Thursday, October 19, 2017

AMUUA MWENZAKE KWA KUMCHONA NA VISU


Na John Gagarini, Kibaha

JESHI la Polisi Mkoani Pwani linamsaka Niniyay Silongoy kwa tuhuma za kumwua kwa kumchoma kisu Lemandra Kishwakwi (35) wote wa Kijiji cha Chamakweza wilaya ya Kipolisi Chalinze-Bagamoyo.
Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani Jonathan Shana alisema kuwa mtuhumiwa huyo alikimbia kusikojulikana baada ya tukio hilo.

Shana alisema kuwa tukio hilo lilitokea Oktoba 18 mwaka huu majira ya saa 11:30 jioni Kijijini hapo baada ya kuchomwa kisu hicho kwenye kwapa la kushoto na mtuhumiwa.

 “Mbali ya kuchomwa kwapani pia mtuhumiwa alimchoma kisu shingoni na mkono wa kulia na mtuhumiwa baada ya kutekeleza azma yake alikimbia na anatafutwa na jeshi hilo kufuatia tukio hilo,” alisema Shana.

Alisema kuwa chanzo cha mauaji hayo ni ulevi ndipo mtuhumiwa alipofanya mauaji hayo ya kusikitisha ambayo haikujulikana kwanini mtuhumiwa alifikia hatua hiyo ya kumchoma mwenzake kisu.

Aidha alisema kuwa mwili wa marehemu ulikabidhiwa ndugu kwa ajili ya mazishi baada ya uchunguzi wa daktari huku juhudi za kumtafuta mtuhumiwa zikiendelea.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment