TAASISI ya Anjita Child Development Foundation iliyopo Halmashauri ya Mji Kibaha imeomba wadau wa kupinga ukatili kushirikiana ili kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye jamii.
Akizungumza wakati wa kuhitimisha siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia Mkurugenzi wa Taasisi hiyo ya Anjita Janeth Malela amesema kuwa ili kufikia hatua ya kupunguza matukio hayo lazima watu, taasisi na mashirika waungane kukabili vitendo hivyo.
Malela amesema kuwa kabla ya kufikia hitimisho la siku hizo 16 za kupinga ukatili walitoa elimu kwa jamii juu ya kukabiliana na vitendo hivyo ambapo jamii imepata uelewa kwani wamejengewa uwezo.
"Tumetoa elimu hiyo na imeonyesha kuwa ndani ya jamii bado matukio kama hayo yanajitokeza hivyo tumewapatia uelewa na namna ya kuripoti mara waonapo matukio kama hayo ili hatua stahiki zichukuliwe,"amesema Malela.
Amesema kuwa ili kupunguza au kutokomeza vitendo hivyo lazima wadau waungane kwa pamoja kwa kutoa elimu kwa jamii ili kukabili vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Taasisi ya Anjita inashughulisha zinazohusiana na watoto na vijana pia kundi la watu wazima kupitia elimu ya malezi changamshi kwa wazazi na walezi kupitia mradi wa Mtoto Kwanza.
Katika kuhitimisha kilele hicho cha siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili Taasisi ya Anjita ilipewa cheti cha pongezi na ófisi ya mkuu wa Mkoa wa Pwani cha kushiriki kikamilifu katika kutoa elimu ya kupambana na ukatili wa kijinsia maeneo mbalimbali ya Mji wa Kibaha.
No comments:
Post a Comment