SERIKALI imewagawia wananchi sehemu ya eneo waliolivamia kwenye Hifadhi ya Chemchem ya Maji ya Moto Wilayani Rufiji na kumaliza mgogoro baina ya wananchi na hifadhi hiyo.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge wakati akitoa tamko la kuhitimisha Mgogoro huo ikiwa ni Utekelezaji wa maazimio la Baraza la Mawaziri nane wa kisekta walioshughulikoa mgogoro huo ambapo Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele alisoma taarifa hiyo ya Mkuu wa Mkoa.
Kunenge alisema kufuatia wananchi hao kumegewa sehemu ya ardhi kutoka kwenye hifadhi hiyo aliwataka wananchi wanaozunguka maeneo hayo kutovamia tena eneo hilo.
"Naagiza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na Kamishna Msaidizi wa Ardhi kupima upya eneo hilo la Hifadhi na kuandaa GN mpya,"alisema Kunenge.
Aidha aliwataka TFS kuchonga Barabara kuzunguka eneo hilo ili Kuweka kinga ya mipaka kati ya wananchi na Hifadhi hiyo.
Katika hatua nyingine Mkoa umetoa taarifa ya kuhitimisha mgogoro wa ardhi kwenye eneo la Delta ya Mto Rufiji Wilayani Kibiti na kuwataka wananchi kutofanya shughuli za kibinadamu katika hifadhi ya Misitu ya Mikoko na mazalia ya samaki.
Akisoma taarifa ya Mkuu wa mkoa ambapo mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali Samwel Kolombo aliisoma amepiga marufuku ukataji wa Misitu ya Mikoko kwenye hifadhi hiyo ya Delta ya Mto Rufiji.
Alimtaka Mkurugenzi wa Halmshauri ya Kibiti kutoa elimu ya uhifadhi kwa wananchi na kuwawezesha vifaa vya kuvulia samaki kwenye maji marefu.
Alisisitiza pia kuanzisha kwa vikundi vya uhifadhi (BMU) ili kuimariasha ulinzi wa hifadhi hiyo ambayo ina mikoko mingi.
No comments:
Post a Comment