Friday, July 19, 2013

AMUUA MWANAMKE MWENZAKE KISA WIVU WA MAPENZI



Na John Gagarini, Kibaha
TATU Abdala (37) mkazi wa wilaya ya Rufiji mkoani Pwani anashikiliwa na jeshi la polisi tuhuma za kumchoma kisu na kumwua mwanamke mwenzake kwa madai kuwa alikuwa akitembea na mume wake Omary Abdala ambaye waliacha naye mwaka mmoja uliopita.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamimu kamanda wa Polisi mkoani Pwani Kamishana msaidizi wa Jeshi hilo Yusuph Ally alisema kuwa marehemu alichomwa kisu hicho tumboni.
Ally alisema kuwa chanzo cha mauaji hayo kinatajwa kuwa ni wivu wa kimapenzi baada ya kubaini kuwa mume wake wa zamani alikuwa na mahausiano ya kimapenzi na marehemu baada ya wao kuachana.
“Mtuhumiwa huyo alitalakiana na mumewe ambaye walizaa naye watoto watano naalipata taarifa ya mtalaka wake
kujenga mahusiano ya kimapenzi na marehemu Hajra kisha kumfuata
marehemu huyo nyumbani kwake na kumchoma kisu tumboni,” alisema Ally.

Ally alibainisha kuwa mtuhumiwa alipata
urahisi wa kutenda tukio hilo  kutokana na kuishi eneo la jirani na marehemu.

Aidha alisema mara baada ya tukio hilo marehemu alikimbizwa kituo cha afya cha
Muhoro na kabla ya kupatiwa matibabu alifariki dunia.
Aliongeza kuwa Mtuhumiwa
alikamatwa na polisi kujibu mashtaka yanayomkabili.
Mwisho

No comments:

Post a Comment