Saturday, December 14, 2024

VITENDO VYA UKATILI PWANI VYAPUNGUA










HUKU Tanzania ikiwa imehitimisha siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili matukio kwa Mkoani wa Pwani yamepungu kutoka matukio 8,573 mwaka 2023 na kufikia matukio 6,916 mwaka huu sawa na asilimia 19.3.

Hayo yamesemwa na Edna Kataraiya kutoka Ofisi ya Mipango na Uratibu Mkoa wa Pwani wakati wa kuhitimisha siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili kimkoa zilifanyika Kwa Mbonde Wilayani Kibaha.

Kataraiya amesema kuwa ofisi yake inashughulikia matukio yanayohusiana na matukio hayo kwa asilimia 40 huku matukio mengine asilimia 60 yanashughulikiwa na idara ya afya.

Kwa upande wake Polisi Kata ya ya Picha ya Ndege Ibrahim Makaruti amesema kuwa moja ya changamoto inayojitokeza ni baadhi ya wazazi kumalizana nyumbani pasipo kuyapeleka kwenye vyombo vya sheria.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Watu Wenye Ulamavu Tanzania (SHIVYAWATA) Kibaha Mjni Jabir Makasala alisema kuwa kutungwe sera ya kuwakopesha wazazi wenye watoto wenye ulemavu ili wafanye shughuli za ujasiriamali kwani wazazi hao hawana kipato chochote.

Naye Mkurugenzi wa African Talent Forum (ATF) Rosemery Bujash amesema kuwa wamekuwa wakitoa elimu ya kupinga vitendo vya ukatili kwa vijana wa makundi mbalimbali kupitia sanaa na michezo.

Akitoa salamu za taasisi ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA) Mariam Mnengwah amesema kuwa wao walitoa elimu iliyosaidia kuibua vitendo vya ukatili na kutoa msaada wa kisheria na msaada wa matibabu.





  

No comments:

Post a Comment