Lydenge ameeleza wakiwa kwenye maadhimisho ya kupinga siku 16 za ukatili wa wanawake na wasichana, wana mtandao wa Polisi wanawake Wilaya ya Kipolisi Chalinze waliona wafike kwenye gereza la Kigongoni ili kutoa msaada huo kwa wanawake wanaotumikia adhabu ya kifungo wakiwa na imani kuwa watabadilika kimatendo na kuwa mfano wa kuigwa watakapokuwa wamemaliza kutumikia adhabu zao.
Miongoni mwa vitu vilivyokabidhiwa leo ikiwa ni mwendelezo wa kusaidia makundi yenye uhitaji kwenye Jamii ni pamoja na Cherehani moja, mafuta ya kupaka, taulo za kike pamoja na sabuni za kufulia na kuogea.
Aidha, Lydenge ameomba uongozi wa gereza kupokea Cherehani hiyo na ikatumike kwenye kuwafundisha wanawake waliopo gerezani ili wakitoka wawe na ujuzi wa kazi ya kufanya.
Akipokea msaada huo Mrakibu Msaidizi wa Magereza Kaziro Ambros kwa niaba ya Mkuu wa gereza hilo amewashuku mtandao mtandao wa Polisi wanawake Wilaya ya Kipolisi Chalinze na kuahidi Cherehani iliyopokewa itatumika kwa lengo kusudiwa kwa kutumika kama nyenzo ya kufundishia ushonaji kwa wafungwa wanawake ili kuweza kuwajenge uwezo kwenye eneo la ushonaji.
No comments:
Post a Comment