Sunday, December 8, 2024

KIBAHA SHOPPING MALL YAZINDULIWA DC AWATAKA WANANCHI WASIENDE DAR ES SALAAM KILA KITU KIPO

MKUU wa Wilaya ya Kibaha Nickson John amezindua soko la kisasa (Kibaha Shopping Mall) lenye thamani ya shilingi milioni 8 ambalo litakuwa likiingizia Halmashauri ya Mji Kibaha kiasi cha shilingi milioni 660.7 kwa mwaka.

John amezindua soko hilo ambalo linamilikiwa na Halmashauri ya Mji Kibaha lipo kwenye eneo la kitovu cha Mji (CBD) amesema kuwa huo ni mradi wa kimkakati ambapo fedha za ujenzi zimetokana na fedha kutoka serikali kuu.

Amesema kuwa soko hilo ni mkombozi kwa wananchi wa Kibaha ambapo haitawalazimu kwenda Jijini Dar es Salaam kufuata bidhaa lakini bidhaa hizo zitakuwazikipatikana kwenye soko hilo ambalo limejengwa kwa miundombinu ya kisasa.

"Kuanzia sasa mtakuwa mnanunua hapa na hamtahitajika kufuata bidhaa Jijni Dar es Salaam hivyo mtapunguzagharama za nauli pamoja na muda ambao mneutumia kufuata bidhaa ambapo hapa zitapatikana kwa bei ya jumla na   rejereja",amesema John.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Dk Rogers Shemwelekwa amesema kuwa mradi huo umeshakamilika na umeanza kazi ambapo kwa sasa uko kwenye kipindi cha matazamio.

Shemwelekwa amesema kuwa soko hilo lina sehemu mbalimbali ikiwa ni pamoja maduka 63, super market moja, kumbi za benki mbili, Atm mbili, eneo la kuchezea moja ni ya chakula mawili, eneo la kuangalia michezo moja, ukumbi wa mikutano mmoja, maegesho ya pikipiki 50, taxi 10, magari 100 na bajaji 30.


mwisho.

No comments:

Post a Comment