KATIKA kuhamasisha matumizi ya nishati safi na salama Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limewataka Watanzania kutumia Mkaa wa Rafiki Briquettes.
Hayo yamesemwa Mjini Kibaha na ofisa masoko wa (Stamico) Hope Mahokola wakati wa maonyesho ya Uwekezaji na Biashara ya Mkoa wa Pwani.
Mahokola amesema kuwa mkaa huo ni nishati safi na salama na una uwezo wa kuwaka kwa zaidi ya saa tatu baada ya kuwashwa.
"Tunamuunga mkono Rais Dk Samia Suluhu Hassan kuhamasisha matumizi ya nishati safi ili kulinda mazingira ili kutoharibu uoto wa asili ili usisababishe mabadiliko tabianchi hivyo Watanzania watumie mkaa wa Rafiki Briquettes ili kulinda mazingira,"amesema Mahokola.
Amesema kuwa mkaa huo unatolana na mabaki ya makaa ya mawe hauna moshi na ni safi na salama katika kupikia na unachangia kupunguza mabadiliko ya Tabianchi.
"Mkaa huu unaweza kutumika nyumbani, vyuoni, mashuleni na sehemu nyingine zenye uhitaji wa nishati ya kupikia,"amesema Mahokola.
Aidha amesema kuwa mkaa huo ni rafiki kwa matimizi, mazingira na gharama na mkaa huo unatokana na makaa ya mawe yanayochimbwa kwenye mgodibwa Kiwira-Kabulo Mkoani Songwe.
No comments:
Post a Comment