KIWANDA cha kuzalisha malighafi zitumikazo kwenye uzalishaji vyuma na mabati na usambazaji wa pikipiki cha Kinglion kinatarajia kutoa ajira kwa watu 1,500 ajira za kudumu na ajira za muda zaidi ya 5,000.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa wiki ya maonyesho ya Biashara na Viwanda ya Mkoa wa Pwani meneja wa kiwanda hicho Anold Lyimo amesema kuwa kiwanda hicho kitafunguliwa muda siyo mrefu.
Lyimo amesema kuwa mara kiwanda hicho kitakapoanza uzalishaji vijana wengi watapata ajira na kuongeza pato la Taifa kwani kitakuwa kiwanda kikubwa na kitauza bidhaa zake hadi nje ya Tanzania yaani nchi jirani.
"Kiwanda kilikuwa kianze uzalishaji mwaka huu lakini kuna changamoto kidogo ikiwa ni pamoja na barabara na gesi ambavyo serikali inavifanyia kazi ili kukabili changamoto hizo,"amesema Lyimo.
Aidha alisema kuwa wanatarajia kiwansa kitakapoanza kazi kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 35,000 kwa mwaka.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amesema kuwa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini Tanzania (TARURA) wataijenga barabara ya kuelekea kiwandani huko yenye urefu wa kilometa 2.5.
Kunenge amesema kuwa pia wanatarajia kusambaziwa gesi kwenye eneo la viwanda la Zegereni ikiwemo kwenye kiwanda hicho cha Kinglion.
No comments:
Post a Comment