Lyimo akizungumza na mwandishi wa habari hizi amesema kuwa hilo ndiyo jambo ambalo ni kipaumbele chake mara baada ya kuchguliwa kwenye uchaguzi wa serikali za mita uliofanyika hivi karibuni na yeye kushinda nafasi hiyo.
Amesema kuwa eneo tayari wanalo wanachofanya ni kuwaandikia wadau wa maendeleo kwenye mtaa huo kwa kushirikiana na wananchi kufanya ujenzi huo ambao ni ndoto yake kuhakikisha mkakati wa kuwa na ofisi unafanikiwa.
“Mpango mkakati wa mtaa kwa sasa ni kuwa na ofisi yake badala ya kutumia ofisi za watu wengine tunataka tuwe na ofisi yetu wenyewe ili tufanye kazi kwa uhuru badala ya kutegemea wengine kwani kutumia ofisi za watu wengine kuna changamoto zake,”amesema Lyimo.
Aidha amesema kuwa anamatumaini ofisi itajengwa kutokana na ushirikiano anaoupata kutoka kwa wananchi na wadau wa maendeleo kwani anaamini ushirikiano huo utafanikisha kupatikana kwa ofisi ya mtaa huo.
“Nataka kwa kushirikiana wananchi na wadau kuhakikisha tunaacha alama ya uongozi kwa kujenga ofisi yetu kwani tukiwa na ofisi yetu tutakuwa na uhuru na tutajenga kutokana na mahitaji ya mtaa wetu ambapo itakuwa na vyumba kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi,”amesema Lyimo.
Amebainisha kuwa jambo lingine ambalo atahakikisha linafanyika ni kuwagawia wananchi eneo la kufanyiabiashara kwa ananchi wa mtaa huo ili waweze kupata huduma ya soko karibu kwani wanataka liwe soko dogo ili kuwaongezea wananchi kipato na kutoa huduma.
“Tunahitaji tuwe na eneo ambalo litakuwa kama soko ambapo wananchi watauza bidhaa zao badala ya kwenda mbali kufuata mahitaji yao nyumbani tunataka wapate hapa jirani na pia itakuwa ni sehemu ya kujiongezea kipato,”amesema Lyimo.
Lyimo alifanikiwa kushinda nafasi hiyo baada ya kumshinda aliyekuwa mwenyekiti wa Mtaa huo Lazaro Joseph ambaye aliongoza kwa vipindi viwili vya miaka 10 huku yeye akiwa ni mjumbe wa serikali ya mtaa huo ambapo alishindwa kwenye nasafi hiyo na mtangulizi wake mwaka 2019 na alikuwa ni mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania Kata ya Sofu na Mjumbe wa mtaa.
No comments:
Post a Comment