Thursday, December 12, 2024

NMB YAKABIDHI VIFAA VYA KUJIFUNGULIA NA MASHUKA HOSPITALI YA WILAYA YA RUFIJI UTETE

BENKI ya NMB imetoa vifaa vya kujifungulia mama wajawazito seti 300 na mashuka 300 kwenye Hospitali ya Wilaya ya Rufiji Utete vyenye thamani ya shilingi milioni 12.3.

Aidha benki hiyo imetoa msaada huo ikiwa ni sehemu ya kumkumbuka mpigania Uhuru wa Tanzania Bibi Titi Mohamed kupitia tamasha la (Bibi Titi Mohamed Festival) linalofanyika kila mwaka.

Akipokea vifaa hivyo hospitalini hapo Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa ameishukuru benki hiyo kwa kutoa msaada huo.

Mchengerwa amesema kuwa benki hiyo imemuenzi mwasisi huyo ambaye pia ni Mbunge wa kwanza wa Rufiji na imeonyesha uzalendo kwa kuwasaidia wakinamama wajawazito kwenye hospitali hiyo ya Wilaya ya Utete.

No comments:

Post a Comment