HALMASHAURI za Mkoa wa Pwani zimetakiwa kutenga bajeti kwa ajili ya shughuli za michezo ili kuinua vipaji vya vijana kwenye michezo.
Hayo yalisemwa Mjini Kibaha na Katibu Tawala wa Mkoa huo Rashid Mchata wakati akifunga mashindano Umoja wa Michezo na Sanaa kwa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) Mkoa wa Pwani.
Mchata alisema kuwa mbali ya bajeti pia Halmashauri zihakikishe kila shule inatenga eneo kwa ajili ya michezo ili wanafunzi wapate sehemu ya kucheza.
Naye ofisa michezo wa mkoa huo Grace Bureta alisema kuwa jumla ya wachezaji 120 wamechaguliwa kuunda timu ya Mkoa ambayo itashiriki mashindano ya Taifa yatakayofanyika mkoani Tabora ambapo timu hiyo imeiingia kambini kwenye shule ya sekondari Kibaha.
Naye mdau wa michezo Musa Mansour alisema kuwa kwa kuwa michezo ni ajira wadhamini waangalie kwa kuboresha upande wa zawadi ili ziwe kivutio kwa vijana kushiriki michezo.
No comments:
Post a Comment