia alisema kuwa maeneo
mengi ya shule hayajapimwa.
Ghasia asliema kuwa anashangaa ni kwa nini halmashauri hazipimi maeneo
ya shule hivyo kuwa rahisi kuvamiwa na watu kwa ajili ya kuyatumia kwa
shughuli za kimaendeleo.
“Inashangaza kuona kuwa maeneo mengi ya shule hayajapimwa na
halmashauri zinaangali tu hali hii ni mbaya kwani mtu anaweza kuvamia
bila ya woga na kwa kuwa hakuna hati miliki hivyo ni rahisi kuichukua
ardhi ya shule,” alisema Ghasia.
Alisema kuwa maeneo hayo nayo yanapaswa kuwa na hati miliki kama
ilivyo umiliki wa watu binafsi au taasisi za serikali.
“Nawaomba wakurugenzi kutekeleza hili ili kuondoa uporwaji wa maeneo
ya shule kwani kwa sasa migogoro ni mingi baina ya mashule na wananchi
ambao wanavamia maeneo hayo,” alisema Ghasia.
Aidha alsiema kuwa halmashauri ziepukane na mawazo ya kuyatoa maeneo
hayo kwa wawekezaji kwa ajili ya kufanyia shughuli za biashara au
matumizi mengine.
“Maeneo kwenye halmashauri yako mengi kwa nini waone maeneo ya shule
ndiyo sehemu ya kuwekeza hilo ni kosa kama wanahitaji maeneo wapewe
maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji,” alisema Ghasia.
Alizitaka halmashauri kuyalinda maeneo ya shule ambayo yamekuwa
yakivamiwa na watu bila ya kuwa na woga wowote licha ya kuwa ni
kinyume cha sheria.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment