Friday, June 7, 2013

MBUNGE AMWAGA VIFAA TIMU YA UMISSETA

Na John Gagarini, Kibaha
MBUNGE wa Jimbo la Kibaha mkoani Pwani Silvestry Koka ametoa seti za
jezi kwa timu za mpira wa pete na soka za mkoa huo zinazojiandaa na
mashindano ya Umoja wa Michezo na Sanaa kwa Shule za Sekondari
Tanzania (UMISSETA) Kanda ya Mashariki inayotarajiwa kutimua vumbi
hivi karibuni mjini Kibaha.
Jezi hizo zimekabidhiwa kwa timu hiyo na mke wa mbunge huyo Selina
Koka kwenye kambi ya timu hiyo iliyopo kwenye shule ya Filbert Bayi
iliyopo wilayani Kibaha.
Mbali ya jezi hizo pia timu ya mkoa iliahidiwa kupatiwa mipira ya
michezo hiyo, mchele, kilogramu 100, mafuta ya kupikia, maji na sukari
pamoja na kumkabidhi mwalimu wa timu hiyo Loyd Mgombele kiasi cha
shilingi 100,000 kwa ajili ya shughuli za kuratibu timu hiyo.
Akiwakabidhi manahodha wa timu ya mpira wa pete na mpira wa miguu Koka
alisema kuwa lengo la kutoa vitu hivyo ni kuhamasisha timu hiyo ili
iweze kufanya vizuri kwenye michezo yake dhidi ya mkoa wa Morogoro ili
kuunda timu ya Kanda.
Koka alisema kuwa mkoa wa Pwani ni wenyeji wa mashindano hayo
wanapaswa kuwa na maandalizi mazuri ili kuweza kuwakilisha vema mkoa
na baadaye Taifa ambapo michuano hiyo itafanyika kwenye viwanja vya
Shirika la Elimu Kibaha Tumbi.
Aliwataka wachezaji hao kujituma kuzingatia yale wanayofundishwa na
walimu wao ili kuhakikisha wanafanya vyema na kutoa wachezaji wazuri
ili kuunda timu ya Kanda inayoundwa na mikoa ya Pwani na Morogoro.
Kwa upande wake ofisa elimu taaluma mkoa wa Pwani Godwin Mkaruka
ambaye aliwakilisha mkoa huo alisema kuwa ana mpongeza mbunge huyo kwa
kuisaidia timu ya mkoa ili iweze kuwakilisha vema mkoa huo.
Aliwataka wadau mbalimbali kujitokeza kuisaidia timu hiyo kwa hali na
mali kama alivyojitolea Mbunge huyo ili iweze kuuletea mkoa ushindi
katika michuano hiyo ambayo hufanyika wilayani humo kila mwaka.
Mwisho.
3 attachments — Download all attachments   View all images   Share all images  
E89A0881.jpgE89A0881.jpg
1311K   View   Share   Download  
E89A0882.jpgE89A0882.jpg
1162K   View   Share   Download  
E89A0874.jpgE89A0874.jpg
1

No comments:

Post a Comment