Daraja linalounganisha mikoa ya Pwani na Dar es Salaam likiwa limejaa maji |
Baadhi ya wananchi wakifuatilia zoezi la uokoaji watu waliosombwa na maji ambao walipanda kwenye miti |
Moja ya kijana aliyenusurika Silas Moshi baada ya kusombwa na maji mara baada ya kuokolowa |
Dada ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja baada ya kuokolewa akiwa amepoteza fahamu akipakiwa kwenye gari la polisi kwa ajili ya huduma ya kwanza. |
Kijana Mohamed Kitindi aliyenusurika baada ya kusombwa na maji |
Furaha Mwaipopo moja ya watu walionusurika baada ya kusombwa na maji na kupanda kwenye mti |
Moja ya watu walionusurika akihojiwa na polisi baada ya kunusurika |
Kened Meshaki ambaye alishika nguzo ya bango huku mwili wake ukiwa ndani ya maji kwa zaidi ya masaa matatu akiwa ameshikwa mkono na polisi kwa ajili ya kwenda kupatiwa huduma ya kwanza |
Na John Gagarini,Kibaha
WATU saba wamenusurika kifo baada ya kusombwa na maji walipokuwa
wakijaribu kuvuka huku wakiwa wameshikana mikono ambapo walijinusuru kwa
kupanda kwenye miti kabla ya kuokolewa na kikosi cha Zimamoto na Uokoaji kwa
kushirikiana na Jeshi la Polisi mkoa wa Pwani.
Aidha kati ya watu hao mmoja alikuwa akininginia kwa
kujishika kwenye bomba la bango la matangazo huku mwili wake ukiwa ndani ya
maji kwa masaa zaidi ya huku akiwa anaomba msaada wa kuokolewa bila mafanikio.
Watu walionusurika ni pamoja na Kened Meshaki, Mohamed
Kitindi, Silas Moshi Henry Francis na mwanamke mmoj ambaye jina lake halikuweza
kufahamika mara moja ambao wote walikimbizwa hospitali ya Rufaa ya mkoa ya
Pwani.
Tukio hilo lilitokea jana eneo la Maili Moja wilayani Kibaha
kwenye daraja linalotenganisha kati ya mkoa wa Dar es Salaam na mkoa wa Pwani
na kusababisha daraja kujaa maji na kusababisha magari na watu kushindwa kuvuka
upande wa pili.
Daraja hilo ambalo linapita kwenye mto Mpiji lilikuwa
halipitiki na kusababisha watu na abiria kushindwa kuvuka upande wa pili kutoka
Maili Moja wilayani Kibaha na upande mwingine Kiluvya wilaya ya Ubungo.
Kutokana na daraja hilo kushindwa kupitika abiria wa mabasi
wameshindwa kuendelea na safari zao za kwenda mikoani na maeneo mengine yanayopita
kwenye barabara ya Morogoro.
Akizungumza na gazeti hili kwenye eneo la tukio hilo ofisa
habari na uhusiano wa Jeshi la uokoaji Harison Mkonyi alisema kuwa zoezi la
ukoaji limefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani wameweza kuwaokoa watu hao wakiwa
salama.
Mkonyi alisema kuwa wamefanikiwa kuwaokoa watu hao kwa
kushirikiana na wadau wengine ambao walijitosa kwenye maji hayo ambayo yalikuwa
mengi na kulifunika kabisa daraja hilo na kusababisha kushindwa kupitika.
“Tunawashukuru wadau mbalimbali vikiwemo vikosi vya majeshi
ya Polisi, Magereza, JWTZ na wananchi ambao walionyesha ushirikiano wa hali ya
juu kuwanusuru watu hao akiwemo mwanamke mmoja,” alisema Mkonyi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment